!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Njia Mbali Mbali Za Kutrade Forex

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo

Kumekuwa na mkanganyiko sana kuhusu njia tofauti za kutrade forex. Forex trading ni industry kubwa sana na karibu kila mtu anayehusika na biashara hii ana njia yake anayotumia kutrade. Kwanza kabla ya kungalia njia mbali mbali za kutrade inabidi tuangalie aina mbali mbali za traders.

Vile vile kama hujasoma Uzi wangu uliopita wa MUUNDO MZIMA WA SOKO LA FOREX ni vyema ukapitia kwani huu ni muendelezo wake.

Aina mbali mbali za traders

Kwanza kabla sijaainisha naomba ufahamu kwamba aina yeyote ile ya trader inachangiwa sana na strategy yake. Kama strategy yake imebase kuswing basi atakuwa swinger vile vile kwa day traders na scalpers etc. Hivyo kabla hujachagua strategy yeyote ile inabidi wewe ujiangalie unaweza kuwa comfortable wapi usije poteza muda wako na pesa pia.

Swing Trader

Huyu ni trader yeyote ambaye ana hold trade zake zaidi ya siku moja au masaa 24. Kama umeshawahi kufungua position moja na kuifunga baada ya masaa 24 basi unakuwa umeswing trade either kwa kufahamu au kutokufahamu. Naweza kusema kwa kiasi kikubwa mimi binafsi ni swing trader kwa sababu trade zangu nazishikilia kwa siku hadi wiki kadhaaa na kuzifunga. Hii ni njia rahisi na isiyo na stress kabisa kwa sababu hakuna uhitaji wa kuketi kwenye screen yako masaa 24 ukifunga na kufungua trade.

Day Trader

Huyu ni tofauti kidogo na swing trader kwa sababu yeye anahold trade ndani ya masaa 24 tu. Haijalishi trade iko kwenye faida au hasara, sheria ni kwamba trade haiwezi kulala kuona siku ijayo. Style hii ina manufaa yake kama kuepukana na kupanuka kwa spreads saa sita hadi saa saba usiku kuelekea kupata hasara zisizo za msingi. Changamoto ninayoona kwenye hii style ni kwamba itakubidi uwe kwenye screen kila siku kufuatilia yanayo endelea na kama haiendani na utu wako (personality) basi inaweza ikakushinda au kukuletea hasara. Vile vile day traders wana kabiliwa sana na changamoto ya over-trading ambayo usipokuwa makini kuwa na nidhamu inaweza kukumaliza haraka sana.

Scalper

Kwa upande wangu hii nii kazi ngumu sana kwa sababu haiendani na personality yangu. Scalping ni kitendo cha kutrade mara nyingi sana na unaweza ukatrade hadi mara 50 – 60 kwa siku. It is a very intesive type of trading na wengi hawafanikiwi kwa sababu inahitaji watu ambao wako very fast na accuracy ya hali ya juu. Kama ni trader mgeni basi sikushauri uwe scalper. Ila kama utasisitiza basi ni vyema ukatafuta EA (Expert Advisors) trading robots ziweze kukusaidia. Wakati unaanza trading, ni dhahiri kwamba hautaweza kuitegemea kama full income, utakuwa either una soma chuo au unafanya kazi hivyo scalping haitakufaa. Soma Uzi Huu: NAMNA YA KUFANIKIWA NA BIASHARA YA FOREX KWA WAAJIRIWA WASIO NA MUDA WA KUTRADE KUTWA NZIMA Utakusaidia sana kukupa dira wapi uanze.

Position Traders

Hawa ni traders ambao wana hold position/trade zao kwa kipindi kirefu sana hadi mwaka na zaidi. Kwa mfano nina trade ya GBPJPY niliyo hold kwa miezi mitatu sasa na sitegemei kuifunga siku za karibuni. Hii ni type ya trading isiyo na stress na unaweza ukaendelea na shughuli nyengine za kiuchumi huku trade zako zina chakata faida. Ukiwa postion trader au swing trader kuna asilimia zaidi ya 90 kuwa na faida kuliko haya makundi mengine. Nafahamu watu wataleta ubishi lakini waambie waonyeshe takwimu zao na utaamini ninachokuambia. Soma uzi huu: HOW TO TRADE LIKE THE BANKS. THEY CONTROL 92% OF THE VOLUME na utaweza ni aina gani ya matrader walioko kwenye hizi financial institutions.

