!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Jinsi ya Kudhibiti Matarajio yako kwenye Biashara ya Forex.

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Kama una miaka zaidi ya miwili au mitatu kwenye biashara ya forex trading unaweza kubaliana na mimi kwamba hakukuwa na uwiano kati ya uhalisia wa biashara na matarajio uliotegemea mwanzoni, yaani reality na expectation vilikuwa vitu viwili tofauti. Kwa asilimia zisizopungua 80, traders wapya huwa na matarijio makubwa sana wakati wanaanza hii biashara ya trading lakini miezi mitatu mpaka minne mbele uhalisia huingilia kati, Kwa kifupi ulichotegemea sio ulichokikuta.

Hii inatokana kwa sababu ya jinsi forex trading ilivyowekwa kwenye mitandao ya kijamii. Lifestyle imekuwa kipaumbele kuliko uhalisia wa biashara yenyewe. Sasa, katika hali ya kawaida trader mgeni anakuwa hyped kwamba mambo ya huku ni mtelezo na kwanini asiingie tu aanze trading huku akiwa namatarijo makubwa pengine kuzidi yule aliyemuona kwenye mitandao haswa instagram na facebook. Ukweli ni kwamba huwezi kuilaumu hii mitandao kwani haitakusaidia chochote ila unaweza kuweka ukuta kwenye mindset ili uweze kuziba uchafu wowote usio na manufaa kwako.

Sasa, Trader yeyote katika hali hii lazima anakuwa na matarajio makubwa na chochote atakachokipata chini ya yale matarijio yanapelekea trader kuvunjika moyo sana kufikia hatua ya kusema trading is a scam. Ila ukweli ni kwamba trading is not a scam, Unaweza ukawa umejiscam mwenyewe tayari kwa kutegemea matarijio makubwa kwenye biashara ambayo huna uelewa nayo kabisa. Forex trading ni biashara ambayo inahitaji intelligence ya hali ya juu haswa kwenye saikolojia kwani matatizo yote humu yanaanzia kwenye saikolojia ya trader mwenyewe. Unaweza kusoma uzi huu: WHAT IS THE MINDSET/PSYCHOLOGY OF SUCCESSFUL TRADERS?

Leo nitakueleza jinsi ya kudhibiti matarajio yako kwenye biashara ya forex trading

Elewa kwamba chochote kinaweza kutokea.

Kama ilivyo biashara nyingi uhakika wa kupata faida sio mara kwa mara yaani mazingira ya soko yanaweza kubadilika na ukashindwa kupata faida kama ulivyotarajia. Embu fikiria katika hali kama hii ambayo uko na matarajio makubwa sana? Unaweza ukakata tamaa. Usiwe na furaha sana unapopata faida na vile vile usiwe na majonzi sana unapopata hasara kwani you will never know which variable will make you profit. Anything can happen. Kwa mfano Kama unakumbuka mlipuko uliotokea lebanon, lebanese Pound ilishuka sana thamani na kama ulikuwa umenununa fedha hiyo dhidi ya dollar basi lazima ulipata hasara ambayo hukutarajia.

Risk Kiasi kidogo kiwezekanacho

Tukitumia mfano huo hapo juu wa lebanese Pound, Embu fikiria ungekuwa umerisk kila kitu kwenye account yako? Hakika ungekuwa umechoma account muda huu. Ni rahisi kusema nitarisk asilimia 1 ya account ila sio rahisi kwani tamaa huingia kati na kukufanya uweze kuongeza risk. Ndio nakubali kwamba More risk = More Profits ila usisahau kwamba More risk is also equal to More Losses. kwa hiyo wakati unafanya maamuzi ya kuongeza risk usisahau hilo. Ukiweza kurisk kiasi kidogo you have a total control with your psychology na hautaweza kupepesuka.

Anza na Mtaji Mdogo Huku Ukitopup Account kidogo kidogo

Ukiwa na mtaji mdogo kuanzia $100 ni vyema ukawa unafanya top up kila mwezi au vyovyote vile uwezavyo. Suala la mtaji limekuwa tatizo kwa watu wengi, hii hupelekea watu kuanza kuweka matarajio makubwa na account zao ndogo mapema hata kabla skill ya trading haijakuwa. Kuna uwezekano mkubwa sana account ndogo kukua kufikia level makini sana lakini siri ni kwamba topping up accounts itakufikisha hapo na ndani muda mfupi unaweza ukawa na account kubwa. Wakati hii account inakuwa kuna mambo mengi sana utajifunza yenye manufaa makubwa.

Vile vile itafanya trading yako iwe process, utaithamini account yako na utakuwa na estimate ya returns unazoweza pata kila mwezi. Ukicheza nje ya hapa kuna uwezekano mkubwa sana ukawa na matarajio makubwa kitu ambacho hakishauriwi.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Goodnardo Elioth Jr
Goodnardo Elioth Jr
10 months ago

I really enjoying reading the article I meet the one who talk my language

Ramadhani
Ramadhani
9 months ago

Thanks good lesson for me

4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x