!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Jinsi Ya Kupata Sniper Entries.

As usual every week napenda kushusha uzi mmoja ambao kwa namna moja au nyengine utaweza kumsaidia trader yeyote ambaye anapambana kufanikiwa kwenye biashara hii ya Forex. Kwenye pita pita huko mitandaoni nina imani umewahi kuona screenshot za trades ambazo ukitafakari entry zake basi unaweza usipate majibu kwamba imewezekanaje especially kwenye fast market ya namna hii mtu kuweza kuingia kwenye eneo lile. Hivyo basi, somo la leo litajikita moja kwa moja kwenye sniper entries, chukua note book yako na soma uzi huu kwa makini sana kwa sababu inawezekana ukawa mwanzo wa safari yako ya kupata sniper entries.

Ili niweze kueleweka kwa urahisi nitatumia strategy yangu moja ambayo ilinisaidia kukuza account yangu kutoka $100 – $13k.

Trend Line, Support & Resistance and Signal (TSS).

TSS ni strategy rahisi sana na inaweza wa kukuza account yako lakini kwa leo sitaongelea maswala ya kukuza account kwa sababu upo uzi maalum unaoongelea Namna unaweza kukuza Forex Account yako. Leo ni siku ya sniper entries.

Kama inavyojieleza kwenye jina TSS. Hii ni strategy inayofunika confluence tatu muhimu kupata entry, tunatumia trend line, support and resistance pamoja na signal. Hapa kwenye signal kuna variable nyingi kama pinbars, railroad tracks, Morning and Evening stars na nyengine nyingi lakini kwa sababu tunajifunza sniper entries basi tutafocus na pinbars kwa sababu ndiyo variable ya pekee inayoweza kukupa sniper entry makini.

Sniper Entries

Unaweza kutumia entry technique nyingi inategemea wewe uko comfortable kwa kiasi gani. Kama wewe unajali risk reward ratio basi sniper entry ni muhimu ili uweze kumaximize profit zako. Kulingana na hii strategy, ili uweze kupata sniper entries inabidi uwe na..

1. Confluence Chache Makini

First unatakiwa kuwa simple sana, usiwe wale traders wenye confluence kama 20 hivi kwenye strategy moja, utachanganyikiwa halafu utaanza kukashifu watu kumbe wewe ndo mwenye matatizo. Keep it simple, TSS is very easy and simple. Confluence tatu kazi umemaliza, sio rahisi kuzipata lakini inawezekana kabisa, ukishakuwa mzoefu yani umepractise vya kutosha basi utakuwa unaziona sana kwenye chart yako. Kumbuka, unahitaji a trending market, trendline alignment, support and resistance kwenye strong key areas pamoja na pinbar. Pinbar haijalishi rangi, unatakiwa ufocus kwenye shape yake, Wick ya pinbar inatakiwa iwe atleast twice as tall than the body. Kuna traders ambao ni tweakers wataenda kuongeza mambo mengine kama moving averege n.k, its up to you asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Stick within these parameters only.

2. Tumia Pending Orders For Execution

Kwa sababu tunategemea TSS zikutane kwa pamoja ili tuweze kupata entry watu wengi wangependelea kutumia market execution method lakini binafsi napata sniper entries nazipata nikitumia pending orders. Usiumie roho endapo pending order yako haijaguswa au market imechukua order yako then ikaenda moja kwa moja kwenye stoploss yako, hizi ni expenses zenyewe na huwezi ukazuia hata ufanye nini.

Ili kuongeza probabilty za ushindi huwa entry zetu zitakuwa kwenye touch ya tatu ya trendline kwa sababu tunaamini by that time trend itakuwa unfolded so we have to ride with the market south. Hiyo ndio sehemu ya kuweka pending order yako, stop loss weka few pips above the level. Kitakacho tokea ni kwamba, price ina probability kwa kugonga kill zone yetu ambayo ni TSS kisha kuchukua order yako then candle ile itanyonya na kufunga chini kwa sababu ya rejection ya support and resistance zone yetu. Utabakiwa na pinbar na utakuwa umeshaingia kwenye trade na uko profitable kwa haraka sana.

Kama ungeamua kutumia market execution ingekubidi usubiri mpaka candle ifunge chini kabisa ndipo uingie, nayo sio mbaya lakini haitokuwa sniper entry tena. Stoploss yako itakuwa kubwa sana na vile vile reward itashuka.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Nathan
Nathan
7 months ago

Mad respect brother. Nice read

mary
mary
7 months ago

Thank you, Ubarikiwe

Nwaka
Nwaka
7 months ago

Tisha sanaaa

Pages: 1 2

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x