!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

KUWA MAKINI NA DHANA YA “KUBANA STOPLOSS”!Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Kumekua na wimbi la Traders kubana stoploss wakitafuta risk reward kubwa sokoni, angalia kwa makini utagundua wengi wanao jihusisha na hii dhana, Trading kwao imezidi kuwa changamoto kubwa.

kwanza kabisa nitafanunua risk reward na stoploss nini?

Stoploss, ni order trader anayoweka sokoni akimwambia broker wake kwamba bei ya bidhaa hii ya kifedha niliyonunua ikifika kwenye bei XYZ naomba unitoe maana huu ndio ukomo wangu wa hasara. Mfano trader amenunua EUR/USD kwenye bei 1.1840 anamwambia broker bei ikishuka mpka 1.1830 naomba ufunge order yangu, hapa order yake itafungwa automatically kwa hasara ya pips 10.

Risk reward ni tofauti kati ya (bei ulinunulia – bei ya stoploss) ukilinganisha na (bei ya utakayochukulia faida takeprofit – bei ulionunulia)

Tuchukue mfano wa EURUSD ya awali tuli nunua kwenye bei ya Entry price= 1.1840, bei ya stoploss ni 1.1830 na tuchukulie bei ya takeprofit ni 1.2040. Hapa tofauti ni ( 20pip stoploss ukilinganisha na 200pips takeprofit)

Ukanda mwekundu unaonesha Sehemu au kiasi cha risk na ukanda wa kijani unaonesha sehemu ya faida ( reward).

Ieleweke sipigi vita risk reward kubwa bali napiga vita kitendo cha kubana stoploss ili upate risk to reward kubwa.

Kwanini kubana stoploss ni hatari:

Kubana stoploss hupunguza winning percentage, Takwimu zinaonesha kila mara reward inapoongezeka kwa 1:1+1 hupunguza winning percentage kwa aslimia -10%. Ni ngumu sana kukuta mfumo wa trading wenye risk to reward kubwa na winning percentage kubwa. Mifumo mingi ya kutrade ambayo trader anakua na stoploss ndogo na risk reward kubwa hua na vipindi vya hasara virefu zaidi kuliko mfumo wenye risk to reward ndogo.

mfano wambinu za trading zinavyokuwa:

mfumoRisk Reward RatioWinning percentage
A1:190%
B1:370%
C1:550%
D1:7 30%
E1:1010%
F1:201%

Ieleweke mfumo wowote wa trading unaweza ukapata nao faida haijalishi win ratio au risk to reward ,ata wa “F” wenye winning percentage ya 1%

mfano hapa chini:

TradeFaida Hasara
1$1
2$1
3$1
4$1
5$1
6$1
7$1
8$1
9$20
10$1
TOTAL$20$9

Changamoto ipo wapi sasa? ni pale, Trader anapojiingiza kwenye mfumo wa risk to reward kubwa bila kujua changamoto yake ya vipindi virefu vya hasara tuchukue mfano wa juu hapo trader ana risk to reward ratio ya (1 Risk :20 Reward) stoploss zake ni 10 pips faida ni 200 pips, lakini kabla ya kupata io faida trader anapitia hasara 8 mfululizo yaani inabidi aendelea kuwa mchezoni kwa hasara 8 bila kuishiwa pesa ili apate faida ukifanya hesabu kweli atakua na faida mwishoni ya $11, Lakini ni traders wangapi wataendelea kuwa na moyo na mbinu kama hii bila kukata tamaa au kukosa kujiamini baada ya hasara 8 mfululizo. Kama wewe utaweza basi mfumo wa kubana stoploss na risk to reward kubwa unakufaa. Lakini kama unahisi hutoweza kuvumilia kitu hichu achana na mbinu za kutrade za namna hii.

Kwangu mimi nimejaribu zote mbinu za risk to reward kubwa na mbinu za risk to reward ndogo. Ukweli ni kwamba mbinu zenye risk to reward kubwa na winning perecentage ndogo kama ile ya E na F hukatisha tamaa na nilijikuta nikiishiwa hamasa ya trading na kuanza kuto kujiamini. Pia zenye risk to reward ndogo sana na winning percentage kubwa kama ile ya A hukujengea kujiamini kupita kiasi, kujiona wewe ni mtaalam wa soko yaani Mungu mtu wa soko hupelekea trader kutokua makini na sheria zake za trading mfano sheria muhimu za usimamizi wa mtaji. Ukienda kwa kujiamini huku, kupata hasara ya ghafla ni jambo la kawaida kabisa. kwa sasa nimechagua mbinu zenye risk to reward ya wastani na win ratio ya wastani. Mfano nikama ile ya C , inanifanya kuendelea kuwepo mchezoni bila kukata taamaa na pia kuendelea kujiamini kwa kiasi kwenye safari yangu ya trading.

Hali ya Trading katika mfumo C.

TradeFaida Hasara
1$5
2$5
3$1
4$5
5$1
6$5
7 $1
8$1
9$5
10$1
TOTAL$25$5

Kwa hali ya kawaida ya kiubinadamu traders wengi mfumo kama huu wa C utawafaa nakuwafanya waendelee kuufuata katika kipindi kirefu mpka kupata mafanikio makubwa, kuliko mfumo wa F ambao ni aina chache sana ya watu/traders duniani wenye uvumilivu wakuufuata katika kipindi kirefu.

Kama umependa nakala hii tafadhali toa maoni yako hapa chini vile vile share kwa rafiki yako wa karibu katika trading, mpaka siku nyingine tena, nakutakia mafanikio zaidi katika trading yako kwakheri na kila la kheri.

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Joshua
Joshua
5 months ago

Ahsante Sana Chief Unatuokoa na Hizi Nyuzi zako.Mungu akubariki Sana

Ramadhani
Ramadhani
5 months ago

Thank you bro once again, nimegundua kitu, ukitafta trades zenye R:R 1:3 plus na una winning rate ya 30% yaani unawin trade 3 katika trade 10, still i can make profit i can’t blow my account.

✌✌✌

Josh Julius
Josh Julius
3 months ago

Shukrani sana kwa hii thread hii kitu imenigusa sana binafsi pia nimewahi tumia RR ndogo ya 1:3 niligundua Win Rate ilikuwa kubwa sana ila hasara zake ni za ghafla na zilikuwa kubwa niliwahi jaribu RR kubwa ya 1:10 pia lakini trade za kuwin zilikuwa chache sana ila RR ya wastani kama hiyo 1:5 imekaa poa sana imebalance vyote nimejifunza kitu kikubwa. Mungu akubariki uzidi kubadili maisha ya watu

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x