!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Jinsi Ninavyopambana na Trading Emotions.

Nina imani umeshawahi kukutana na haya maneno somewhere kwenye hustle zako za trading “Psychology in Trading is Key to Success” Haya maneno yana ukweli kwa asilimia 100 kwa sababu ukishavuruga tu kwenye eneo hili basi hutoweza kuvuna hata senti moja sokoni.

Trading psychology inabeba asilimia ya 80 kwenye msingi wa mafanikio ya trading, Risk management inabeba asilimia 15 na trading strategy ndio asilimia 5 ya mafanikio yako. Unaweza kuona kwamba ukicheza na psychology basi lazima uangukie pua. Ukweli ni kwamba hata trading gurus unaowaona huko mtandaoni wanapambana na emotions kila siku lakini kwa sababu we are human beings and not robots. We make mistakes everyday either kwa kusahau au tamaa na mambo mengine mengi.

Bila kumumunya maneno hutoweza kufikia level ambayo trading robots zimefika ila nitakuambia kitu kimoja ambacho unaweza kufanya na kikakusaidia sana. Unaweza kupunguza mistake and error rate down to 1 or 2 %. Binafsi nimekuwa nikistrugle sana kupunguza mistakes kila siku na nimefika point ya kutofanya makosa hata ndani ya miezi 4 hadi 6 na kama hasara ikitokea, then it was just a bad trade. I followed my plan blindly but the results where the outcome of the market movement which I can not control.

Last week ilikuwa profitable lakini I made a mistake for the first time after four months of trading.

Utaweza kuona kwamba katika trade tatu nilizochukuwa, trade moja haikugonga Target Price, nilifunga manually. Hizi ni mistake ambazo zinatokea na kila siku lazima uweke jitihada ya kutofanya makosa haya.

Somo la leo nitakupa tips chache lakini ukiwa makini na kuweza kufuata basi utafanikiwa mapema sana. Siwezi kukuambia kwamba utakuwa kama robot lakini utakuwa kwenye level ambayo inatosha kabisa kutengeneza kipato.

Posted on piptwitz.com

Prepare Your Trading week.

Changamoto kubwa ambazo traders wanapitia ni kushindwa kujianadaa mapema na wiki ikifunguliwa basi trader anarusha trades huku na huku. Kwa style hii lazima hasara zitakuwa salamu ya kila siku. Binafsi kila siku ya jumapili huwa nafanya preparation ya wiki inayofuata. Hii hunisaidia nisitoke nje ya reli kati kati ya wiki. Kumbuka kila utokapo nje ya reli basi ni hasara kwa hiyo naweza kusema njia moja ya kupunguza hasara ni kutotoka nje ya reli kwanza. Focus na trading plan yako cheza humo humo ndani na ikitokea hamna fursa basi kaa mbali. Kumbuka Not being in a trade is also a profitable trade. Always protect your capital at all costs.

Record Every Action and Review the tape every day.

Kila ninapoanza a trading session huwa na record screen yangu ili niweze kureiview the tape kila siku jioni. Watu wengi hawafahamu lakini kila unaporeview tape utajifunza mengi sana na kujua makosa endapo utafanya na kufahamu wapi uweke mkazo. Ni rahisi sana kusahau miss ndogo ndogo ambazo bila tape huwezi kuona na kufanya urudie makosa yale katika siku za usoni.

Hapa naelewa wale ambao hawana computer kubwa si lazima sana kuwa na software unaweza kutumia hii chrome extension kurecord desktop yako. Screencastify

Vile vile tape hizi zitakusaidia kuona what really happened before the mistake, what triggered you to make the mistake and what was your reaction after the mistake. Hizi zote ni data muhimu sana ambazo traders wengi hawana na ndio maana failure rate ni kubwa.

Ongea Na Rafiki au Mtu wa karibu Kuhusu Changamoto Unazopitia

Kadiri unavyobeba mambo mazito ya kuchoma account ndivyo unavyozidi kujichimbia kaburi. Nafahamu watu wengi wanaotrade Forex ni Vijana wadogo wengi wao wakiwa chuo au wamemaliza. Kundi hili hupata pressure kubwa sana haswa pale wanapochoma account wakitafuta kutengeneza pesa. Kwanza kabisa ondoa shaka kuhusu kuchoma account kwa sababu ni kawaida kwa newbie kikubwa ni kujifunza haraka na kutorudia makosa.

