!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

KWA NINI NA TRADE FOREX PAIR MOJA TU.Kutrade forex pair tofauti sio diversification bali kutrade asset class tofauti ndiyo diversification.

Baadhi ya forex traders wanachanganya mambo wakijua kwamba wanapotrade forex pair tofauti ni diversification sio kweli soko lote la forex lina uwiano wa asilimia fulani kila forex pair ina uwiano na nyingine kwa asilimia fulani ukitaka kudiversify basi wekeza kwenye asset class tofauti.

Assect class ni kikundi cha mali za zinazofanana mfano kuna class ya Hisa, forex, hatifungani, real estate n.k

ukitaka kudiversify basi portfolio yake iwe hivi kiasi cha pesa unawekeza kwenye forex kingine kwenye hatifungani kingine hisa.

Mimi sio mtu ninae amini sana kwenye diversification tena haswa pale unapoanza safari yako ya uwekezaji

Si semi diversification ni kitu kibaya lakini kwa pale unapoanza uwekezaji unakuwa huna pesa ya kutosha ya kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja. Mwanzoni mtaji mkubwa ni nguvu zako mwenyewe huna pesa yakuajili mtu akufanyie trading au awekeze kwa niaba yako. Shika kimoja tu mwanzoni kwa kutia muda wako wote katika trading utajenga msingi mzuri ambapo baadae utaweza kudiversify kwa kuchukua faida zako za trading ukuwekeza sehemu tofauti mfano unaweza uka nunua hatifungani za makampuni ambapo utalipwa interest ya asilimia flani bila kuhitaji muda wako au nguvu zako uku ukiendelea kufanya trading yako. Pia unaweza kuwekeza kwenye mali zisizohamishika kama nyumba za kupangisha ukawa una pata kodi kila mwezi na ongezeko la thamani ya nyumba, hivi ni vitu ambavyo havihitaji muda wako wote.

Hivyo baki na forex trading kwanza na kwenye forex, shikilia ku trade forex pair moja ijue vizuri tengeneza faida endelevu kisha chukua baadhi ya faida diversify kwenda kwenye asset class tofati kama Vito vya thamani, mali zisizo hamishika, hisa, hatifungani n.k

HITIMISHO

Kwako wewe inaweza ikawa GBPUSD Kama mimi pia inaweza ikawa pair nyingine yoyote ilimradi tu iwe pair ambayo imekuwa ikikupa faida mara nyingi zaidi. Kisha anza kuisoma hiyo pair muda gani ina volume kubwa, muda gani ukiitrade inakupa hasara zaidi, muda gani inakupa faida zaidi na setup gani zina kupa faida zaidi na forex pair hiyo kisha shikilia sehemu ambazo zinakupa manufaa zaidi kwakufanya hivyo utakua unatengeneza faida endelevu.

Nikushukuru kwa kutumia muda wako kusoma uzi huu nina imani nitakuwa wamchango mkubwa kwa namna moja au nyingine kuboresha trading yako pia nakuomba uwatumie uzi huu wenzako ili pia wapate kunufaika. Hadi siku nyingine tena kwa heri.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
14 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Goodnardo Elioth Jr
Goodnardo Elioth Jr
4 months ago

I got you Brother working on it now….!!

Goodnardo Elioth Jr
Goodnardo Elioth Jr
4 months ago

Elaborated Smoothly….️

Joshua
Joshua
4 months ago

Shukrani kwa Maarifa

Kidonation32
Kidonation32
4 months ago

Iko pouw xna bro

Constantine kalangi
Constantine kalangi
3 months ago

Ni muda Gan gbp/usd uki I trade inakuwa hasaraa zaidii nilikuwa naomba ufafanuzi hapo na ni muda gani uki trade inakupa faida, muda gani has a ni mzuri

Ramadhani
Ramadhani
3 months ago

Too late to read the thread, but i got the entire point!! added it to my Brain!! Thanks Master

Pili Nkumbi
Pili Nkumbi
2 months ago

Shukrani sana,hakika nimejifunza kitu hapa. Ubarikiwe

Pages: 1 2 3

14
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x