!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Tatizo La Kurudisha Faida Zote Sokoni.

Ile hali kupiga pesa halafu ghafla tu Ijumaa inafika umepiga mzinga faida zote na pengine hata sehemu ya mtaji imepotea sokoni huumiza sana. I get you my brother hata mimi wakati naanza trading hali hii ilikuwa ina nikumba sana hadi ikafika mahali nikatamani kuacha hii biashara.

Nakumbuka kipindi flani wakati bado ni newbie, nilideposit dola 300 kwenye trading account yangu. Nikawa na trade vizuri lakini kila wiki sifungi faida au kuna baadhi ya wiki nafunga na balance ya $280 au $180. Sio kwamba nilikuwa sipati winning trades Hapana! Nilikuwa napata tena nyingi tu lakini hasara zilikuwa nyingi na kubwa kiasi cha kufanya account isisogee mbele wataalamu wanasema 1 step forward, 3 steps back. Kuna wiki moja nilijiandaa vizuri sana na kufuata plan yangu, wakati huo nilikuwa nimeshapiga mizinga kadhaa na balance ilibakia kama $180. Hiyo wiki ilikwenda safi account ikapanda hadi $250, nilifurahi sana lakini kufikia alhamisi ego ilinipanda na kujiona unstoppable nikawa nataka kufikia $300 angalau nibreak even. Aisee! kilichotokea ni kuchoma ile account kwa sababu kila trade baada ya hapo ilikuwa mzinga nikajikuta niko kwenye panic mode na kuanza kuweka lot mashine ili tu niweze kurecover lakini haikuwezekana tena it was too late for recovery. Kama mnavyofahamu ukisha hit 50% drawdown unahitaji 100% kurudi tu pale ulipo. Kwa macho ya kawaida unaweza kusema it’s okay the market moves the way it does lakini kuna makosa millioni (Literally) yametendeka hapa na kama sio mtu wa kufanya review unaweza kujikuta unarudia haya makosa miaka na miaka bila mafanikio na mwisho unaquit.

Somo la leo nitakupa sababu kwanini unarudisha faida zote sokoni na solution ya kutatua tatizo hili hivyo chukua notebook yako kalamu and let’s go to class.

Kwa nini faida zinarudi sokoni?

Kubahatika mwanzoni

Sometimes naona ni bora usibahatike kabisa mwanzoni kwa sababu asilimia kubwa ya traders waliopoteza pesa zao sokoni ni kwa kujaribu tena bahati kwa mara ya pili wahenga walisema bahati haiji mara mbili. Ukibahatika mara ya kwanza kuna raha flani hivi huja pamoja na dharau ya kuona hii kitu ni rahisi “Yani kuanza tu nimepiga hela je nikiweka $1000 yangu si nitakua milionea?” laiti kama trader huyu angefahamu anakwenda kurudisha zile faida pamoja na pesa mfukoni asingeendelea bali kuchukua zile faida za bahati na kununua kitu ili iwe ukumbusho lakini ni asilimia moja tu ya watu hufanya hivi, umeonjeshwa kidogo ili ukalete zote 😂.

Kupata bahati mara ya kwanza kunafanya traders wengi kuamini wataweza kulipiga hili soko kwa kubonyeza tu buy au sell button kwenye mt4 bila kuweka jitihada zozote kumbe ni vice versa. Ni angalau upate vitasa mwanzoni ujifunze kuwa serious kwani utakwenda kuweka nguvu na kujipanga kuliko yule aliyepata bahati mwanzoni. Niliwahi kusema “Luck is not a consistent reliable strategy.” You will eventually return all the profits made and donate all your money in the bank.

Kujiamini Kupitiliza (Over Confidence)

Hakuna tatizo lolote kujiamini lakini kujiamini kukipitiliza huleta matatizo. Point hii itaendeleza kidogo na point ya kwanza kwa sababu trader anapobahatika sokoni anapata ego na ego ni mbaya sana, inakufanya ujihisi unstoppable na madhara yake ni kukumaliza kabisa. Hapa ndipo yale matatizo ya over trading na overlooking your trading plan (Kufanya analysis kwa juu juu) yanapojitokeza. Katika hali ya namna hii ni dhahiri kwamba unarudisha faida zote ulizotengeneza aidha kwa kubahatisha au la na pengine ukachoma account na kuanza kuingia mfukoni tena ili uweze kutrade. Umaskini ndio unaanzia hapa kwa sababu hili tatizo likiendelea unaweza kujikuta unajimaliza pesa zote na ukifika hatua hiyo ndipo akili zinarudi sasa.

Ni vizuri sana kujiamini lakini kuwa na control ya confidence hasa katika kipindi unapopata trade nzuri (winning streaks) kwa sababu ni rahisi sana kuteleza na kuangukia kubaya na pengine usiweze kurudi ulipokuwa financially.

