!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Mambo Haya Yatakufariji Endapo Utachoma Account.

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo

Karibu kila trader kwenye masoko ya kifedha amewahi kukumbana na hii changamoto aidha kwa kujaribu, kutokujua au tamaa za kutaka kulichakachua soko. Naomba niwe wa kwanza kukuambia kwamba usichukulie poa kuchoma account kwani tabia hii ikiendelea huwa inakuwa sugu na huenda isikome hadi utakapoacha trading.

Somo la leo nitaongelea jinsi ya kujifariji endapo utakutana na hii changamoto. Muda mwengine kuchoma account huumiza sana roho na wengine hufikia hatua ya kushindwa kuendelea na hii biashara kwani huenda akawa amepoteza kiwango kikubwa sana cha pesa na pengine ilikuwa pensheni, mkopo au vijana wengine hufikia hatua ya kuchomoa pesa ya ada na kujaribu trading bila kuwa na ujuzi wowote. Katika hali hii lazima ukumbane na hii changamoto ya kuchoma account.

Nakumbuka account yangu ya kwanza kuungua ilikuwa ni ya dolla 1000 ambayo ilikuwa savings zangu za muda sana na ilipotea ndani ya siku moja tu, roho iliuma sana na lakini sikukataa tamaa kabisa. Nilichekecha mambo flani flani hivi amabyo yalinisaidia sana ambayo leo nitakueleza.

Kwanza kabisa naomba nikuambie kwamba, endapo utachoma account usijaribu kudeposit tena hata kama unapesa bank.

Kuna kitu kinatwa revenge trading, maana yake ni hasira ya kulipiza kisasi sokoni pale unapopata hasara. Masoko ya kifedha ni ya kibabe sana yaani huwezi kuyapiga bila kutumia akili ya ziada. Katika hali ile ya kuchoma account, akili yako hapo katika state nzuri na unaweza fanya maamuzi ambayo yanaweza kukucost kwa namna moja au nyengine kubwa likiwa kupata hasara mara mbili au tatu zaidi. Sasa usije ukafanya kosa hili tena, subiri muda upite huku ukitafakari kosa lilikuwa wapi.

Pitia Trade Iliyochomesha Account

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Setisfx
Setisfx
7 months ago

Thank you brother, ubarikiwe

Ramadhani
Ramadhani
7 months ago

Thank you my kaka, article hii imenilenga mimi kabisa, sitoeleza mengi ila tu ni kwamba nashukuru nimetoka kuchoma choma accounts lakini hii ni week ya tatu na refresh mind(figuring out my mistakes more in pyshology and mindset few in setups) sijafanya kudeposit tena japokuwa nilibaki na pesa ya trading nimefanya kutulia kwa muda ila sijawa na fikra mbovu. najifunza makosa yangu.

Pages: 1 2

5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x