!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Unahitaji Muda Kiasi Gani Kuwa Profitable?

Hili swali limekuwa likiulizwa sana haswa na new traders wanaoanza career ya trading, wakati likiwa ni swali la kawaida kabisa ambapo new trader anatarajia kupata jibu lililonyooka kutoka kwa experienced trader, binafsi nimekuwa nikilikwepa sana kulitolea ufafanuzi kwa sababu jibu haliko constant.

Kila trader yuko tofauti na ninataka uelewe kwamba hili sio swali zuri sana kuuliza kwa sababu ukimuuliza mtu ambaye hana uelewa mzuri na trading anaweza akakupa timespan ambayo itakuweka kwenye mihemko na mwisho wa siku utakuwa disappointed. Kwa mfano ukiniuliza swali hili halafu nikakuambia mwaka mmoja tu unatosha, nina imani utafurahi sana lakini ukweli ni kwamba kila trader is built differently, yes nimekutana na traders waliofanikiwa kuwa profitable ndani ya miezi sita na wengine hadi miaka mitano cha kushangaza ni kwamba kila trader anastory yake ya kipekee na haziwezi kufanana hivyo kuuliza swali kama hili haliwezi kukusaidia sana zaidi ya kukuyumbisha kifikra.

Matokeo yake ni kuhamisha focus kutoka kwenye learning process yani what it takes to be profitable? kwenda kwenye when will I get to be profitable? Ukweli ni kwamba ukifocus kwenye what it takes to become profitable basi suala la “when” halichelewi hata kidogo changamoto ni kwamba karibu kila newbie anapoteza focus kwa kuuliza wrong questions kama hizi na kuishia kupotezwa kabisa na scams, inexperienced traders/mentors au watu wengine wanasemaje.

Kwa hiyo uzi wa leo utakuongoza direct kwenye maswali ya msingi ambayo new trader anatakiwa ajiulize ili abaki kwenye focus na kutokuyumbishwa.

Trader anatakiwa kufanya nini ili kuwa profitable?

Hili ni swali la msingi sana na muhimu kuliko title ya uzi huu. Nini haswa cha kufanya ili kuwa profitable?. Nafahamu ni ndoto ya traders wengi kufanikiwa hivyo maswali unayouliza lazima yaelekee kwenye kukujenga na si kukubomoa.

Huwezi kuwa profitable trader au kuwaza itakuchukua muda gani kuwa profitable kama hufahamu nini cha kufanya. Lazima ujifunze kutrade vizuri ndipo uanze kufikiria maswala ya kuwa profitable. Nimeandika masomo kadhaa yatakayokupa mwanga zaidi kwenye kujifunza trading vizuri.


Inachukua nini kuwa profitable trader?

(What does it take to become a profitable trader?)

Hili ni swali lengine unalotakiwa kujiuliza, kimsingi hili swali limejikita zaidi kwenye trading mentality/psychology pamoja na mindset.

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
hassan
hassan
6 months ago

Very informative. Asante sana kaka Ray!

Joshua
Joshua
6 months ago

Mungu awabariki Sana kwa elimu mnayotupa .Ahsanteni

Pages: 1 2

4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x