!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Jinsi ya Kutengeneza 3.6 Million Tzs ($1400+) Kirahisi Kwenye Trading.

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Ni ukweli usiopingika kwamba zaidi asilimia 80 ya retail traders online wanashindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali ambazo tumezianisha kwenye makali hii : Why Most Traders Are Still Losing Money Up To Date. Zipo sababu nyingi sana na nina imani ukipitia makala hii unaweza kujifunza mambo mawili matatu yanayoweza kusaidia kwa namna moja au nyengine.

Leo tutafocus na mambo machache sana yenye umuhimu wa hali ya juu. Kutengeneza Kipato Dhabiti Kwenye Forex Trading. Inawezekana unasoma makala hii ukiwa umekata tamaa kabisa kwenye biashara hii na unafikiria pengine kuiacha, ila napenda kukupa imani kwamba uko katika nafasi nzuri sana ya kutengeneza kipato, pengine ukisoma nakala hii kwa umakini mkubwa sana unaweza kufanikiwa. Mwaka 2020 umekuwa mwaka mgumu sana haswa kwenye masoko ya kifedha, traders wengi wameshindwa kupata returns au faida walizotegemea kupata na wengine wamepata hasara. Walioanza career zao mwaka huu basi lazima wamekutana na mwamba huu. Lakini kwenye msafara wa mamba huwa kuna kenge, Yawezekana mfano huu usilete mantiki sana lakini nimeutumia kutofautisha tu kwamba kwenye kundi la watu wengi kuna wanojaribu lakini wapo wanaofeli na wapo wanofanikiwa.

Kutengeneza $1400 au zaidi ambazo ni sawa na millioni 3.6 za kitanzania ndani ya trade moja inawezekana kabisa, pamoja na mataifa makubwa tunayo trade fedha zao kuathirika kwa janga la corona bado movement za pair mbali mbali za forex zinatembea na una uwezo wa kuchota kiasi kikubwa sana. Kumbuka sio rahisi bali inawezekana. Nitakupa mfano mmoja wa trade niliyoanza kuifuatilia kutoka mwezi wa tano ambayo imeweza kuzaa zaidi ya dola $1400. Kazi yangu ilikuwa ni kusubiri tu baada ya kufanya execution.

Mfano wa hii trade #USDCAD. Ni trade ambayo ni swing. Naposema swing trade namaanisha trade iliyolala zadi ya siku moja na kuendelea.

Broker Ninaemtumia ni Tickmill FCA Regulated.

Sasa nimewezaje kupata trade kama hii kwenye masoko yasiyotemebea wakati wa huu wa pandemic? Jibu ni rahisi sana. Sio kila pair iko hivi ila ni baadhi na ni chache sana. Kazi yako ni kufanya research na unaweza kupata. Labda nikupe chache tu ambazo unaweza ukafocus nayo (GBP/JPY) ikiwa moja wapo ila nyengine ikawa ni siri yangu. Nitakuwa nimekuendekeza sana kama nitakupa zote, lazima ujifunze kufanya Research and Development (R&D) kama unataka kufanikiwa kwenye hii biashara.

Watu wengi wameacha kutrade kwasababu wameshindwa kutafuta pair nzuri za kutrade. Hakuna kitu kibaya kama kuacha kutrade kabisa yaani unakuta mtu amefunga chati zake anafanya mambo mengine. Skill ya trading ni kama hesabu yani kila siku walau lisaa limoja unacheck chati zako kufuatilia masoko.

Waswahili wanasema mtafutaji hatoki mikono mitupu lakini kwenye trading mtafutaji anaweza kuambulia mikono mitupu kama anatafuta kwenye hakuna. Hapo ndo kunapokuja umuhimu wa kujifunza jinsi ya kufanya research and development. Nafikiria kuja kuandika uzi wa research and development ndani ya forex trading lakini haitakuwa hivi karibuni. Hii ni siri kubwa ya mafanikio kwani inakusaidia pair zipi za kuepukana nazo na zipi za kukamia sana kwa wakati fulani.

Hata utumie strategy gani duniani, hautaweza kuwa right asilimia mia moja ila kupitia research and development unaweza kusogeza asilimia zako kufikia 80. ”Not Being In a Trade Is a Profitable Trade”. Maamuzi ni yako, unaweza ukawa sniper kama mimi kwa kujiamini na kufanya Research and Development au ukawa kama swala ambaye anaruka ruka huku na kule na kuishia kuliwa na chui. Sina maana mbaya kukupa huu mfano lakini kama umehangaika sana day trading bila mafanikio basi jaribu kubadilisha approach yako kwenye masoko.

Jambo la mwisho ambalo ningependa kukuacha nalo ni kupunguza risk na kuongeza reward zako maradufu. Wakati huu amabapo bado nchi nyingi hazijaweka sawa uchumi wao sio jambo la busara sana kuongeza risk amount yako, kimsingi unahitaji kupunguza kiasi ili uweze survive hiki kipindi. Asilimia kubwa ya traders hawawezi surivive crashes za namna hii na fursa zikitokea wanakuwa wameishiwa kabisa.

Unapo snipe trade kama hizi hakikisha unajizolea pips za kutosha. Kwa mfano trade kama hiyo hapo juu risk amount ilikuwa ni nusu ya asilimia moja ya mtaji wote. Kwa vyovyote vile hata ingekuwa hasara basi nisingeweza kuumia kwani ni kiasi kidogo sana ila faida yake imekuja maradufu.

Unatakiwa kuwa na calculated risk, maana najua motivational speakers wengi wanasema bila risk huwezi kufanikiwa lakini ukweli ni kwamba blind risk ndizo zinazo wakwamisha traders. Akishasikia risk your money to make more basi anajilipua bila kujua kwamba hili game ni survival, the more you see the more you learn the more you earn.

Take Away

  1. Tambua wakati sahihi wa kuingia sokoni, sio kila muda kuna fursa.
  2. Fanya swing trading kama day trading haikulipi.
  3. Jifunze kufanya Research and Development (R&D).
  4. Umuhimu wa kufanya Risk Management yaani take calculated risks na siyo blind risks.
  5. Survive, Hili game sio kwa wadokoaji you have to participate long enough to make money.
  6. Uwe positive na amini kwamba unaweza.

Weka comment yako chini una mpango gani wa kufanya mageuzi kwenye trading yako.

Sponsored Learn More

Connect with me on Piptwitz.com @ray_heriel, I share some tips and active trading there as well.

Subscribe
Notify of
guest
10 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
john
john
6 months ago

nice read thank you

KidoNation32
KidoNation32
6 months ago

Nimekuelewa bro Kwa mwangaza huu

meshack
meshack
6 months ago

brother nashkuru sana naamini naweza sana sijakata tamaa hata kama nimechoma sana.

Ramadhani
Ramadhani
6 months ago

Thanks sana bro, Got the task from your Top six 6 take away, especially R&D while waiting for a thread of R&D, I will start myself on, to make things easy. Others are just for improvement. But Thanks bro.

10
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x