
JE FOREX NI UTAPELI?
Forex Money Managers feki
Forex Money Management ni profession kubwa sana duniani na yenye heshima yake, hapa naongelea Forex Funds, hedge funds n.k. Hizi taasisi zina leseni kutoka kwa mamlaka husika za kusimamia washiriki wa masoko ya kifedha kwenye nchi husika. Hapa Tanzania kuna CMSA (Capital Markets And Securities Authority) na kwa upande wa kenya wana CMA (Capital markets Authority of kenya).
Lakini kuna matapeli mitaani huanzisha upatu feki wakitumia jina la forex trading, wana ahidi kwamba watakupa asilimia 50 mpaka hata 100 kwa mwezi ili tu uchanganyikiwe kuona ni faida kubwa na ya haraka, ukisha wapa pesa yako sema kwa heri. Wanachofanya ukiwapa pesa yako wataitumia pesa ile kulipa wawekezaji wa zamani kisha kuwatumia wale wawekezaji walio lipwa na pesa yako kama ushuhuda wa kudaka wawekezaji wapya ambapo wakipatikana wawekezaji wapya pesa yao hutumika kukulipa wewe basi mchezo huu utaendelea mpaka siku itakapotokea hakuna watu wapya wakujiunga na money management scheme hiyo. Hapa sasa wamiliki wa huo upatu wanakimbia na kuondoka na pesa zenu.
Kama huna muda wa kutrade na unataka kuwekeza kwenye Forex money management fund fanya uchunguzi kama wana leseni kutoka mamlaka husika za masoko ya mitaji, kisha angalia track record yao jiridhishe kama ndio aina ya uwekezaji unataka kufanya kisha wekeza. Kamwe usitoe pesa yako mtandaoni kwa mtu anayedai yeye ana manage forex accounts ni tapeli.
Somo kubwa sana kaka, itoshe tu kusema ASANTE
Asante kaka Kwa kutufumbua macho, kiukweli ubarikiwe sana, Na sintochoka kujifunza kutoka kwako Moki..
Kimsingi, ningepata namna ya kuwasiliana na ww ingependeza. Kama hutojali_naomba unitafte kwa hii email (ambroseuromi@yahoo.com)
Hongera kwa somo zuri hili