!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

kujifunza forex kwa kiswahili

Foreign Exchange (FOREX)

Forex au “Foreign Exchange” kwa lugha ya kiswahili ni ubadilishaji wa fedha za kigeni. Embu chukua mfano unasafiri kwenda marekani ila mfukoni una pesa taslimu za kitanzania laki mbili na thelathini (230,000/-) unafika airport unagundua kwamba hautaweza kuzitumia pesa hizo ukiwa marekani hivyo unafanya maamuzi ya kuingia bank au beuro de exchange iliyo karibu na wewe ili uweze kubadilisha pesa. Unapo mpatia cashier zile fedha taslimu za kitanzania yeye anazichukua na kukupatia pesa kiasi cha dola 100 za kimarekani. Hapo unakuwa umeshajihusisha kwenye soko kubwa la fedha duniani. Kila nchi huwa na viwango vyake vya ubadilishaji (Exchange Rate) mfano $1 = Tzs 2300/- ndiyo maana baada ya kubadilisha zile fedha bank uliweza kupatiwa dola 100 za kimarekani. Exchange rate hubadilika mara kwa mara kutokana sababu mbali mbali za uchumi na siasa.

Wakati naandika uzi huu dola 1 ya kimarekani ilikuwa sawa na pesa taslimu za Tanzania shillingi elfu mbili mia tatu na ishirini (2320/-) yawezekana ikawa tofauti siku utakayosoma uzi huu.

Soko la fedha duniani ni kubwa sana kufikia ujazo wa trillioni 6.6 kwa siku kulingana na takwimu za mwaka 2020. Hii inafanya soko la fedha kuwa soko kubwa zaidi kuliko masoko yote ya hisa duniani ukiyakusanya pamoja.

Kwa mfano niliokupa mwanzoni wa pale airport tumefanya kitu kinaitwa traditional currency exchange kitu ambacho sio focus yetu. Sisi tutafocus sana na kitu kinaitwa Online Forex Trading

Online Forex Trading

Hii ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni mtandaoni. Miaka ya nyuma ilikuwa ni ngumu sana kutokana na changamoto za teknolojia lakini kuanzia miaka ya 95 na kuendelea online forex trading ilirahisishwa sana hadi kuruhusu watu wa kawaida (Retail Traders) kuifanya. Ilikuwa sio kawaida kwani zamani ulihitaji mtaji mkubwa sana kuanza kutrade forex lakini baada ya mapinduzi ya teknolojia kila mtu anaweza sasa kufungua account kwa broker na kuanza kutrade forex mtandaoni hata ukiwa na mtaji mdogo kuanzia dola 50, unachohitaji ni laptop na internet connection.

Unaweza kujionea mwenyewe jinsi forex trading illivyokuwa miaka ya themanini na tisini kabla ya online technology kwenye video hii: HOW FOREX WAS TRADED IN THE ’80S AND ’90S.

Mahitaji Muhimu

Kama nilivyosema awali kwamba sisi muda wote tutafocus na online forex trading, kuna mahitaji muhimu sana ambayo utahitaji ili uweze kutrade forex.


1. Laptop na Internet Connection

Hizi ni nyenzo muhimu sana kwa sababu itakuwezesha kupata access ya ile trading software ya Metatrader 4 au 5. Software hii itakuwa installed kwenye laptop yako au simu ya mkononi ambayo utatumia kuweka order zako. Vile vile utatumia sana laptop yako kujisomea mambo mbali mbali kuhusu forex hivyo ni muhimu sana. Usiwe na shaka pia kwani software hizi ni bure na utapewa na broker.

1. Laptop na Internet Connection

Hizi ni nyenzo muhimu sana kwa sababu itakuwezesha kupata access ya ile trading software ya Metatrader 4 au 5. Software hii itakuwa installed kwenye laptop yako au simu ya mkononi ambayo utatumia kuweka order zako. Vile vile utatumia sana laptop yako kujisomea mambo mbali mbali kuhusu forex hivyo ni muhimu sana. Usiwe na shaka pia kwani software hizi ni bure na utapewa na broker.

2. Online Forex Broker

Bila broker au dalali hautaweza kutrade forex, yeye ndiye anahusika na kukupa software, access ya masoko duniani na vile vile kukulipa pesa wakati unapo pata faida. Ni vyema ukawa makini sana unapo tafuta forex broker kwa sababu ukiingia kwenye mikono mibaya broker anaweza kufanya safari yako iwe na machungu sana, Lakini usiogope kwani mwisho wa uzi huu nitakuwekea broker makini ambaye hana longo longo. Unaweza pia kusoma uzi wa msingi sana: JINSI YA KUMKAGUA ONLINE FOREX BROKER. Utakusaidia sana mbele ya safari utakapo anza kujitegemea.