Trading Kulipiza Kisasi (Revenge Trading)

Kulipiza kisasi kamwe hakubadilishi hali halisi. Wakati mwengine unaweza kufanya kitu kwa hasira lakini saa chache baadae majuto yakawa ni makali na bado hali halisi haijabadilika. Unapopata hasara sokoni na kitendo cha wewe kutaka kutrade tena na lot kubwa ili kufidia zile hasara kunahatarisha sana hata zile faida zilizobaki. Every trader duniani get losses lakini kinachotofautisha pro traders from newbies ni kwamba pro traders wana manage risk kisawasawa, hasara za pro traders haziwezi kuchochea panic ambayo mwisho wake ni kulipiza kisasi. Unakuta new trader ameanza vizuri lakini somo la psychology halijakaa sawa basi account inakua vizuri, lakini anafika sehemu anapatwa na loosing streak ya trade 4-6 mfululizo. Hapa sasa ndo mtihani traders wengi wanachemka na kuanza kuogopa, the next trade kinachotokea ni kuongeza lot size ili aweze kurudisha zile hasara kumbe trade ile haikuwa yenyewe basi mzinga unakuwa mkubwa zaidi. Trader anarudia mara mbili mara tatu kwisha, account imeshafika nusu.

Kwanza unapokuwa kwenye drawdown au loosing streak akili yako inatakiwa kuwa very strong kuliko kipindi chochote kile, hapa kuna external na internal forces zinapingana sana yani reality ya plan inakuambia wait and relax find another good trade lakini your conscious can not handle the heat inakuambia ooh my God i am losing all of my money na kwa sababu internal forces ina nguvu kuliko plan yako unafanya maamuzi ya ku ignore your plan. Sasa ukifanya hivi kila siku utakuwa wale watu wakusema daah hii biashara imenishinda.

Toka nimeanza kufanya Forex sijawahi kusikia au kuona mtu amerevenge trade na kufanikiwa kila mtu anaishia kula hasara ambayo hata moyo unashindwa kuvumilia. Kuna rafiki yangu mmoja alitokwa na machozi sana baada ya kupoteza kila kitu na ilibidi aanze from scratch.

Never revenge trade utaokoa faida nyingi sana, Unaweza kusoma zaidi kuhusu revenge trading kwa kupitia uzi huu: WHAT IS REVENGE TRADING? AND HOW TO AVOID IT?

Vile vile unaweza kusoma uzi huu OVER TRADING. THESE 3 SIMPLE QUESTIONS WILL HELP YOU STOP COMPLETELY. Utakusaidia sana kuepukana na matatizo ya kurudisha faida zote sokoni.

Solution

Kwenye kila tatizo ni muhimu kutafuta ufumbuzi. Uzuri tatizo hili limeshapatiwa ufumbuzi muda mrefu sana na ulinisaidia sana wakati naanza trading, actually kuna wakati nilizama kwenye huu mkumbo na solution hizi zilinisaidia sana and i am always grateful for my mentor kwa msaada huu.

Acha kufanya yote niliyotaja hapo juu.

Nafahamu ni ngumu sana kuvunja tabia mbaya lakini naamini ukivipa muda vipaumbele hivyo unaweza kuacha na kusahau kabisa. Span, itakuchukua miezi hadi nane kama utakuwa na nidhamu, mwanzoni itakuwa ngumu sana lakini hakuna kinachoshidikana.

Vile vile acha kutrade kwa bahati nasibu UTAPOTEA! tafuta course ya mtu unayemuamini, soma kwenye mitandao, jiunge online communities zenye msaada kwako usiwe wale watu ambao kila siku unatrade vitu tofauti kumbuka Forex trading ina edge lakini kamari haina edge kwa hiyo kuwa smart unapofanya maamuzi. Kama unahisi utatapeliwa basi google is everything soma, focus on expanding your knowledge. You will have a better chance of success kulingana na trader anayecheza kamari na kutegemea bahati.

Withdraw Profits Regularly

Kuna traders wanapenda sana kukuza account bila kuwa na malengo. Withdrawing profits kutakusaidia sana kuepeusha matatizo ya kurudisha faida sokoni. Kila mwezi kama umepata faida kiasi fulani ambacho kipo kwenye withdrawal threshold fanya withdrawals. Nakumbuka kuna siku moja account yangu ilikuwa sana, kama mnakumbuka flash crash ya mwaka 2017 iliyotokea kwenye USD/CHF monday morning January 2017. Nilikuwa na order yangu lakini soko lilipofunguliwa jumatatu likatembea against my order pip nyingi sana na kufanya nile mzinga mkubwa hapo ndipo nilipojifunza unatakiwa kufanya regular withdrawals mara kwa mara ili masoko yakienda ndivyo sivyo you already secured the bag.

Lakini sasa, linapokuja suala la withdrawing inabidi uwe profitable na kuwa profitable sio suala la mchezo ni jambo la kuwekeza focus na nguvu zako zote unaweza kusoma uzi huu kufahamu zaidi SIRI YA KUPATA CONSISTENT WITHDRAWALS.

Vile vile unaweza kusoma uzi huu utakusaidia sana kufanya maamuzi ya profits zako HOW TO INVEST YOUR FOREX PROFITS WISELY.

TOA FAIDA MARA KWA MARA KWENYE AKAUNTI YAKO YA TRADING.

Nina imani sana utakuwa umejifunza vya kutosha kwenye somo hili, kama una swali unaweza kuuliza kwenye comment section hapo chini.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Joshua
Joshua
9 months ago

Itoshe kusema kwamba Mungu awabariki Sana tunajifunza mengi na mnatuokoa sana

Ramadhan
Ramadhan
9 months ago

Raymond you always my favorite certified Trading Psychology mentor. Bro Naomba kujua one thing. Drawdawn ina maana gani? Kingine Ni just Joke, crash ya USDCHF 2017 Hukuweka SL ? maana hadi unaikumbuka sijui kilitokea nini hahahaaa muda huo sijui kama kuna kitu kinaitwa forex kumbe watu wanapambana.

9
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x