!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JE FOREX NI UTAPELI?Forex Prop Firms Feki

Prop Firm Trading ni profession ambayo imekuwepo kwa muda mrefu, Ki halali muundo wa biashara hii upo hivi, kampuni inakuwa na mtaji na kisha huajiri traders kutrade ule mtaji. Hawa traders watafundishwa namna yakuwa portfolio managers/ traders wazuri na baadae kukabidhiwa kiasi flani cha mtaji kukitrade. Hulipwa mshahara kama waajiriwa na wakitengeneza faida hupewa kiasi kisichozidi 2% ya faida kama bonus. Prop firm huwa zinamilikiwa na Ma bank au tasisi kubwa za kifedha zenye mtaji binafsi kwa ajili ya uwekezaji.

Lakini sasa kumekuwa na wimbi jipya la prop firm feki wana jitanganza hivi “NJOO TUKUPE MTAJI, TRADE PATA FAIDA TUGAWANE” hizi kampuni ni chui aliyejivisha ngozi ya kondoo, wamegundua traders wengi hawana mitaji hivyo hutangaza kwamba watakupa $25,000 mpaka $1,000,000 kama mtaji wako kisha mtagawana faida nusu kwa nusu na wengine wameenda mbali wanatangaza utapewa asilimia 70 na wao watabaki na asilimia 30 ya faida.

Sasa hapa ndipo wana kupiga pesa yaani kujiunga tu unatakiwa ulipie kiingilio cha $500 mpaka $1000 kutegemeana na ukubwa wa account unayotaka na kisha utapata account kubwa na elimu ya trading. Kweli ukimaliza masomo utapewa account kubwa.

Sasa, tuseme ulilipia $1000 kupata account ya $100,000 kweli utapewa hiyo account lakini hutoweza kutoa hizo pesa isipokuwa kiasi cha asilimia flani ya faida mlicho kubaliana. Ujanja upo hapa, wanakupa minimum management balance ambayo ukifikia basi mkataba na wewe umekwisha

Kwa mfano, kwenye account ya $100,000 watakuambia minimum management ni $99,600 yani ukipata hasara account isifikie hapo. Hapa wanalinda faida yao ya $400 kule kwenye $1000 uliowapa na wanajua asilimia 90% ya traders watakaojiunga wanafeli na kuifikia hiyo minimum balance kwa hasara.

Na wale watakao fuzu basi hutumia mtaji mdogo sana usiozidi $400 yani ni kwamba umetangaziwa $100,000 ukalipia $1000 lakini ukweli umepewa $400, ufupi umenunua baiskeli kwa bei ya gari.

Prop firm wana tumia njia ya panya kukuuzia trading course zao bila wewe kufahamu. Hakuna kitu kibaya kununua trading course lakini nunua ukifahamu unalipia course na sio kudanganywa kwamba utapewa mtaji mkubwa.

Kama ukijiunga na hizi prop firm fahamu kabisa unauziwa trading course na hakikisha kampuni inayokuuzia hiyo course ndiyo unahisi itakuwa na msaada kwako. Kwenye trading kamwe usiingie kwenye mtego wao ukiamini utapewa mtaji baadae.

Hitimisho

Forex trading ni biashara nzuri sana kwangu ni kipato namba moja cha kuendesha maisha yangu haijanichukua miezi kufika hatua hii bali ilikua safari ndefu lakini nashukuru kuifahamu hii fursa na kuifanyia kazi. Jifunze Forex vizuri ifanye mwenyewe usitegemee mtu mwingine hakuna ataekaye kulinda kuingia kwenye mikono ya hawa matapeli zaidi ya wewe mwenyewe na huu uzi niliyotumia kufukua mbinu zote ovu zinazotumika. Hata ukitegemea mamlaka za kisheria itakua ni jambo la baadae sana na la gharama kubwa, hivyo jilinde wewe mwenyewe kwanza. Usisahau kuwatumia wenzako unaowapenda uzi huu ili uwaepushe na changamoto kama hizi.

Kama umejifunza tafadhali comment chini hapa hadi wakati mwengine.

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Chogo
Michael Chogo
4 months ago

Somo kubwa sana kaka, itoshe tu kusema ASANTE

Ismail
Ismail
4 months ago

Asante kaka Kwa kutufumbua macho, kiukweli ubarikiwe sana, Na sintochoka kujifunza kutoka kwako Moki..

Uromi
Uromi
4 months ago

Kimsingi, ningepata namna ya kuwasiliana na ww ingependeza. Kama hutojali_naomba unitafte kwa hii email (ambroseuromi@yahoo.com)
Hongera kwa somo zuri hili

Pages: 1 2 3 4 5 6

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x