3. Document Muhimu

Ukisha mpata online forex broker na kufungua account utahitaji document muhimu sana ili uweze kufanya uhakiki wa utambulisho wako (Proof of Identity) pamoja na makazi yako (Proof of Residency) Mara nyingi kwenye proof of identity utatumia document zilizotolewa na serekali kwa mfano Kitambulisho cha taifa au Leseni ya udereva

Vile vile kwenye utambulisho wa makazi utahitaji bank statement yako ambayo sio ya muda mrefu angalau kuanzia miezi mitatu nyuma. Zaidi ya hapo broker anaweza akaikataa. Bank statement inaonyesha anuani yako hivyo ni rahisi broker kuamini. Kumbuka wakati unafungua account broker atahitaji ujaze anuani yako hivyo ni vyema ukaweka anuani yako ambayo ipo kwenye bank statement. Ukiweka tofauti basi broker atareject application yako. Unaweza kwenda bank na kuomba statement yako au kama una online banking ukadownload kama pdf.

Sina Bank Statement Nifanyeje?

Nafahamu kuna watu ambao hawana bank statement au ikawa shida kuipata. Njia nyengine ambayo broker anaweza kukubali application yako ni Affidavit. Download document hii jaza kisha nenda kwa mwansheria agonge muhuri. Itakugharimu shillingi elfu 15 hadi elfu 20 kwa muhuri mmoja, baada ya hapo unaweza ukawasilisha kwa broker.

Jinsi Ya Kudeposit Mtaji Wako Kwa Broker

Ili uweze kutrade forex lazima uwe na mtaji, sasa utaniuliza huo mtaji nadeposit wapi? Jibu ni rahisi sana, itakubidi ufanye deposit kwa broker na ukishafanya hivi utaweza kuona mtaji wako kwenye metatrader. Kwa mfano ukideposit dola 100 itaonekana kwenye metatrade software ya broker wako.

Lazima uwe verified ili uweze kudeposit kwa hiyo ni vyema ukafuata maelekezo nliyokupa kwenye aya za awali hapo juu.

Ili uweze kudeposit mtaji kwa mabroker wengi itakubidi uwe na bank account yenye visa card usijali sana kuhusu kuwa na dola account, sio lazima kwa sababu bank itabadilisha fedha automatically kuwa dola kisha kutuma kwa broker kama illivyo. Unaweza kufungua account kwenye bank kama Absa, FNB na CRDB haijalishi as long as bank ina visa card na account yako in uwezo wa kufanya online transactions. Baada ya kufanya deposit ni lazima itareflect hapo hapo kwenye metatrader yako.

Kwa nini nifanye forex?

Una weza ukaniuliza kwa nini nifanye forex? Je kuna mafanikio kwenye hii biashara? Napenda kukuambia kwamba katika biashara yenye utajiri mkubwa ni forex trading. Kuna watu mbali mbali wametajirika na trading kwa sababu ya uwepo wa margin trading. Unaweza ukawa na mtaji mdogo na ukapata mkopo bila dhamana yeyote yani kitaalamu unaitwa margin trading au leverage. Unaweza ukatrade ukubwa wa account balance yako hadi mara elfu moja. Kwa sababau hii unapata nafasi kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa, lakini leverage au margin trading ni risky kama hauna skill na haufahamu namna ya kutrade ndiyo maana utahitaji elimu.

George Soros aliweza kutengeneza zaidi ya dola billioni 1 za kimarekani alipotrade dhidi ya Pound mwaka 1992 kwenye trade moja tu.

Richard Denis Alitoa Dola 400 mpaka dola million 150 ndani miaka 8 tu.

Bill Lipschutz alitoa dola $12,000 aliyoachiwa kama urithi na wazazi wake na kufanikiwa kuikuza mpaka $250,000. Kisha akajiunga na Solomon Brothers na kuwa mkuu wa kitengo cha forex trading na kuweza kuitengenezea Solomon brother faida ya zaidi ya $300,000,000 kila mwaka.

Paul Tudor Jones alitoa dola $20,000 mpaka $1,000,000 na kufungua hedge fund yake ambayo kwa sasa ina manage zaidi za dola billioni 38.

fano wa Margin Trading

Hii account ilianza na mtaji wa $50 na kwenda hadi $6000 plus ndani ya muda mfupi tu.$50 – $6560

Mfano Account Hii ilitoka $100 hadi $900

Hii nayo ilitoka $50 – $1700

Elimu Ya Trading

Yote haya niliyo kueleza juu ni elimu ya awali tu. Trading ni industry kubwa inyohitaji elimu kwa undani sana. Kuna uwezekano mkubwa usipate mafanikio kwenye hii biashara kama usipopata elimu ya msingi. Hivyo basi jitahidi sana kusoma na kufanya research sana. Unaweza ukapitia website hii kuna masomo mengi sana kuhusu forex trading bure kabisa. Naamini kabisa ukiweka misingi imara lazima utafanikiwa tu. Kama ungependa kusoma trading na kuifanya iwe professional business unaweza kubofya hapa kujua zaidi.

Vile vile unaweza kusoma uzi huu wa msingi sana: FOREX TRADING TANZANIA, YAFAHAMU HAYA KABLA YA KUJIINGIZA KWENYE HII BIASHARA. Utakupa mwanga zaidi unapoamua kujiingiza kwenye hii biashara.

Mwisho kabisa ili kurahisisha process ya kufungua account ningekushauri utumie recommended broker ambaye ana uaminifu wa hali ya juu na ambaye nimekuwa nikimtumia kwa muda mrefu. Bofya Link kwenye story hapo chini.

Kama una maswali unaweza kuuliza kwenye comment chini hapo.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x