!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

MBINU BORA YA KUWEKA STOP LOSS ORDER.STOPLOSS ORDER KULINGANA NA MARKET VOLATILITY (VOLATILITY STOP)

Volatility ni kiasi ambacho soko linaweza kusogea kwa muda fulani. Kwa maneno rahisi, Volatility ni kiasi ambacho soko linaweza kusogea kwa muda fulani. Kutambua ni kwa kiasi gani cha pips Currency Pair unayo trade inatembeaga ita kusaidia kuweka kiwango sahihi cha Stop Loss ili kuepukana na kutolewa hovyo katika trade zako.

Kwa mfano, ikiwa unajua GBP / USD imesogea takribani pips 150 kila siku kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita basi kitendo cha kuweka Stop Loss Order yako kwa pips 20 itakufanya utolewe nje ya trade mapema kwa intraday move ndogondogo. Kujua wastani wa volatility hukusaidia kuweka Stops zako katika sehemu salama na kuipata trade yako nafasi ya kutosha kupumua.

Nitajuaje volatility ya soko

Njia rahisi ya kujua volatility ya Currency Pair ni kwa kutumia kipimo cha Average True Range (ATR) kinachopatikana kwenye Charting Platform karibia zote ikiwemo ambayo mabroker wanatoa bure platform maarufu ya MT4.

Kinachohitajika kwenye ATR ni uingize “kipindi” au kiwango cha Bars/Candlesticks, au Muda ili kiweza kukupa hesabu ya wastani ya vipindi hivyo.

Kwa mfano, ikiwa unaangalia chati ya siku, na ukiingiza “20” kwenye Settings za ATR, basi kipima cha ATR kitahesabu kiwango cha wastani cha volatility ya Currency Pair kwa siku 20 zilizopita.

Ukiangalia hapo kwenye chart panel ya chini upande wa kushoto juu utagundua ATR ni pip 139 hivyo kama uta trade GBPUSD kwenye Daily timeframe basi stoploss yako isipungue hiyo ATR pia unaweza ukatafuta ATR kwenye timeframe za chini itategemea wewe mwenyewe unatumia timeframe gani, jinsi unavyozidi kushuka timeframe za chini ndivyo ATR yako itapungua.

STOPLOSS ORDER KULINGANA NA PRICE CHART.

Mbinu hii ni yakuweka stoploss order kulingana na price chart inavyosema, stoploss hukaa juu au chini ya candlestick pattern ambazo price chart imetengeneza. Pattern hizi zaweza kuwa ni za muda mrefu au muda mfupi.

Tuangalie mfano mmoja wapo wa hii patten (pinbar) ya muda mfupi ambayo inatengenezwa na candlestcik moja tu.

Hapa tunaona stoploss inakaa juu kidogo ya mkia wa candlestick kama ni bearish pinbar candle na chini kidogo ya mkia wa candlestick kama ni bullish pinbar candle.

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
WAZIRI
WAZIRI
3 months ago

Ebana shukrani sana kwa elimu muhimu unayotupatia kaka.
Sasa kwa trader akitaka stoploss yake isizidi pips 25…ATR inabidi isome ngapi ?

Pages: 1 2 3

3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x