!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

TOA FAIDA MARA KWA MARA KWENYE AKAUNTI YAKO YA TRADING.

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Nilipoanza biashara ya Trading 2016 nilikua na taswira yakujifunza trading niweze kukuza akaunti yangu iwe kubwa kwa kudunduliza faida siku hadi siku, na huwa ndivyo brokers watakwambia kwenye seminar zao zamafunzo kwasababu ukweli ni kwamba nia yao uendelee kuwepo kila siku watengeneze mapato.

Takwimu zinaonesha asilimia 97 ya retail traders ambao hupata faida kubwa mwishowe huishia kurudisha na kupoteza faida zote.

Mimi pia nilikua muhanga wa hili jambo kupata faida kubwa na kuzirudisha zote sokoni kwa kupata hasara. Wapo watakaosema “wilbroad ulikua hauko makini ndiomaana ulikua ukirudisha faida zote sokoni”. Elewa Unapo pata faida kubwa sokoni kutokana na mabadiliko makubwa ya bei, hii utokana na halishwari ya soko lilotrend kwa kipindi hicho. Sasa jiulize soko likianza ku consolidate yaani kutembea upande sio juu wala chini utatengeneza faida au hasara. Ni wazi utapata hasara na hata kurudisha faida zote ulizo pata kipindi cha soko linapo trend, kwa maana masoko yana consolidate mara 5 zaidi kuliko yanvyotrend kwa kipimo cha muda. Ni vigumu kwa trader mmoja kuwa master wa mbinu mbili za trading zitakazo fanya vizuri mida yote yaani kipindi cha masoko yanapo trend na kipindi ambacho masoko haya trend. Traders wengi hua ana mbinu moja tu itakayofanya kazi kati ya soko moja tu aidha soko la kutrend au consolidation/ranging.

Tuangalie upande wa proffesional trading wanafanyaje yaani Hedge funds n.k. Haya ni makampuni ya uwekezaji, yaani wanapokea pesa na kutrade kwa niaba ya wawekezaji wao kisha huwatoza asilimia flani ya faida mara nyingi huwa ni asilimia 20-50 ya faida itakayopatikana mwaka husika.  kila mwaka kwao ni mwaka mpya yaani wanatoa faida kwenye fund kwa kuangalia matokeo ya mwaka husika, sio kutoka fund ilipoanza. Ni hivi, tuseme fund imeanza 2018 mwaka huo ikapata hasara ya asilimia 12 hapa hawata toa chochote kwenye fund sababu wamepata hasara, mwaka unaofuata wakipata faida ya asilimia 10 ingawaje hawajarudisha kiasi kilichopotea watatoa faida na kuwalipia wawekezaji wao, na wenyewe hujilipa perfomance fee asilimia 20 ya faida ingawaje bado fund kiujumla iko nyuma kimtaji. Kisha hulipia pesa nyingi kwenye matangazo kwenye vyombo vyahabari vya kifedha, viwatangaze wamepata faida huo mwaka. Mwaka mpya ukianza wanapata wawekezaji wapya na elewa kima cha chini cha kuwekeza kwenye fund hizi hua ni mamilioni hadi mabilioni ya pesa kutegemeana na ukubwa wa fund. Hivyo tunagundua wao hata wakipata hasara wawekezaji wapya huja kuziba lile pengo. Sasa wewe ambae huna wawekezaji utafanya nini!

Tuachane na hawa proffesional traders kwa maana wao ata wakiyumba hutegemea watapata investors wapya watakuja kuwaongeza kimtaji pale tu mwaka unaofuata wakifanya vizuri ata kama kiujumla bado wapo kwenye hasara. Kwaio wao wamesha jitengenezea njia ya kuendelea kuwepo mchezoni.

Sasa hapo tunajifunza nini kama hawa professional wenye mitaji mikubwa na team kubwa zakufanya tafiti, wanafanya hivi kwanini wewe usifanye pia kwa maana kesho ya soko hauijui ni vyema kutoa faida tuseme kila baada ya miezi mitatu ili hata ukipoteza mtaji mbele ya safari ue na pesa mfukoni kurudi sokoni pale ambapo soko litakaa vizuri na kukupa faida tena.

sheria namba moja ya trading ni kuendelea kua mchezoni sasa ukiishiwa pesa huwezi kurudi tena siku nyingine.

