
NAMNA YA KUTRADE FOREX KAMA UNAANZA NA MTAJI CHINI YA $2500.
Kipindi cha high returns (mtaji chini ya $2500)
Hiki nikipindi ambacho utahitaji ustadi mkubwa na utulivu wa hali ya juu. Utaanza na mtaji mdogo ambao utakuwa una risk kiasi kisichopungua $10 kwenye kila trade. kwa kuwa unaanza na mtaji mdogo itakubidi kuwa aggressive sokoni ili uweze kukuza kiasi hicho kwa haraka kifikie kiasi cha mtaji ambacho lengo lako litabadilika kutoka kwenye kukuza account haraka kwenda kwenye lengo la kulinda akaunti na kutengeneza faida endelevu sokoni.
Ukweli ni kwamba kurisk $10 kama unaanza na mtaji chini ya $500 kuna hatari ya drawdown kubwa inayoweza kusababisha account kuteketea lakini sasa utafanya nini kama huna namna nyingine yoyote ya kupata mtaji mkubwa? Mimi pia nilikua sina namna nyingine yeyote zaidi ya hii njia, kuliko kukukubali umaskini nilisema nitajaribu hata mara mia moja lakini nikiweza mara moja tu nitakuwa na mtaji wakufanya forex vizuri.
Profxtigers hii tunaita “firepovertystrategy” yaani kwa mfano hai tunaweza kusema una risk sokoni pesa ya Tshirt $10 kupata pesa ya smartphone $200 kisha unachokua faida hiyo ya smartphone $200 una risk yote kupata pesa ya gari $4000 hapa tayari unakuwa na mtaji wa kutrade forex vizuri na kufuata usimamzi wa fedha mzuri bila wasiwasi wa faida ndogo ndogo sana.
Utahitaji kuwa na broker mwenye leverage isiyopungua 500:1 Tuseme mtaji unaonza nao ni $50-$500. Kwenye huwo mtaji wako utarisk $10 tu kwenye fursa yenye risk to reward kubwa, inatakiwa uwe na risk reward isiyopungua 1:20 yaani kama utarisk $10 faida yako isipungue $200 kisha utachukua hiyo $200 yote na kuirisk katika fursa ya 1:20 tena nakupata $4000.
Tunaona kwamba utahitaji trade mbili tu kufikia malengo, lakini sio trade mbili tu bali trade mbili kubwa tunachokifanya ni tutatrade pair moja tu nakuielewa kwa undani mfano tuchukue mfano “GBPUSD” kwenye pair kama hii tutatafuta fursa yakuingia sokoni na stoploss ya pips 25 na Takeprofit ya pips 500 kwakufanya hivyo ndio tutakuwa na risk to reward ya 1:20.
TRADE YA KWANZA.
KIASI | |
STOPLOSS | PIPS 25 = $10 |
PAIR | GBPUSD |
KIASI CHA RISK | $10 |
TAKEPROFIT | PIPS 500 = $200 |
RISK : REWARD | 1:20 |
LOT SIZE | 0.04 |
Mbinu hii itahitaji mtu mtulivu wakutafuta fursa kwenye timeframe za juu ya masaa manne H4, ya siku D1 au ya wiki W1
Ukifanikiwa trade ya kwanza utakuwa na faida ya $200 hapa ndipo safari yako itaanza kuelekea $4000.
TRADE YA PILI
KIASI | |
STOPLOSS | PIPS 25 = $200 |
PAIR | GBPUSD |
KIASI CHA RISK | $200 |
TAKEPROFIT | PIPS 500 = $4000 |
RISK : REWARD | 1:20 |
LOT SIZE | 0.8 |
Kufikia hapa utakuwa namtaji ulionza nao awali jumlisha $200 na $4000 za faida.
Ukishafikia hatua hii elewa kwamba ulichokuwa unakifanya awali ilikua ni mbinu yenye hatari kubwa ya kupoteza mtaji wako hivyo inabidi uhamia kwenye mbinu mpya.
That’s mok umeongea kitu muhimu sana. Be blessed
Ahsante sana kwa kutuongezea maarifa kupitia threads mbalimbali Mungu awatunze
Shukran Kwa elimu hii
Thank you