!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Ni Hatari Sana Ku Break-Even Trade Zako.Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Nafahamu kwamba kuna watu watasema huyu brother mbona kama amepatwa na wazimu ila kabla hujapanick na kuanza kujudge embu tulia kwanza na kusoma uzi huu kwa makini sana kwani unaweza ukakufungua kimawazo.

Kwanza kabisa break even nini kwenye forex trading?

Hiki ni kitendo cha kusogeza stoploss yako mpaka kwenye entry yako au juu kidogo ili trade iki retrace au kugeuka mazima uweze kutolewa bila faida au hasara. Watu wengi wamekuwa wakitumia hii njia kupunguza risk ila inaonekena inaongeza risk maradufu haswa kwa upande wa winning trades. Huyu ndo mchawi wa traders wengi kufikia mafanikio kwani wanaharibu trade nyingi sana ambazo hazijakomaa.

Kama umeshawahi kuswing trade zaidi ya mwaka au zaidi utakuwa unanielewa kwamba mara nyingi unapo hold trade zako zaidi ya asilimia 80-90 ya trade hurudi kwenye entry mara nyingi sana kabla ya kufyatuka kuelekea upande wako. Binafsi kama nisingeacha ku break-even ningejikuta nimeharibu trade nyingi sana na kuelekea kufunga mwaka kwa hasara au bila faida kabisa kwa sababu kwa karibu trade zote zilirudi kwenye hasara na kukaa zaidi ya siku tatu mpaka wiki kisha kuendelea na safari. Embu imagine ningekuwa nimesogeza stoploss yangu mpaka kwenye entry (Break Even) je ningebaki salama?

Siwezi kuongelea upande wa day traders lakini kama unahold trade zako zaidi ya siku moja wewe ni swing trader na kubreak even trade zako si salama kama unataka kuwa profitable mwisho wa mwezi au mwaka.

Break Even Ni Woga, Inaonyesha Ni Jinsi Gani Hujiamini Na Maamuzi Yako

Kuliko kuharibu trade yenye potential ya kukupatia faida mara 10-20 ni bora nikakubali hasara ndogo (Calculated Risk). Hii ndiyo philosophy yangu kwa sababu by the time trade imetembea bila ya mimi kuwepo, kile kiasi nlichokuwa nakilinda kisipotee hakitakuwa na maana tena kwani ni sawa na punje ya mchanga kwenye bahari.

Jiamini. Kila unapo execute trade zako, amini kwamba you are right kwa sababu umefuata sheria zote za ile trade. Ukiona mtu amebreak even kuna mambo kadhaa ambayo yananijia kichwani na kwa asilimia 99.99 huwa niko sahihi.

  1. Trade iliyochukuliwa haikukidhi vigezo, kitaalamu tunaita bad trade.
  2. Risk amount ni kubwa kiasi cha kufanya trader awe muoga na kuamua kulinda kitita chake.

Naamini break even ni another risk on top of another. Yaani ni sawa na kujingiza kwenye lion cage. Muda mwengine market movers just come to test the entry zone just to liquidate your positions, kumbuka sio wewe bali ni millions of traders wanakuwa na the same psychology. Sasa akikuta stoploss yako pale je unadhani utabaki salama?

Its okay to be different, one loss can be repaid on the next swing na ukasahau what happened.

Ukikutana na soko lenye tabia ya kuwa na steep retreacments inawezekana kwamba unaweza usipate trade hata moja na kuelekea kuwa na mwaka mbovu.

Nimalizie kwa kusema pima kwa makini nilichokuambia na kama utaona kinafaa unaweza kukitumia ila kama hakita leta maana yeyote kwako si lazima ukifanye.

Unaweza ukazidisha win ratio kwa karibu asilimia 50 kama utaacha kubreak even na kualicha soko litembee naturally.

Natumaini umejifunza kitu, nakaribisha majadiliano chini kwenye comment.

Jifunze zaidi kuhusu trading Forex kutoka kwa team ya pro traders.

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x