!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

True Story: Shuhudia $1000 Ilivyopotea Ndani Ya Siku Tano.Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo

Kutana na Jayson, Jayson ni trader aliyenitumia message kwenye mtandao wa piptwitz.com akiwa na huzuni ya kuchomewa account yake ya $1000 ndani ya siku tano na trader aliyekutana nae Telegram. $1000 kupotea ndani ya wiki is no joke japo ina uwezo wa kupotea hata ndani ya saa chache tu lakini yote hayo huashiria kuna uzembe au ulimbukeni wa hali ya juu kwa mtu aliyefanya tukio hilo.

Ikiwa $1000 ndio mtaji basi ni lazima trader afahamu kwamba risk amount per trade ni 1% au half % . Kama professional trader huwa sifurahishwi na watu wenye tabia hizi hasa kwa wanafunzi wangu. Sasa, kulingana na Jayson, trader aliyemkabidhi account aliweka lot size nzito sana kiasi cha account kushindwa kuhandle mikiki ya soko. Lot ya 1 au 1.5 ni kubwa sana na kama unatrade pair kama Eur/usd 1 pip ni sawa na $10 au $15. Ndiyo maana asilimia 34 ya account ilichoma ndani ya lisaa limoja.

Uhalisia ni kwamba risk amount ya account yenye $1000 ni $5 na $10 maximum. Anything above that threshold ni over risking na ni hatari kwa usalama wa account yako. Haijalishi wewe ni expert kiasi gani sometimes masoko hayaendi vizuri na kitakacho kuokoa ni kurisk kiasi kidogo mara kwa mara.

Hadi kufikia Ijumaa Jayson alibakiwa na $30 kwenye account yake. Sasa, inawezekana Jayson akawa na uwezo wa kudeposit tena na kujifunza kutokana na haya makosa lakini kuna watu wasio na uwezo wa kudeposit tena pengine ni savings zake zote.

Somo kubwa tunayopata hapa ni mawili..

Usikubali kufanyiwa Account Management, jifunze skill ya trading mwenyewe kwani unaweza ukawa account manager wa account yako mwenyewe na ukawa profitable. Kama huna muda wa kujifunza basi kumkabidhi mtu account yako uliyekutana naye mtandaoni ni risk na kama you are willing to take the risk then go ahead.

Tumia Risk Management na Siku zote kumbuka kulinda the downside kabla hujafikiria kupata faida. Ni rahisi kurecover kwenye hasara kama unatumia risk management ila ukishachoma account ni ngumu sana kurecover na itakubidi uingie mfukoni tena kuweka mtaji.

I hope umejifunza kitu, weka comment yako chini kama umewahi kukumbana na changamoto hizi za account management.

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
setisfx
setisfx
5 months ago

Aisee mimi walishawahi kunitapeli $800 yangu iliniuma sana.

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x