Sasa, kuna traders ambao wanashindwa kushare hizi stress na kupelekea kuwa weak psychologically. Kwanza kabisa fahamu hili, unapokuwa psychologically weak lazima ufanya haya makosa:- Kujawa na tamaa, kulipiza kisasi na kutrade kuzidi viwango. Haya makosa hayana mwisho mwema lazima itaback-fire kwenye account yako.

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta trading partner au kuongea na rafiki yako angalau utoe stress ili uweze kumove on Note, Rafiki yako lazima awe ni trader kwa sababu mtu wa nje hawezi kukuelelwa hata kidogo.

Unaweza kujiunga na communites online zenye positivity pale ambapo unahisi kukata tamaa basi kuna watu wengi wanaweza kukusaidia kimawazo ili uweze kurudi kweny reli. Ukibaki mkiwa lazima utaquit kwasababu trading ina stress nyingi sana mwanzoni you need a team to rely on. Nakiri kabisa hata mimi nisingekuwa na team mwanzoni nisingekuwa hapa leo nilipo hivyo nakushauri usiwe solo trader, find a space of positive minds and learn together.

Usiangalie Faida Au Hasara Wakati Una Trade.

Unaweza kudhani ni masiara na ukachukulia poa lakini katika mambo ya msingi yatakayoweza kukusaidia kudeal na emotions kwenye trading ni kutokuangalia zile faida au hasara wakati una trade. Binafsi wakati naanza kujipambania nilikuwa na nafunga terminal yote na kubakisha chart, sikuwa napenda kuchungulia zile faida zikiwa zinafluctuate kwa sababu nilikuwa ninapata pressure na kufunga nikiona faida kidogo na kufreeze nikiona hasara na kuziacha ziwe kubwa.

Unaweza kubadilisha zile running profits kuwa pips kama umeshindwa kabisa kuvumilia atleast itakusaidia lakini kutokufungua terminal ni njia dhabiti kabisa kucontrol emotions kwenye trading. Ikifika jioni then unaweza kuona mlolongo mzima wa siku na kufanya maamuzi ukiwa na sharp mind. Ukiona unapata hamu ya kuchungulia faida basi jikaze sana, ukweli ni kwamba itakuwa ngumu sana mwanzoni kwa sababu ya curiosity lakini its for the best, in the long run itakusaidia.

Punguza Trading Size (Lot) Zako

Muda mwengine traders wanachukua risk kubwa sana kiasi kwamba wanashindwa kuhandle stress. Account ina dola 100 halafu trader anaweka lot ya 0.5 hadi 1 maana yake ni kwamba amekwenda full margin. Account ikichoma basi anaingia mfukoni kwa hasira kudeposit tena huku akirudia jambo lile lile. Fahamu kwamba unatakiwa kudeposit pesa ambayo uko tayari kuipoteza na si vinginevyo. Tofauti na hapo ni kujipa stress, binafsi kwenye account yangu huwa naweka mtaji ambao hata ukipotea (kitu ambacho kwangu ni impossible) huwa siwezi kuumia. Always make withdrawals to motivate yourself.

Mpaka hapo utakuwa umeweza kucontrol tatizo la emotions kwa asilimia 10 kazi yako ni kurudia haya kila siku hadi zifike asilimia 80 ndipo utaweza kuwa comfortable na hii biashara. Ukifanya mara moja na kuacha it will make no sense at all.

Concluding

Nikuache leo kwa kusema sio jambo jepesi kuwa perfect lakini namini kabisa ukiweka jitihada utakuwa bora kuliko yule asiye na jitihada.

Trading ni kama mnayvokwenda shule na mwalimu wa hesabu ana fundisha darasani, sio kila mwanfunzi atafaulu kwa daraja A lakini wale wenye jitihada ndio wanaofaulu. Hivyo ishi na huu mfano kila siku unapotrade usitegemee maajabu kwenye kipato chako kama huweki jitihada za kufanikiwa.

Natumaini umejifunza jambo la msingi sana leo na ni imani yangu kwamba utayafanyia kazi. Happy Weekend

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Joshua
Joshua
7 months ago

Shukran Boss kwa elimu hii.
God Bless y’all

Noah Chris
Noah Chris
7 months ago
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x