!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Siri Ya Kupata Consistent Withdrawals.

Withdrawing profits kutoka kwenye trading account ni ndoto ya traders wengi lakini uhalisia ni kwamba traders wengi wana withdraw tu masalia ya account. Hapa namaanisha chenji chenji zile zinazobakia baada ya kuchoma account. Kama una kumbukumbu siku kadhaa zilizopita niliachia uzi ulioelezea jinsi account ya $1000 ilivyo teketea na kubaki $30 ndani ya siku tano. Kama bado hujasoma unaweza kupitia hapa: TRUE STORY: SHUHUDIA $1000 ILIVYOPOTEA NDANI YA SIKU TANO. Yani hivi ni vitu vinayvotokea kila siku ukiachana na wale wanaokumbana na matapeli mtandaoni.

Ukweli ni kwamba withdrawing profits ni raha sana, hata wao wanaotoa chenji chenji kuna raha flani hivi wanasikia hata kama ni kidogo. Ile feeling kwamba hela inatoka kwa broker na kufika kwenye account yako inaleta raha flani isiyo na kifani 😂. Lakini changamoto ni moja, sio kila trader ana nufaika, naweza kusema traders wanaotoa chenji chenji yaani masalia baada ya kuchoma account hivyo hawapati ile raha ninayo zungumizia na kwa asilimia kubwa ni traders wengi sana zaidi ya aslimia 90.

Kama hautaweza kupata consistent withdrawals ni dhahiri kwamba hautaweza kufanya trading ikawa full time job. Kwanza kabisa ninaposema consistent withdrawals namaanisha unapofunga hesabu zako za kila quarter profit unayopata unaweza kuwithdraw na unaweza uka sustain kila mwezi hadi the next quarter (reasonable income).

Trading is a speculative business yani kubashiri. Traders tunachofanya ni kubet thamani ya pesa flani aidha ipande au ishuke kulingana na technical analysis na kama uko sahihi unapata faida. Kumbuka sio kila mwezi unaweza ukafunga faida kwani masoko ya kifedha duniani yana athiriwa na changamoto nyingi ikiwemo za kiuchumi au kisisasa. Hivyo kuna miezi utafunga faida na kuna miezi hautafunga faida, professional traders tunagawa mwaka katika quarter 4 yani vipindi vya miezi mitatu mitatu ndipo tunaangalia faida iliyopatiakana na kuwithdraw profit.

Mfano wa Quarter

  • January, February & March = Quarter 1
  • April, May & June = Quarter 2
  • July, August & September = Quarter 3
  • October, November & December = Quarter 4

Sasa, ili upate consistent withdrawals inabidi ufahamu mambo yafautayo ambavyo ndio lengo la uzi huu leo.

1. Uwezo wa kufunga faida yani (Profitability)

Hakuna namna unaweza kuwithdraw kama hupati faida labda kuwithdraw masalia ambayo sio tunayo yazungumzia hapa. Lazima uwe na uwezo wa kuzalisha faida walau miezi miwili kwenye kila quarter. Suala la kuwa profitable sokoni linawezekana kabisa asilimia 100 kama una skill ya kutosha na uzoefu wa hali ya juu. Unaweza kuwa profitable mara moja au mbili lakini hizi tunahesabu kama bahati. Huwezi kuwa full time trader kama wewe unategemea bahati lazima uwe na uwezo wa kuzama sokoni na kuchanganua soko kwa makini ndipo unaweza ukapata faida. Skill hii haipatikani kirahisi inabidi ujifunze na kuwekeza muda wako sokoni ndipo utaweza kuwa profitable. Watu wengi huja na kubahatika lakini ukimwambia rudia tena basi anarudisha faida zote sokoni kwa kupata hasara tena kwa spidi sana. Lazima uwe profitable kila quarter kupata consistent withdrawals. Soma vitabu, fanya research wekeza muda wako uweze kuwa profitable ukishindwa kuwa profitable hata rafiki zako wa karibu wanaweza wakakuona unapoteza muda na pesa hivyo pambana kadiri uwezavyo uweze kutusua.

2. Mtaji wa kueleweka (Sound Capital)

Hii ni factor muhimu sana hasa kama unataka kuwa na uwezo wa kupata consistent withdrawals. Mtaji ndio utakao kuwezesha kufikia malengo yako. Usipokuwa na mtaji ambao unaweza ukazalisha consistent income, matokeo yake ni kufanya mambo ya ajabu kama over risking. Angalau naweza kusema trader hutakiwi kuwa na kiasi chini ya $5000 kama uko very serious na biashara hii, tena usibaki hapo kwenye $5000. Jitahidi kuongeza mtaji kadiri unavyoweza kidogo kidogo ukiangalia account inakwendaje. Sasa usinielewe vibaya kama bado unajifunza ni vizuri ukaanza na live account ndogo maana demo account haikufundishi vizuri jinsi ya kutrade live money kitu ambacho utakifanya maisha yako yote.

