!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Je? inawezekana kuanza na mtaji wa laki 2 ($100) ukawa billionea ($ 1 milllion dollar) kwenye Trading!Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Hili ni swali ambalo traders wengi hututumia katika chat box zetu. Na niwazi kwamba mtu anae uliza swali hili ni mtu ambae hanapesa nyingi za kuanzia katika biashara ya trading.

Usijione wa ajabu, unapo anza trading na  mtaji mdogo  kwasababu kundi kubwa la traders huanza na mitaji midogo.

Katika kulichanganua swali hili tuanze kwa kuelewa trading ni nini?

Biashara ya trading ni biashara ya kubashiri muelekeo wa masoko ya kifedha, ya weza kua forex, hisa n.k . kwakizungu tunaita speculation.

Tunaposema ubashiri ni kitu ambacho hakina uhakika wa Asilimia zote, matokeo yaliopita huwezi kuyatumia kuhalalisha matokeo yajayo.

Wapo watu walio tajirika na trading wakianza na mtaji mdogo na wapo wengi pia waliofeli na kupoteza mitaji yao. Sasa kwanini wengi hufeli na wachache kufanikiwa?

Asilimia kubwa ya traders wanafanya trading kama biashara yakila siku. naomba nikwambia hicho kitu futa huwezi kubashiri soko kila siku ukawa sawa. Traders wanaofanikiwa hufanya uchambuzi wa soko na kutafuta hali flani za soko na kutrade hali iyo tu ikiwa haipo wanapotea na kuendelea na shughuli zao nyingine mpka watakapo ona hali hiyo ndo huja sokoni tena kutrade. Ila kundi kubwa la traders hujaribu kubashiri kila siku kwenye masoko tofauti tofauti huishia kupata faida na kuzipoteza zote kesho yake mwishowe hukata tamaa kabisa.

Ni vyema unapo hamasika na mafanikio ya trader flani mkubwa aliyeanza na mtaji mdogo akafanikiwa usiige tu alichofanya, kwanza angalia alikua anatrade soko gani na hali ya soko husika ilivyokua kipindi hicho ndipo uchukue mbinu yake na kuiga lasiivyo ukichukua mbinu tu bila kuzingatia hali ya soko lakipindi hicho ukilinganisha na sasa. Ni sawa na kuchukua ndoana ya kumvua samaki kibua ukajaribu kumvua nyangumi.

Turudi kwenye swala letu Je? inawezekana kuanza na mtaji wa dolla 100 ukatajirika na trading. Ndio inawezekana na hali flani ya soko na kwa risk toreleance flani

Kwenye hali yamasoko yanayo trend kuelekea upande mmoja kwa nguvu ni rahisi sana kwa traders kutengeneza faida kuliko masoko ambayo yana consolidate(soko ambalo haliendi juu wala chini linacheza kwenye bei zile zile)

Mfano wa soko linalo trend

Hapa trader ananunua Gold kwa kutumia technical event driven strategies.

Pichani juu, tunaona bull run ya Gold, trader angeanza na $100 aka scale in jinsi faida zinapo ongezeka baada ya miaka 8 angekua ametengeneza Faida  ya dolla za kimarekani million 10.953 sawa na faida ya Billion 25.4 za kitanzania. Kwa kupatia kubashiri muelekeo wa  trade moja tu na kuiongeza kila mara bei ikirudi kwenye eneo la mvutano wa soko kuelekea juu (DIP BUYING).

Hali yakimasoko kama hii haijaanza leo na sio mwisho bado unafursa yakuweza kufanikiwa na hali kama hizi zikijitokeza. Tuangalia baadhi ya traders walioweza kukuza mitaji kwa Trend following.

1970’s  –  1980’s  Richard Dennis  Commodity/Forex Trader

$ 400 – $200,000,0000

na vile vile miaka 1990’s mpka 2000’s kwenye technological  bubble crash traders kama vile Takashi Kotegawa (aka BNF / J-Com man) stock trader.

$13,000 – $ 153,000,000

Hivyo tumegundua kutajirika kwenye Trading na mtaji mdogo inawezekana lakini sio kwenye kila soko na sio kila siku,kila mwezi wa kila mwaka. Hali ya kimasoko kama hii ipo event driven, kwa ustadi wa makini kuyatabirika inawezeka inahitajika kuwa sawa mara moja tu.

Usikate tamaa hata ukianguka mara 99 unahitaji kuwa sawa mara moja tu.

Kujifunza namna ya kutengeneza event driven strategy na kutabiri hali kama hizi bonyeza hapa.

Mafanikio kwenye trading ni juhudi zako binafsi utawashiwa taa uone mbele lakini ni jukumu lako kutafuta njia ya kufika.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
11 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
setisfx
setisfx
5 months ago

noma sana bro

Ramadhani
Ramadhani
5 months ago

I always Appreciate bro, its a good article for traders. I think two things; knowlegde first plus experience with a lot more market conditions in head, experience comes with time and dedication. uongo kaka

Last edited 5 months ago by Ramadhani
Michael Chogo
Michael Chogo
5 months ago

Nimekuelewa sana mkuu. Thanks

meshack
meshack
5 months ago

haya ni madini kama ya laizer..

meshack
meshack
5 months ago

Nimesoma site nzima had imeisha naombeni muwe munatoa article kama hizi angalau mara tatu kwa wiki. zinatusaidia sana kupata motivation. Ni rahisi kukata tamaa. Please

11
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x