Utajiuliza kama hii biashara ya trading sio yakuaminika kiasi cha kujiami hivi, mpaka kutoa faida mara kwa mara kwanini niendelee kuifanya. jibu ni hili kwenye biashara ya trading ndio biashara pekee ambayo utapata taasisi ya kifedha ikakupa mkopo (margin/leveraged trading) bila dhamana yoyote wala kuwa na biashara yenye historia yakutengeneza faida ndani ya miaka kadhaa. Hivyo ni rahisi kwa trader mzoefu na mwenye ustadi kukuza mtaji haraka ndani ya kipindi kifupi sana. kwa leverage inawezekana kabisa kwa trader mzoefu kukuza mtaji kutoka $100 mpaka $20,000 ndani ya muda mfupi sana.

Sasa tunafanyaje kufanikiwa kwenye biashara kama hii, yatupasa kufanya diversification. kila mara unapopata faida kubwa kwenye trading toa nusu ya faida au yote ikiwezena wekeza kwenye biashara zenye uhitaji wa mtaji mkubwa, zenye hatari ndogo kabisa ya kupoteza mtaji na zenye faida ndogo mfano nyumba n.k

Kisha acha mtaji mdogo ulio anza nao kwenye trading na rudia tena hii itakusaidia pale ambapo bishara ya trading ikiyumba utakua na pahala pakujishikiza tena mfano kwenye mali zisizohamishika unaweza ukawa unapa kodi kila mwezi ikakusidia kurudi sokoni, na sio lazima uwekeze kwenye mali kama hizi unaweza ukawekeza kwingine kokote ilimradi tu hatari ya pesa kupotea iwe ndogo zaidi na utapata cashflow daily au monthly.

Kwa upande wangu hii mbinu imenisaidia sana kukua katika trading hata kipindi ambacho nikiyumba sokoni hua ninakua na sehemu nyingine yakupata mtaji wakuendelea na biashara ya trading kikubwa ni kwamba  usije ukaishiwa pesa kabisa kwenye trading.

Trading hua inavipindi vichache sana ambavyo trader mwenye ustadi hua ni  rahisi kwa yeye kupata faida na vipindi vingi vigumu ambavyo hua ni ngumu sana kupata faida. Yaani asilimia 80 ya muda masoko ya kifedha hayaendi popote ucheza kwenye bei zile zile  (range market)  na asilimia 20 ya muda masoko hutembea na kuwapa faida traders.

Na ukweli ni kwamba ni ngumu sana kuvigundua vipindi hivi mapema ni rahisi hapa kwenye picha ya chini kwa sababu muda umeshapita lakini kwa muda uliopo ni ngumu kugundua je trend itaisha wapi nakuanza wapi. Ingekuwa rahisi kungekua na trader wengi Zaidi wanaofanikiwa.

Ingawaje zipo mbinu tofauti tofauti zakugundua soko linalotrend lakini sio sayanisi ya uhakika ni sayansi ya uwezekano wa asilia flani.

Kujifunza mbinu bora yakupata fursa za trading kama hizi za masoko yanayo trend, mbinu itakayokuwezesha kwa asilimia 75 kuingia mapema pale ambapo soko linaanza kutrend, bonyeza hapa.

Kwenye trading kutengeneza faida ni jambo moja na kuzitunza izo faida zikazaa tena bila kupotea zote ni jambo lingine.

Professional traders wamejua namna yakucheza na hii biashara kama nilivyoainisha awali  na sisi retail traders tujue namna ya kucheza nahii biashara kwa namna yetu.

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Ramadhani
Ramadhani
9 months ago

Thanks for the contents, Another point: withdrawing profits is a way motivating urself to love the market much more, although I haven’t yet done this, I heard somewhere, yes. I will if not wish do this one day. Another interesting part is kumbe nao Professional traders (hedge funds) wana lose!!!!? LoL!!!! This market is amazing Broo. I had to work hard.

4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x