
UNAFIKIRIA KUKATA TAMAA TRADING? SOMA HII KWANZA.
Acha kutrade kwa kipindi kifupi au punguza risk
Kama unaona hasara zimezidi hauoni mwanga wowote basi unaweza uka simamisha kutrade live kwa muda flani ukahamia kwenye demo mpaka pale utakapo ona hali hiyo imepungua. Anza kwa kukagua matokeo au history yako ya trading kagua kila trade unayochukuwa kama unafuata sheria zako za trading ipasavyo kama una zifuata zote elewa kuna vipindi ambavyo hali ya soko hubadilika ukilinganisha na strategy yako ilivyo hivi vipindi vikitokea kwangu huwa na punguza risk hapa ndipo umuhimu wa usimamizi mzuri wa fedha unajitokeza. Hivyo ukiona hasara za mfululizo zisizo za kawaida kwako unaweza ukatumia mbinu hii yakuhamia kwenye demo mpka mambo yakianza kurudi sawa.
Soma vitabu au sikiliza interview za watu waliofanikiwa na trading.
Kama bado hujaweza kutengeneza faida endelevu au upo kwenye drawdown mbaya unaweza ukaanza kufikiri kwamba hakuna mtu anayeweza kutengeneza faida endelevu sokoni na hata hii trading ni bahati na sibu au haiwezekani kabisa kuwa kazi yenye tija. Muda huu ndio watu wengi hukata tamaa na kuacha trading hivyo ni vyema ukiwa kwenye vipindi kama hivi usome vitabu au kusikiliza interview za traders waliofanikiwa ili ubaki na mtazamo chanya na biashara hii. Unaweza ukaanza kusoma kitabu cha MARKET WIZARDS by Jack D. Schwager na kisha The complete turtle trader by michael covel.
Ondoa dhana ya kutajirika haraka
Mimi na hao wote uliowai kuwasikia wamefanikiwa na trading jua kabisa wamepitia changamoto nyingi na bado wanaendelea kuzipitia changamoto mpya kila siku. Huwezi kulala ukaamka kesho wewe ni mbobezi wa fani hii inachukuwa muda hivyo hata mafanikio huja hatua kwa hatua na kuchukuwa muda mrefu.
HITIMISHO
Nakuomba uelewe hakuna kitu kama “forex trading sio kwa ajili yangu nikwa ajili ya watu fulani wenye uwezo wakipeke”. Ata kama kwa sasa mambo hayaendi vizuri haimaanishi basi mwakani itakuwa hivyo au baada ya miaka mitatu itakuwa hivyo. Napenda nikuache na huu msemo wa kizungu “winners never quit and quiters never win” ukimaanisha washindi kamwe hawakati tamaa na wanao kata tamaa kamwe hawashindi. Shukrani sana kwa usomaji wako napia nakutakia kila la kheri kwenye trading yako usisahau ku comment “NEVER GIVE UP” chini hapa, hadi ijumaa ijayo kwakheri.
Sponsored Learn More
Dah bro always u’re make me to feel proud to join with a community…..u’re words give me a power of continue hustling in this game inspite am in a circle of lossing money…but still i never give up no matter what….Be blessed bro
Never give up. Thanks for the insight mok
NEVER GIVE UP
NEVER GIVE UP AT ALL …..!!!!!!!!!!!!!!
NEVER GIVE UP