!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JINSI FOREX INAWEZA KUWA NJIA KUU YA KIPATO

Ni ndoto ya forex traders wote kufikia hatua hii katika trading lakini ukweli ni kwamba sio forex traders wote watafikia hatua hii bali tu wale wachache watakao weka jitihada sahihi na kutokata tamaa katika kipindi cha mwanzoni. Kipindi cha changamoto za kujifunza namna ya kuwa trader mzuri.

Naomba nieleweke ninapo sema Forex iwe njia kuu ya kipato sina maana kwamba forex iwe njia kubwa ya kipato kila siku au kila mwezi bali iwe njia kuu na kubwa ya kipato ndani ya kipindi kirefu cha miezi kadhaa au miaka.

Forex trading sio ajira ni uwekezaji na uwekezaji ukiwa unajitosheleza unaweza ukawa ndio sehemu kubwa ya kipato chako kuliko sehemu zingine zote.

Forex trading inaweza kabisa ikawa njia yako kuu ya kipato kama utakuwa na yafuatayo.

Uzoefu wa kupata faida ndogo ndogo kwa kipindi kirefu.

Namna ya kwanza ya kujiweka katika nafasi ya kufanya trading kuwa kipato kikuu ni kuacha kutafuta njia za mkato za kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi, ni rahisi sana kupata faida kwa muda mfupi wa wiki mpaka miezi. Wengi wamefanikiwa hili lakini je Faida hizi utaendelea kuzipata katika kipindi kirefu? Sasa hiki ndicho kinachowashinda traders wengi na ndicho kinachofanya trading iwe ngumu kuwa kipato chako kikuu na kikubwa kuliko vyote.

Kwa wachache walioweza kufanya trading kuwa kipato chao kikuu wameweza kutafuta njia za kupata faida kidogo kidogo na hasara kidogo kidogo ili mradi mwisho wa siku wanatengeneza faida kwa kipindi kirefu .

Mfano mimi kila ninapo trade huwezi kukuta nimepata faida inayozidi asilimia 20% ya akaunti yangu pia huwezi ukakuta nina hasara zaidi ya asilimia 3% katika wakati wowote ule wa trading.

Tunacho kifanya ni kuto kuwa na tamaa ya kupata faida kubwa leo au kesho na kutoweka akaunti yetu ya trading katika hatari ya hasara kubwa pale hasara zinapotokea.

Usijaribu kujenga ghorofa kwa siku moja kwani litaishia kudondoka tu. Ukiweza kupata hasara ndogo ndogo na faida ndogo ndogo na ukamaliza miezi au mwaka na faida sasa unaweza ukafanya trading kuwa kipato chako kikuu endapo utakuwa na mtaji wa kutosha.

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Pages: 1 2 3

0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x