Ukiwa na mtaji wa $5000 na kila mwezi ukaweza kupata trade mbili tu zenye risk reward ratio ya 1:50 yani ukirisk $50 una uwezo wa kuvuna $500 ni vyema sana. Hasara zitakuwepo pia so imagine ukapata hasara 3 mwezi huo? kimsingi uta poteza $150 tu kama unafanya risk management. Kwa hiyo faida yako itakuwa $350 huo mwezi. Quarter moja ina miezi mitatu so kama utaweza kurudia nilicho sema point number moja hapo juu (kuwa profitable) na ukawa consistent kila mwezi maana yake ni kwamba una faida ya $1050 sawa na millioni mbili na laki tatu baada ya quarter moja na sasa una mtaji wa $6050. Sasa Maamuzi ni yako kama utaitoa au kubakiza huyo ni wewe.

Point yangu ni kwamba ukifanya hivyo kwa mwaka mmoja tu bila kupata drawdown kubwa kuna uwezekano kabisa kwamba trading ikawa your full time job. Kinachokwamisha wengi ni kutokuwa na mtaji na skill ya trading. Ukiweza kupata mtaji wa 5-6 figure uko kwenye safe place laking jitahidi kufanya diversifcation kwani speculative markets hubadilika muda wowote hivyo ni vyema ukawa na vyanzo vingine vya mapato. Unaweza kusoma uzi wangu nilioandika kitambo kidogo wa HOW TO INVEST YOUR FOREX PROFITS WISELY.

3. Broker Sahihi

Yote haya ni kazi bure kama unatumia broker ambaye huna uhakika kwamba atakulipa endapo utapata faida. Broker wako ndio nguzo yako, bila broker trader si kitu kwani broker ndiye anayetupa fursa ya kuhusika sokoni (participation). Forex trading ndio soko lenye mabroker wengi sana duniani na kwenye msafara wa mamba kuna kenge pia. Imefikia hatua broker wanakubali deposit hata kama hujahakiki account yako ilimradi tu akuzuie kuitoa hiyo pesa baadae mpaka ufanye uhakiki. Na ukishindwa kufanya uhakiki kwa sababu yeyote basi hesabu hiyo hela imekwenda na maji. Nimeandika uzi kuhusu JINSI YA KUMKAGUA ONLINE FOREX BROKER. ni muhimu sana ukasoma kama unataka kuwa salama na pesa zako.

Broker anatakiwa kuwa rafiki yako na siyo mtu anayekutega apige pesa zako. Broker anatakiwa awe na uwezo wa kukulipa muda wowote. Broker anayeweza kukulipa muda wowote anatakiwa kuwa na segregated account kwa ajili ya wateja wake. Hapa namaanisha broker hatakiwi kuchanganya pesa za kuendesha biashara na pesa za trading za wateja wake. Hata strict regulations kama FCA UK huwabana sana lakini mabroker wengi sana hukwepa. Hakuna njia rahisi kujua hili isipokuwa kuchelewesha withdraw kwani broker anakuwa hana pesa na anategemea traders wengine wachome au wadeposit ndipo wewe ulipwe. Ikitokea imeshindikana basi huwezi kulipwa. Kumbuka ukideposit pesa kwa broker haiendi kwenye MT4, Pesa inakwenda straight bank na kinacho onekana kwenye mt4 ni reflection tu ya ulichodeposit. Zile ni number tu zilizounganishwa na data au price feed kutoka kwa liquidity provider. Ni rahisi sana kwa mabroker matapeli kucheza na zile platform.

Nakumbuka mwaka jana nilitrade the Nasdaq na broker mmoja wa South Africa and nilideposit $400 na kufanikiwa kuikuza account hadi $8000. Kilichotokea ni kwamba zile profit sikuwahi kuziona tena kwani broker alicheza cheza na platform wakafuta trades zote na kubakisha deposit amount tu. Hapa ndo nlipogundua kwamba huyu broker alikuwa anajihami nisije kumvunja. Ile trade ilikuwa na uwezo wa kwenda hadi $38,000.

Ukijaribu kuwatafuta wanakupa sababu zisizokuwa na msingi na baada ya siku kadhaa mt4 account yangu ikawa invalid.

Kwa hali hii huwezi kuwa na consistent withdrawals, broker akikuwamisha unaweza jikuta umepoteza muda mrefu sana na effort zako zikawa zimeenda na maji. Ni vizuri kufanya utafiti unapotafuta broker kwani ukizembea tu unaweza jikuta kwenye mikono ya majangili.

Natumaini umejifunza jambo lam msingi sana kwenye somo la leo. Kama una maswali au hujaelewa basi weka kwenye comment hapo chini.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
thomas mussa
thomas mussa
1 month ago

ni broker gan brobunatushauri tumtumie kulingana na experiance yako

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x