Baada ya haya nina imani kubwa sana kwamba utakuwa umefahamu wapi ujiweke katika hayo makundi manne. Kinachofuata sasa ni kuona unaweza kutrade forex kwa kutumia njia ngani.

Retail traders wanaweza kutrade forex kwa kufanya chambuzi (Analysis) lakini chambuzi hizi zimegawanyika katika makundi matatu.

1. Technical Analysis

Uchambuzi huu hutegemea sana data zilizopita ili kuweza kutabiri yajayo (Past Results To Predict The Future) trader anayetumia technical analysis kama guidance yake ya kufanya maamuzi basi mara nyingi itambidi awe na charts zake kuangalia nini kilitokea miaka ya nyuma na kutafuta pattern hizo kwenye siku zijazo kwa lugha ya kitaalamu tunasema backtesting. Unaweza kusoma uzi huu: BACK TESTING A FOREX STRATEGY kujifunza zaidi. Technical analysis hubeba kundi kubwa la retail traders duniani na ninaweza kusema huku ndo chimbuko la strategies nyingi tunazoziona kama Pure Price action yote, Elliott Waves, Wyckoff na Expert Advisors. Yani kwa kifupi ni lazima uwe na charts ili uweze kufanya decisons baada ya kubacktest miaka ya nyuma na kuona pattern zilitokea vipi.

2. Fundamental Analysis

Trading ya aina hii hutegemea sana sababu mbali mbali zinazoathiri uchumi wa nchi husika. Kwa mfano pair kama EUR/USD, hizi ni nchi mbili tofauti na kukiwa na repoti mbaya ya ajira (Unemployment rate report) inaweza ikaathiri thamani ya dola kushuka na kupeleka pair ya EUR/USD kupanda, vilevile kwa upande wa Euro. Mpaka hapo unaweza kuona ukiwa fundamental trader kazi yako kubwa itakuwa ni kusoma report mbali mbali zinotolewa kwenye nchi husika na kufanya maamuzi. Taarifa hizi ziko nyingi na kitaalamu tunasema Economic News. Sasa Unaweza ukaniuliza nazipata wapi?

Kuna website nyingi zinazotoa hizi taarifa ila nitakupa mbili ambazo huwa nazitumia.

  1. Fxstreet
  2. Myfxbook

Sasa sio kila economic news zitaleta movement hivyo kazi yako ni kufocus na High Impact News, zile habari zenye utepe mwekundu.

Fxstreet calendar. Focus na High Impact News

Note: Ukiamua kuwa fundamental trader basi fahamu kwamba muda mwingi utakuwa unatrade kukiwa na high volatility hivyo kumbuka kutumia risk management kuepukana na slippage kubwa. Kama hufahamu volatility ni nini unaweza kusoma uzi huu: UNDERSTANDING VOLUME AND VOLATILITY. TRADERS NEED TO KNOW THIS.

3. Sentiment Analysis

Huu ni uchambuzi unaotegemea sana idadi ya watu walionunua au kuuza fedha au pair fulani. Style hii pia naweza kusema hutegemea mawazo ya umati wa watu (Crowd Psychology) , Yani watu wengi wakiwa wamenunua pair flani basi traders huamini bei itakwenda juu lakini muda si mrefu itadondoka hivyo kupata fursa ya kuuza baadae pale ambapo bei itakuwa imefubaa. Hii style huwafaa sana traders wanaotrade reversals. Binafsi huwa sitrade kwa kutumia style hii lakini kama ungependa kupata sentiment analysis unaweza kufuata link hii Sentiment Analysis

Mpaka kufikia hapa ninaamini utakuwa umepata mwanga sahihi, part one tumeongelea aina za traders na part tu tumeongelea njia mbali mbali za kutrade forex. Embu niambie kwenye comment hapo chini umechagua wapi kwenye part one na part two?

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x