!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Mambo (6) ya Msingi ⚖ kuzingatia kwenye Trading 2020.Leo tar 25 Dec 2019 ikiwa ni siku kuu ya krismas kuelekea mwaka mpya 2020 nimeona nitumie muda huu kukumbusha maswala ya 6 ya msingi kwa trader yeyote ambaye anataka kufanikiwa kwenye biashara hii ya Forex. Kwanza kabisa haijalishi mwaka umekuwa mgumu kiasi gani kwako, au umechoma account ngapi mwaka huu. Ujumbe huu unaweza kukusadia kwa asilimia kubwa sana kufanya mapinduzi ya trading kwa mwaka 2020.

Nimekuwa nikitrade kwa takribani miaka mingi sasa, Nakumbuka mwaka 2016 ndio ilikuwa mara ya kwanza kusikia neno Forex Trading kutoka kwa rafiki yangu Moki.Jr. Naweza kusema hapo ndo safari ngumu ilipoanzia, Kwa vile nilikuwa na access na pesa za pocket money chuoni basi nilitumia sana zile fedha kutrade na sikuwahi hata siku moja kupata faida. Faida ndogo ndogo zilizokuwa zinapatikana ilikuwa ni kama kupunguza hasara ambazo zimeshatokea. Nililivamia soko kwa hasira ya kutoka kwenye umaskini haraka ila nikajikuta kwenye umaskini maradufu. Kwa miezi 6 straight hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha kushindwa kumudu gharama za maisha kila siku.

Hapa ndo nilipojifunza somo la kwanza kwamba Forex Trading Sio Get Rich Quick Scheme. Ndani ya miezi sita nilitumia strategy kama 10 tofauti bila mafanikio. Kibaya zaidi nilitrade bila kufuata kanuni za risk management na kujikuta niko kwenye hasara kubwa yaani drawdown amabazo ki ukweli huwezi kurecover. Hili likawa somo la pili kujifunza baada ya kupoteza pesa kiasi kikubwa sana.

Safari haikuishia hapo bwana, siku zilizidi kusonga mbele lakini kwa wakati huu nilitumia strategy moja na ukweli ni kwamba nikaanza kuona mwanga lakini bado kuna makosa mengi ambayo nilikuwa nayafanya, hivyo hasara hazikukoma risk management ilinikwamisha sana na haikuchukua muda tena account nyengine ya dollar 300 ikawa imekwenda na maji 😅.

Katika pita pita zangu mtandaoni kutafuta material nikakutana na kitabu kimoja cha market wizards ambacho kimeeleza historia ya traders mashuhuri walioahi kutokea kipindi cha nyuma huko. Nikanunua kile kitabu amazon. Nikasoma kitabu chote. Kitu cha msingi nilichojifunza kwenye kile kitabu, traders wote waliochoma pesa zao ni kwamba walikaidi kanuni ya one percent. Wengi walipiga pesa lakini ego zikawapanda wakapuuzia risk management na hivyo wakaanguka tena. Hili likawa jambo la tatu baada ya risk management. Kuna mtu anakwambia ana trade kwa risk management ila anarisk 5-10% per trade, kibaya zaidi ana overtrade aisee dot’s zikaanza kumake sense.

  1. Forex sio get rich quick scheme.
  2. Focus na strategy moja.
  3. Risk management ndio mpango mzima.
  4. One percent ina mchango mkubwa pindi unapokuwa kwenye draw down.
  5. Risk management haina faida kama una overtrade.

Baada ya kujifunza haya yote mwaka ukawa umekata na mfukoni sina mia. Basi nikaanza jidunduliza kutrade na account za dollar 20,50,100,200 etc. Sasa yote niliyojifunza ndani ya mwaka vikawa irrelevant kama sikuwa na mtaji unaoeleweka. Nikawa najaribu kuforce lakini wapi hakuna hata kimoja ningeweza kuaaply kwasababu mtaji ni mdogo.

Hiko ndo kinawakwamisha traders wengi, mtaji ni changamoto sana hii hupelekea traders kuingia na tamaa na kurisk account nzima na hapo ndo anapozamisha meli. Baada ya kuchoma account ndogo ndogo kadhaa nikaona huku nakoelekea sina future na unaweza kuzeeka maskini. Kwa vile nilikuwa bado mwanafunzi nikaanza kusave kila senti nayopata Niliishi below means kwa muda sana hadi kupata mtaji wa kuanzia. Nikalipia mentorship online ili niweze kupigilia nondo, Forex ikawa 24/7 and the rest ni historia.

Kama wewe ni trader unaeanza na upo kwenye position niliyokwepo basi usikate tamaa kwani inawezekana sana issue ya msingi ni kujielewa na kufocus kwenye vision yako. Tatizo traders wengi wanataka kuondoka kwenye umaskini haraka sana, wala siwalaumu hata mimi niliwaza hivyo ila baada ya kushinda humu sokoni nikaona haiwezekani ila unaweza kutengeneza fortune ukiwa mtulivu na kuwekeza muda wako zaidi ya masaa elfu kumi.

Hints ziko nyingi sana ila chache ni za msingi na endapo ningeambiwa mapema pengine nisingekuwa hapa nilipo. Nitaendelea kushare hints mbali mbali na nyie kadiri ya uwezo wangu.

Tunapo elekea mwaka 2020 Mungu akijalia basi ukawe wa mafanikio sana kwako jaribu kufuata hints nilizokupa hapo juu na safari yako haitachukua muda kama ilivyo nichukua mimi. Nikuhakikishie kwa asilimia 100, suala na kuchoma account itabaki kuwa historia.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x