!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JINSI FOREX INAWEZA KUWA NJIA KUU YA KIPATOMtaji wa kujitosheleza wakati wa vipindi vigumu.

Changamoto nyingine ambayo inafanya trading kutokuwa kipato kikuu ni kukosa mtaji wa kutosha, sito fumba fumba nitasema ukweli mtupu. Hakuna maajabu uko nje utakayoyafanya kwa kipindi kirefu bila mtaji wa kutosha katika trading. Trading ina vipindi virefu vya hasara kama ilivyo kwenye faida unaweza ukaanza leo trading ukajikuta unapata hasara tisa mfululizo je? utaendelea kuwa na mtaji wako!

Kwenye swala la mtaji hakuna kiasi kimoja kwa kila mtu, inategemeana na trader mwenyewe ana hitaji kuwa na kipato cha kiasi gani kwa mwezi au mwaka na pia anaweza kuvumilia drawdown kiasi gani. Kwa mtu ambaye huwezi vumilia risk kubwa chukuwa kiasi unachokitaka kwa mwezi kisha zidisha kwa 12 jibu litakalopatikana ndio mtaji wako. Mfano: kiasi ninachokihitaji kwa mwezi ni $500 basi chukua hii $500 kisha zidisha kwa 12 jibu litakuja $6000 huo ndio mtaji wako. Utakuwa unarisk asilimia 2% kila trade na kwa wastani utakuwa unapata asilimia 8.3% kila mwezi ambapo kwa mwaka ni asilimia 99.6%.

Kwa mtu anayeweza kuvumilia drawdown kubwa kwa kiasi chake chukua kiasi unachokitaka kuingiza kwa mwezi kisha zidisha kwa 6 jibu litakalopatikana ndio mtaji wako. Mfano: kiasi ninachohitaji kuingiza kwa mwezi ni $500 basi chukua hii $500 kisha zidisha kwa 6 jibu litakuja $3000 huo ndio mtaji wako. Utakuwa unarisk asilimia 3% kila trade na kwa wastani utakuwa unapata asilimia 17% kila mwezi ambapo kwa mwaka ni asilimia 204%.

Sishauri kurisk akaunti yako kwa zaidi ya asilimia 3% atakama una uwezo wa kuvumilia risk na drawdown kubwa kwa kuwa ni hatari pale hasara zikifuatana, unaweza ukijikuta akaunti ina ungua kabisa…..

Wengi wanasema sasa mimi sina mtaji kwa hiyo niachane na forex trading hapana anza hapo ulipo hata mbuyu ulianza kama mchicha. Kama una mtaji mdogo jifunze kutrade fanya jitihada usipoteze huo mtaji pigana utengeneze faida ndogo ndogo na uongeze mtaji wako mara kwa mara.

Kiasi cha mtaji

Ukiweza kuwa na mtaji wa $1000/ 2,300,000/= utakuwa una uwezo wa kutengeneza $170/391,000/= kwa mwezi. Mtaji wa $1000 ni pesa ambayo asilimia kubwa ya Watanzania wanaweza wakajibana kwa miezi kadhaa au mwaka wakawa nayo na kuweza kuanza nayo forex trading na hata kama huna $1000 unaweza ukaanza na $100 ukapata faida ya 17% kila mwezi ukajenga uzoefu na kukuza mtaji wako pole pole huku ukiendelee kuongezea mtaji kila mwezi.

Kwenye utafutaji anza ulipo usingoje sana, anza na $100 ikuze kwa faida jibane kutafuta mtaji wakuongezea kila mwezi. Ongezea $50 kwenye akaunti yako baada ya mwaka utakuwa na zaidi ya $2000 kimtaji. Mfano hapa chini kwenye compound interest calculator tunaanza trading na mtaji wa $100 (current principal) kila mwezi tunaongeza $50 kwenye akaunti apo zimeandikwa (annual addition) lakini tuzichukulie kama (monthly addition), tunapata faida ya asalimia 17% kila mwezi kwa miezi 12 apo imeandikwa (years to grow) lakini tuchukulie kama (months to grow).

Tunaona kwa mwendo huu baada ya mwaka unakuwa na $2299.20 tuseme hata kama miezi mingine ungeruka kuongeza $50 usingepungua mtaji wa $2000 baada ya mwaka.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Pages: 1 2 3

0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x