!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

MBINU BORA YA KUWEKA STOP LOSS ORDER.

Wajibu namba moja wa kila trader iwe kwenye Forex au soko lolote la kifedha ni kuhifadhi mtaji na kudhibiti risk sokoni. Kuna msemo unasema “ukiweza kusimamia na kuhifadhi mtaji wako vizuri basi faida zitajijaza zenyewe”

Kwenye Forex trading namna kuu ambayo traders hutumia kudhibiti risk na kuhifadhi mitaji yao ni kwa kutumia stoploss order.

Stoploss order ni nini?

Ni order ambayo trader huweka sokoni akimwambia broker wake huu ndio ukomo wangu wa hasara endapo bei itaenda kinyume na matarajio yangu. Order hii huwekwa kupitia trading software ambayo trader hupewa na broker wake.

Chukulia mfano trader kanunua GBPUSD katika bei ya 1.28400 anaweza akaweka stoploss order kwamba bei ikienda kinyume na matarajio yangu yaani ikishuka basi ukomo wangu wa hasara uwe katika bei ya 1.28000. Hapa trader huyu endapo bei itaenda nje na matarajio yake atakuwa amepata hasara ya pip 40.

Pia kwa mfano trader ameuza GBPUSD katika bei ya 1.28400 anaweza akaweka stoploss order kwamba bei ikienda kinyume na matarajio yangu yaaani ikipanda basi ukomo wangu wa hasara uwe katika bei ya 1.28800. Hapa trader endapo bei itaenda nje na matarijio yake atakuwa amepata hasara ya pips 40.

Bei za forex pairs hutembea juu au chini kupitia kuongeza ua kupungua kwa uniti za pips. Lakini sisi kama forex trader tunapoingia sokoni lengo letu ni kutengeneza pesa au kudhibiti upotevu wa pesa taslimu na sio pips.

Hivyo yatupasa kujua namna ya kuzi badilisha izi pips za sokoni kuwa pesa ili tunapo risk izi pips tujue tuna risk kiasi gani kama hasara na tutapata kiasi gani kama faida. Hapa ndipo position size calculator ya forex inakuja kufanya kazi.

Tuchukulie mfano wa awali wa kubuy GBPUSD trader alikua ana mtaji wa $2500 na kiasi chake cha kurisk ni asilimia 3% sawa na $75.

Kutokana na hesabu iliyofanyika kwenye position size calculator juu hapa inaonekana kwamba ili stoploss ya pip 40 iwe ina risk asilimia 3% ya mtaji yampasa trader kutumia position size ya standard lot 0.18.

Kila unapoweka stoploss sokoni yakupasa ujue una risk kiasi gani cha mtaji wako ili endapo trade unayoweka ukakosea basi iwe hasara unayoweza kuimudu.

Kwakua stoploss order ndiyo kipima hasara chetu kwenye trading basi yatupasa kujua namna yakuweka hizi stoploss order katika maeneo salama zaidi.

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
WAZIRI
WAZIRI
8 months ago

Ebana shukrani sana kwa elimu muhimu unayotupatia kaka.
Sasa kwa trader akitaka stoploss yake isizidi pips 25…ATR inabidi isome ngapi ?

Pages: 1 2 3

3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x