!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Usiyo Yafahamu 😱🙆‍♀️Kuhusu Technical Analysis.Kwenye ulimwengu wa online Forex trading kuna mambo mengi sana ambayo trader yoyote mgeni lazima achanganyikiwe. Kwa kawaida huwa inachukua takribani mwaka mmoja hadi miwili kwa trader mgeni awe stable yaani experienced. Nature ya biashara hii ni kuficha sensitive information yaani tacktick za pro traders wanazotumia kutengeneza faida sokoni huwa zinafichwa na wengi hawakubali kuzionyesha hadharani bali kWa watu wachache sana anaowafundisha na kuwaamini.

Katika makala hii ya leo nawaletea mambo traders wengi wasiyoyafahamu kuhusu technical analysis na kwanini bado watu wengi wanachoma account Kila kukicha.

Sio kwamba Online Forex trading ni utapeli, Hapana. Industry is real but watu wanayoizunguka ndio wanaleta picha mbaya kwenye Industry. Hakuna namna utaweza kutajirika na Forex Trading Kwa haraka na ukiona mentor Instagram au kwenye mitandao ana hubiri falsafa hii inabidi ukae nae mbali. Hawa ndio wanaochafua industry.

Sasa kutokana na jopo kubwa la new traders kuaminishwa na hawa Fake Guru’s hii inawaathiri hata kwenye maendeleo ya wao wenyewe kwenye trading, Trader anajikuta anafukuzia upepo tu na miaka inaenda bila mafanikio na mwisho wa siku anasema Forex Trading is a Scam. Binafsi hua nasikitika sana nikona trader ana quit kwani hajui anakaribia ku uncover nini. Potential ni kubwa sana kama utaweza kuwa mvumilivu na process. Hakuna kitu kirahisi, hii ni biashara kama zilivyo biashara nyengine, utofauti wake ni kwamba hii hauzunguki juani kutafuta wateja bali hii unashinda kwenye screens ukijifunza na kutafuta fursa sokoni.

Asilimia 95% ya traders wapya huanza kujifunza technical analysis pindi tu anapoingia kwenye trading. Technical Analysis kwa lugha ya kiswahili ni “Uchambuzi Wa Kiufundi” Technical analysis ni rahisi sana hata ndani ya wiki unaweza ukawa umemaster kutrade kama una kichwa kinachonasa haraka. Hii hutumiwa sana na gurus wengi kuwanasa traders wapya kwani wengi wanaona ni rahisi. Hapa trader anaona kwanini nisikae mkao wa kula 😂.

Kumbe mambo hayaendi hivyo, Technical Analysis yaani Uchambuzi wa Kiufundi ni basic step kwenye safari ya kuwa Advanced Professional Trader. Kibaya zaidi trader huwekeza kila alichonacho bila kuwa na Usimamizi mzuri wa Fedha (Risk Management) kwenye elimu ya awali. Hii hupeleka idadi ya watu wanochoma account kukua kila mwezi.

Traders wengi wanafundishwa jinsi ya kuchora mistari tu eti wanategemea price itaheshimu mstari uliochora wewe 😥, Kwa kufanya hivi basi hutaweza kuona mafanikio. Biashara Ya Forex ina wahusika wakubwa sana ikiwemo Central banks, Hedge Funds N.K. Taasisi hizi zinawekeza pesa nyingi kwa akili sana hivyo usitegemee ki order chako ya 1 au 2 Lots kitaweza kuleta effect yeyote kwenye soko. Ndio maana usimamizi mzuri wa fedha ndio silaha yako. Hakuna mchambuzi anaefahamu uelekeo wa soko kila mchambuzi huwa na asilimia zake za uhakika wa uelekeo wa soko na haiwezi kufika 100%

Advanced Technical Trading, Fundamental Research Na Risk Management.

Hivi vitu vitatu ndio nuru na mwangaza kwako. Kama ulikuwa gizani basi leo kupitia platform hii ondoka na hivi vitatu ukavifanyie kazi kwa mwaka 2020. Psychology ya mjasiriamali aliyebobea inaweza kuelewa namaanisha nini. Iweke mindset yako sawa na uwe tayari kufight kuja at the Top. Haitakuwa rahisi kama unavyodhani ila ukifuata haya niliyokuambia basi utakuwa umepunguza zaidi ya nusu ya mihangaiko. Usiendelee kuhussle kwenye wrong direction, Kuwa tayari kubadilika na na kuyafanyia kazi mapungufu ulionayo.

Risk:Reward Ratio ni muhimu sana kwenye maisha ya forex trader. Nilipogundua hii dhana miaka kadhaa iliyopita ilinisaidia sana wakati wa drawdown. Trade moja inayowekwa huwa lazma iende angalau mara 8-12. Advanced technical trading huwezesha haya yote. Unapotrade Basic Technical analysis/Price Action mara nyingi reward huwa ni ndogo sana na kubwa niliyo ona ni 1:3/4. Ubaya wa hii ni kwamba unaweza ukaingia drawdown ya trade mpaka 5 mfululizo ukajikuta umekula mtaji na ikawa ngumu kurudi juu. Ila kama ulikuwa trader wa kuchukua 1:8 au 1:12 basi drawdown kama hizi zinapita salama na unasogea mbele.

Leo niishie hapa, Asante kwa kufika mwisho unaweza kujadili mjadala huu kwenye comment.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x