!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JINSI FOREX INAWEZA KUWA NJIA KUU YA KIPATOAkiba ya kutosha kuendesha maisha ya kila siku.

Hapa profxtigers tunasimamia ukweli na uwazi hivyo tunasema unapoanza Forex trading usitegemee kupata faida yakuendesha maisha ya kila siku huu ni uwekezaji unaweza ukapata hasara mwezi wa kwanza na wa pili kisha mwezi wa tatu ukapata faida ya asilimia 51%, hapa kwa wastani wa miezi mitatu hii umepata asilimia 17% kila mwezi. Sasa katika taswira hii kama ungetegemea kila mwezi upate faida ndipo uendeshe maisha lazima ungekwama na kujikuta ukilazimisha fursa zitokee sokoni, ukifanya hivi unakuwa unazidi kujitengenezea mazingira ya hasara zaidi.

Kwa ufupi usitegemee faida za forex kuendesha maisha yako ya kila siku bali jenga forex iwe sehemu yako ya kujipatia mapato kwa kipindi kirefu bila wewe kuhitaji izo faida kila siku na mwezi unaweza ukawa una toa faida mara moja kila baada ya miezi mitatu, sita au mwaka kabisa kutegemeana na hali ya soko na faida utakazo tengeneza lakini haiwezi ikawa kila siku au kila mwezi.

Mimi nilipofikia kwa sasa na tegemea forex trading kama pato langu kuu kwa njia hii kila trade huwa na risk $400 ili kutengeneza angalau $2000 mpaka $4000 kutegemeana na volatility ya soko kwa muda huo.

Trade hii ikiendelea kuwa sawa naweza kutengeza faida ya $2000 mpaka $4000 au kama sitakuwa sawa ntapata hasara ya $400. Lakini faida moja hai hakikishii faida mwisho wa mwezi au mwaka hivyo nitaendelea kutrade hivi baada ya miezi sita kwa wastani naweza kuwa na faida ya $40,000 mpaka 80,000. Hapa ndipo nita toa faida kiasi fulani kuendesha maisha ya miezi sita ijayo na kuacha kiasi kingine kikuze mtaji wangu.

HITIMISHO

Forex trading haitakufaa kama upo kwenye matatizo makubwa ya kifedha na unataka kuyatatua kwa haraka ni kheri uende ukatafute ajira. Forex trading ni uwekezaji utakao anza kuufanya leo, kutegemeana na ukubwa wa mtaji wako itakuwezesha uwe na uhuru wa kifedha baada ya miezi au miaka.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Pages: 1 2 3

0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x