!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Nini Cha Kujifunza Unapopata Winning Trades?Working on winners

Katika mambo ya msingi yaliyonisaidia ni kukomaa na trade zilizoleta faida. Yaani kwa lugha ya trading tunaita drilling or working on winners.

Uzi huu wa leo nitaongelea drilling on winners na kwa nini inaweza kukusaidia sana kufanikiwa kwenye trading yako.

Kama wewe ni trader mwenye plan yaani rule based trader ambaye unaamka asubuhi kufuata a well proven plan kila unapotrade, hili somo litakusaidia sana kupiga hatua moja kwenda nyengine.

Ninaposema drilling on winners simaanishi kuscale-in kwenye trade zilizo kwenye faida, hapana. Hii ni hatari sana na kuna uwezekano ukaharibu profitable trades endapo soko likaretrace kwa zaidi ya asilimia sabini ya ile impulse move. Hapa namaanisha kujifunza kwa undani zaidi na kufahamu kwa nini ile trade imefanya kazi perfectly.

Hii ni philosophia ambayo itakusaidia sana kupata mavuno yenye faida kadiri siku zinavyoenda. Wanajeshi wakiwa wanafundishwa masomo ya kivita kuna wale wanaonekana wako perfect na wengine wanakuwa sio perfect. Kundi la wale perfect soldiers ndiyo huchukuliwa kwa ajili ya mazoezi zaidi na mastery wakati wale wengine hupelekwa kitengo kengine. Je unafahamu ni kwanini wanafanya hivi?

Hawa perfect soldiers ndiyo watakao enda vitani wakiwa na odds kubwa sana za mafanikio kuliko wale wengine. Ni rahisi sana kurekebisha mambo madogo madogo kuliko kukomaza kitu ambacho ki uhalisia itachukuwa muda mrefu na ukiwaweka pamoja vitani hawa imperfect soldiers wanaweza wakasababisha error ambazo zita cost team nzima, hivyo basi wakufunzi huwachuja na kuacha kikosi makini kwa ajili ya kazi.

Nini Cha Kujifunza

Trader unatakiwa kuiga mfano huu kwani itakusaidia kuchuja takataka zote zinazoleta madhara kwenye statement yako. Chukulia mfano trader anayetumia TrendLine, Support & Resistance pamoja na signal kama strategy. Lakini kwenye signal akawa na signal 4 tofauti kwa mfano pinbar, tweezers, doji na kadhalika. bila shaka setup yake itakuwa kama hivi

Sasa, baada ya kutrade kwa muda mrefu na kupata data sahihi, trader anagundua kwamba kila akitumia signal ya Tweezer, trade hiyo haina risk reward nzuri au kila akitumia Doji trader anagundua kwamba trade zote alizotumia tweezer na doji kama entry signal zilileta hasara au hazikuleta reward nzuri.

Kama wewe ni smart trader hutakiwi tena kuendelea kutumia hizi entry signal tena. Unatakiwa kuchuja na kuachana nazo na kubaki na entry signal moja tu ambayo huwa na reward nzuri na kuwa faida. Huu ni mfano tu, sijasema kwamba pinbar ndio zinafaida sana, hii ni kazi yako nakuachia ukafanye research.

Ukifanya hivi kwenye kila sector kwenye trading yako kuanzia technical strategies, psychology na risk management everything that you will touch will turn to Gold. Utakuwa very accurate kwenye trade zako, utakuwa very profitable na una uwezo wa kufanya trading ikawa full time job.

Hata shule za msingi na sekondari hufanya mchujo kila mwisho wa mwaka ili kubaki na wanafunzi watakao weza kupambana kwenye mtihani wa taifa sasa kwanini na wewe usifanye hivyo kwenye trading yako?

Chuja system yako, baki na wanajeshi wenye uwezo, baki na wanafunzi wenye uwezo. Our Goal is to make money.

Natumaini umejifunza jambo la msingi sana leo. Hakika ukiweza kufanyia kazi utapiga hatua kwenye trading yako. Weka comment yako chini kama una maswali au hujaelewa chochote.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
setisfx
setisfx
5 months ago

Bro I can’t say enough. Asante sana

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x