!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

KWA NINI STRATEGY MAARUFU HAZIFANYI KAZI?Elewa trading usikariri trading

Ukitaka kufanikiwa na biashara sio vibaya kuiga biashara ya mtu mwingine lakini ubunifu ndio utakufanya ufanikiwe kwenye hiyo biashara ulioiga, hata kumzidi yule uliye muiga.

These 5 Things Happen to Your Brain When You Quit Drinking

Usipokuwa mbunifu utafeli kwasababu sasa utaanza kushindana na yule uliyemuiga na siku zote unaposhindana na mtu mwenye uzoefu zaidi, mtandao wa wateja zaidi yako na mtaji mkubwa zaid yako lazima utafeli. Mfano unaweza kuiga kwa mtu biashara ya kuuza vitumbua lakini wewe ukawa mbunifu ukaongeza dhamani ya vitumbua vyako kwa kuweka chocolate katikati ya vitumbua ikawavutia kwa macho na kwa ladha wateja wako wapya.

Mimi nimesoma vitabu vingi sana vya trading lakini hakuna mtu alienifundisha ninachokifanya kila siku ni ubunifu wangu mwenyewe, pia kwako wewe sio vibaya kujifunza trading kupitia watu wengine au vitabu lakini ya kupasa kuwa mbunifu kadri siku zinavyokwenda yaani angalia madhaifu yako ni yapi na ubora wako upo wapi kisha shikilia hapo kwenye ubora wako na ongeza ubunifu hapo.

Lazima ifike sehemu una mbinu yako yaki pekee yakuingia na kutoka sokoni. Mbinu hiyo unaweza ukaitumia wewe na watu wako wakaribu lakini ikishakuwa maarufu ikawa inatumika na ma millioni ya traders inakuwa changamoto sokoni kutokana na mvutano wa demand na supply.

Je yanipasa kutengeneza mbinu mpya kabisa ya trading.

Hapana sio lazima iwe mbinu mpya kabisa ya trading unaweza ukachukuwa mbinu kutoka kwenye vitabu mbali mbali mfano tuongelee price action hii ni approach kubwa sana ambayo unaweza ukawa mbunifu ukatengeneza mbinu yako yakipekee ya kuingia na kutoka sokoni ikakuwezesha kuwa tofauti na traders wengi sokoni. Pia unaweza ukachukua mbinu kutoka kwa trader ulikuwa na uhakika kwamba anaetengeneza faida endelevu sokoni ukatrade nayo ikakupa mafanikio kwa sababu kama inampa faida endelevu muda huo basi hiyo mbinu sio maarufu kabisa.

Ukisikia soko linabadilika kimoja cha visababishi nisisi traders wenyewe soko lina badilika kutokana natunavyo trade na tabia zetu sokoni yaani demand na supply Ninachotaka ukielewe kichwani mwako ni kwamba forex startegy nyingi hua haziishi milele lazima ubadilike pia uweze kubadilika na soko. Lakini jinsi strategy yako inavyozidi kuwa yakipekee ndivyo uwezekano wake wakuishi miaka mingi unaongezeka.

Subscribe
Notify of
guest
12 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Brian
Brian
2 months ago

Naamini hii mala yakwanza nime fumbua machoyangu daaaa! Shuklan.

Zephania enos
Zephania enos
2 months ago

Naomb mafunzo zaidi

Manasejr
Manasejr
2 months ago

Kuna mambo mazuri na matamu unaongea, big up bro

Mr.tarq
Mr.tarq
2 months ago

Brother nisaidie tafadhal ni juwe hii biashara nakuomba

ray_heriel
ray_heriel
2 months ago

Word Brother.

baraka abdalah
baraka abdalah
2 months ago

Asante sana bro kwa darasa zuri….nlikua naomba kuuliza we kn ww hua unatumia mbinu gan inayofanya uwe vizur sokon

Pages: 1 2 3

12
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x