!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Jinsi Ya Kukuza Account yako ndogo ($50, $100, $200).

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Suala la mtaji linaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi hasa traders wadogo, wengi wanakuja wakiwa na matumaini ya kupata mtaji wao wa kwanza huku, lakini mara nyingi imekuwa ndivyo sivyo.
Trading imekuwa kama sehemu ya kumchangia broker sasa maana asilimia kubwa ya traders wanapoteza pesa zao bila kujua nini cha kufanya.

Ukweli ni kwamba risk management kwenye Account ndogo hufanya traders wakate tamaa mapema sana hata kama ni cent Account na kuishia ku giveup mapema sana, wengi hufikia hatua ya kulaumu mentor wake. You have to be responsible kwenye trading yako, ukiwa mtu wa kulalamika basi mafanikio utayaskia kwa wengine.

Kama wewe hauna kipato cha kila mwezi basi ni dhahiri kwamba top up method ya kila mwezi itakushinda na the only option ni kuwa aggressive which is bad kwa asilimia 98% kama hujanoa skill yako kisawasawa. Utapoteza kila kitu, tena kwa haraka sana. Ila option ya pili inahitaji pia uwe high skilled trader kama mimi and my team with high accuracy kwenye execution zetu. Unahitaji patience ya hali ya juu kusubiria setups zenye probability kubwa then add a little more risk kwenye trade.

Hii haimanishi you will be right 100% kila siku lakini ukiwa na high skilled expertise, your odds of success ziko juu sana compared to low skilled trader. Trade za namna hii huwa zinapatikana kwenye higher timeframe na unaweza kuhold zaidi ya miezi miwili hadi mitatu sometimes hadi minne. Uzuri wa hizi trade zitakupa reward nzuri ya kukufanya usonge mbele. Hakuna haja ya kutrade kila siku kutafuta reward ndogo ndogo wakati unaweza ukatega mtego mmoja mzuri tu na ukavua papa.

Kwanini Nimesema High Timeframe?

Kule ndo kuna clear price movements zisizo na kelele. Lower timeframe kama h1 kushuka chini kuna kelele sana na hautaweza kusnipe high probability trades. Ukiweza kurudia hili mara kadhaa na ukafanikiwa basi utaweza kupata mtaji unaohitaji sokoni. Kumbuka njia hii ni hatari sana na kama hujawahi hata kuwa profitable usithubutu. Kama ni mgeni sahau kabisa maana ni njia ya haraka sana kuwa maskini.

Wapo waliofanya wakafanikiwa ikiwemo mimi lakini nakuhakikishia kwamba kama skill yako ni ya kitoto uko kwenye hatari ya kuzama baharini.

Live account kutoka $94 mpaka $813

Kila kitu tunachofanya kwenye maisha ni risk, hata kufungua biashara nayo ni risk, chochote kile hata kwenda kwenye majukumu ya kila siku ni risk tunachukua, hakuna anayejua nini kitatokea sekunde chache zijazo.

Hivyo basi ili kuepuka na emotional 😭 torture kama mambo hayajaenda sawa (which is normal) ni vyema ukawekeza kiasi ambacho uko tayari kupoteza. Tafuta mtaji mdogo wa $100 au $200 kisha tenga mafungu kadhaa kwa mfano mtu wa $100 anaweza kugawa mara 20 akawa anarisk $5 kila trade.

Ukipata trade 15 na ukakosa 5 hakika mtaji utakuwa nao baada ya muda na kwa vile utakuwa unatrade high timeframe ndani ya mwaka utakuwa umekamilisha zoezi. Mwaka ni mfupi sana maana sasa tuko August nusu. Next year August you will be somewhere else kama utakuwa na discpline.

Kama umekata tamaa kabisa unaweza kujiunga na our community of elite traders kuna experienced traders ambao wanaweza kukuongoza ukafanikiwa kwenye trading industry, hatupendelei watu wavivu wasiopenda kujituma, trading sio rahisi, inahitaji watu wenye uchu wa kujifunza na kufanyia kazi walichojifunza.

Nitaendela kukupa madini kila wiki na nia yangu nikisaidie ukae kwenye mstari ulionyooka.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
12 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Setisfx
Setisfx
10 months ago

Kaka umenipa elimu kubwa sana. Ntalifanyia kazi.

Goodnardo Elioth Jr
Goodnardo Elioth Jr
10 months ago

Love you brother

Kelvin Seme
Kelvin Seme
10 months ago

Umeniongezea kitu hapa bro…. thanks

Ramadhani
Ramadhani
10 months ago

Asante Sana kaka mkubwa, I appreciate sanaaa! Tiger

Musa Saguda
Musa Saguda
3 months ago

Nashukuru najifunza mengi sana kuhusu fx mmekujq wakati sahihi

12
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x