!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Software Nzuri Kwa Ajili Ya Forex Trading.

Kuna software nyingi sana kwa ajili ya forex trading na kwa jinsi teknolojia imekuwa kwa kasi sana wengi mnazifahamu metatrader (4 au 5), Trading View, C-Trader, Ninja Trader na nyengine nyingi ambazo zimekuwa zikitangazwa kwa nguvu sana. Kila software ina uzuri na ubaya wake lakini kwenye suala la utendaji kazi nitakuambia kitu kimoja tu.

Kutokana na experience yangu ya trading kwa miaka mingi Metatrader (4 au 5) is the best software kwa sasa kwa sababu ni all in one platform iko fast na secure, ukiwa nayo huna haja ya kuwa na other platforms kwa ajili ya execution na mambo mengine.

Nafahamu watu wanapenda trading view kwa sababu ya muonekano wake pamoja na uwezo wa kusave michoro ya chart na kuziview kwenye device yoyote ile. Hilo ni kweli lakini pamoja na uzuri wake wote itakugharimu kulipia kila mwezi $15 na isitoshe bado huwezi kufanya order execution kama broker wako hayupo intergrated, Hadi kufikia leo ni broker wachache sana wako integrated na trading view kwa hiyo itakubidi uwe na trading view kwa ajili ya analysis na metatrader kwa ajili ya execution. Hizi ni complication tu na kiuhalisia huitaji sana trading view labda kama una uwezo wa kulipia kila mwezi na isiathiri kipato chako.

Nakumbuka wakati nikiwa mgeni kwenye hii biashara niliishia kupoteza pesa nyingi sana kwenye software fees zaidi ya ($1000) kwa providers mbali mbali kwa kuamini zina secret lock to success kumbe si kweli bali ni ulimbukeni na kutokujua. Always keep it simple and as long as you have a working strategy, the software does not matter. Nafahamu watu wamelipia trading view miaka na miaka lakini bado hawatengenezi pesa. Binafsi natumia trading view kufanya illustrations kwa wanafunzi wangu tu au nikiwa na Ipad pro yangu kwenye safari ninapokuwa airport nasubiri ndege inaniokoa sana lakini hii siyo sababu dhabiti kujustify kwa nini nalipia trading view haina ulazima sana kama ni trader unayeanza career yako.

Metatrader Hutolewa Bure Na Broker

Kama nlivyosema awali kwamba hii software ni bure na unapewa na broker unapofungua account. Huitaji software nyengine kabisa labda kama ni mtu wa kubadilisha vifaa vyako mara kwa mara, Unaweza kusoma uzi huu kujifunza kuset mt4 yako: HOW TO SET UP A CUSTOM TEMPLATE ON THE METATRADER PLATFORM.

Ni Rahisi Kutunza Kumbukumbu za Trading Yako

Hakuna kitu kibaya kama kutrade bila kufuatilia kumbukumbu zako (Trading History). Mt4 imerahisisha sana kwani inatunza kumbukumbu zako toka siku ya kwanza umedeposit na wamefanya kazi nzuri ya kukuwezesha kuextract history hiyo kwa mfumo wa pdf.

Unaweza kutumia statement hiyo kudadisi maeneo ambayo hufanyi vizuri kwenye trading yako na kurekebisha, huwa nasema kila siku kujifunza kutokana na makosa ni jambo litakalo kusaidia sana kupiga hatua mbele. Metatrader imekurahisishia hilo kwenye upande wa kumbukumbu.

Kama bado unahangaika utumie software gani basi nakushauri utumie metatrader itakuondoa kwenye zile newbie stress kama nilizokuwa nazo mimi, itakufanya ufocus na the real business of trading na kutengeneza kipato na utaepukana na kupoteza pesa kwenye useless fees. Kama nia yako ni kutengeneza pesa basi platform ina mchango wa asilimia 1 tu.

Inafanya Kazi Vizuri Sana Na Expert Advisors (TRADING ROBOTS)

Kama wewe ni mpenzi wa algorithmic trading basi metatrader ni nyumbani kwako. Kwanza kabisa kama inakupa development environment (Meta Editor) nzuri na stable sana kwa ajili ya coding pamoja na deployment. Kwa karibu asilimia 98 ya experts kwenye forex trading zimetengenezwa mahususi kwa ajili ya metatrader. Vilevile metaquotes language (mql) in community kubwa sana ya watu ambao wanaweza kukupa msaada endapo utakwama wakati unadevelop robot lako.

Kama bado unahangaika unaweza kudownload metatrader hapa

Kama unatumia Mac fuata masharti haya Ku install Download Instructions

Final Note

Kuna traders ambao wana prefer both platforms, ni kitu kizuri lakini uzi huu umelenga kumsaidia trader mgeni na mwenye mtaji mdogo. Sio lazima ufanye complication kwa sababu complications husababisha hasara. Kama una budget basi ni sawa ila kama una struggle basi sio lazima. Vile vile usiwe na shaka eti kwamba ukitumia platform tofauti kwa ajili ya analysis utapata faida, hicho kitu hakipo. Unaweza pia kusoma uzi huu kufahamu ni jinsi gani utaweza kutengeneza consistent profits. SIRI YA KUPATA CONSISTENT WITHDRAWALS.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x