!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

NI WAKATI WA KUBADILI STRATEGY YAKO.

Kila trader duniani kwenye soko lolote la kifedha yupo katika hali ya kutafuta au kuboresha strategy yake ya trading kila siku. Trading strategy bora ni kitu namba moja kinachofanya trader awe na nafasi ya kutengeneza faida sokoni kwa kipindi kirefu. Pale tu trading strategy inapokuwa sawa ndipo trader anaweza sasa kuanza kutafakari mambo mengine kama ya saikolojia ya trading n.k.

Ikumbukwe trading strategy humfanikisha trader pale anapozingatia na kuifuata strategy kwa kipindi kirefu. Lakini kuifuata strategy yenye mafanikio duni kwa kipindi kirefu ni ngumu sana.

Kwenye uzi huu mfupi nitaelezea viashiria kadhaa kwamba huu ni wakati sahihi wa kufanya mabadiliko ya strategy yako.

Umetrade mara 25 au zaidi na Net P&L yako ni hasara

Huu ni wakati wa kusimamisha trading na kuangalia nini unafanya ambacho hakipo sawa. Ukishafanya utafiti kwenye matokeo yako na kila kitu kipo sawa, yaani ulifuata sheria zote, basi ni wakati wa kubadili strategy.

Umetrade mara 25 au zaidi na net P&L yako ni break-even au faida kidogo ukilinganisha na matarajio yako.

Hapa siyo vyema kubadili strategy yako, bali ni wakati wakufanya analysis kwenye matokeo yako ujue ni mazingira gani unapata faida sana na mazingira gani unapata hasara sana kisha weka nguvu zako zaidi kwa kutrade tu mazingira unayopata faida sana na kuacha kutrade mazingira unayopata hasara sana.

Trading strategy haiendani na tabia yako.

Kuna trading strategy ambazo haiziwafai watu wasio na uvumilivu wa hali ya juu na kuna strategy ambazo haziwafai watu ambao sio wachangamfu. strategy za kushikilia trade kwa muda mrefu yaani (swing trading) huwafaa watu wenye uvumilivu wa hali ya juu kuona faida zikipungua na kuongezeka lakini ukiwa si mtu mvumilivu sana unaweza ukajikuta unaharibu trade za namna hii kabla hazijakomaa. Strategy hii huwa na drawdown kubwa yaani winning percentage yake ni ndogo na reward zake ni kubwa huitaji mtu mvulivu kwenye vipindi virefu vya hasara. kusoma zaidi juu ya strategy zenye win ratio tofauti tofauti bonyeza hapa.

Watakao weza kuketi mbele ya kompyuta kutwa nzima wakifungua na kufunga trades.

Strategy ambazo zinamuhitaji trader kuketi mbele ya kompyuta kwa muda mrefu kama scalping haziwafai watu ambao si wachangamfu. Kama strategy yako haiendani na tabia yako, ni vyema kuachana nayo. Ni vyema ukatafuta strategy itakayo endana na wewe kwa sababu mafanikio kwenye trading sio jambo la ghafla, ni hatua kwa hatua na safari ya miaka.

Trader kutokuielewa jinsi strategy inavyofanya kazi.

Ili trader awe na uwezo wa kufanikiwa na strategy yeyote, lazima awe na ufahamu jinsi inavyofanya kazi kiundani na kuvumilia kipindi cha mitikisiko na changamoto ya hiyo strategy. Hii ni muhimu zaidi kwa traders wanao tumia EA’s Robots, ni vyema kuelewa jinsi EA inavyofanya kazi kwa undani kabla ya kulinunua au kulikodisha.

Trading strategy yako ni Baridi.

Trading strategy baridi ni ile strategy ambayo hufanya kazi kwenya aina moja ya soko tu, yaweza kuwa soko la kutrend au la kuconsolidate. Sasa strategy kama hii yakupasa kuibadili pale soko linapobadilika au kuacha kuitumia pale soko linapobadilika.

Muhtasari.

  1. Umetrade mara 25 ukaishia kupata hasara na hakuna faida kabisa. SIMAMISHA TRADING BADILI STRATEGY.
  2. Umetrade mara 25 hakuna faida hakuna hasara /breakeven au faida kidogo. ENDELEA KUTRADE NA HYIO STRATEGY, IBORESHE ZAIDI.
  3. Trading strategy haiendani na tabia yako. SIMAMISHA TRADING BADILI STRATEGY IENDANI NA WEWE.
  4. Umeshindwa kuelewa strategy inatendaje kazi? JIFUNZE INAVYOFANYA KAZI AU BADILISHA TAFUTA UNAYOWEZA KUELEWA.
  5. Trading strategy yako ni baridi. BADILIKA NAYO AU SIMAMISHA TRADING IKIWA MAZINGIRA RAFIKI HAYAPO.

Ni vyema kuwa na mfumo wa trading utakao weza kubadilika kutokana na mazingira kwa sababu kubadili strategy mara kwa mara sio jambo jema ila ikumbukwe mara nyingine inabidi ili kupata matokeo chanya katika trading.

Kujifunza mbinu mbadala ya trading itakayo kuwezesha kutrade katika mazingira tofauti ya soko bila kuwa na wasi wasi wa mabadiliko ya soko bonyeza hapa.

Napenda kukushukuru wewe msomaji kwa kuchukua muda wako kusoma uzi hii mfupi, nakukaribisha kuendelea kujifunza na kusoma zaidi kupitia tovuti yetu.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x