!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JE FOREX NI UTAPELI?Wauzaji wa signals au trade alerts

Hizi huwa ni notification ambazo trader mzoefu anatoa kwa traders wengine (subscribers) kwa gharama ya mwezi au wiki. Hizi huwataarifu muda muafaka wa kununua na kuuza pair fulani ili wajipatie faida. Hapa kinachofanyika ni kwamba hawa subscribers hupata faida kupitia ubobezi wa kichambuzi wa trader anayetoa hiyo huduma.

Wapo traders wabobezi wa soko ambao kweli wanatengeneza faida sokoni na ukifuata signals zao kwa ufasaha utaweza kutengeneza faida lakini changamoto inakuja pale ambapo hufahamu strategy ya trader huyo iko vipi na mpo kwenye draw-down, inakuwa ngumu kuamini kufuata kitu usichokijua kwa ufasaha.

Vile vile wapo matapeli ambao wao hutafuta pesa za viingilio kwenye magroup yao ya trading kwa njia za kijanja yani anakuwa na magroup mawili, group la kwanza anawaambia BUY group la pili anawaambia SELL kwa wakati mmoja na baadae group moja kati ya yale mawili litapata faida kisha tapeli yule hutumia group lile lililopata faida kama ushuhuda wakujipatia wateja wapya mitandaoni.

Sishauri mtu afanye subscribtions za signals kabisa, jifunze kutrade mwenyewe, fanya maamuzi yako binafsi. Kama uko busy na huna muda wakufanya analysis sokoni cha kufanya ni tafuta Forex Money Manager mwenye leseni ya kufanya shughuli hizo. Leseni itoke mamlaka ya kiserikali inayohusika na kuwakagua hawa money managers kama wame timiza vigezo vya kufanya shughuli hizi na hapa ndipo utapeli mwingine unazaliwa.

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Chogo
Michael Chogo
4 months ago

Somo kubwa sana kaka, itoshe tu kusema ASANTE

Ismail
Ismail
4 months ago

Asante kaka Kwa kutufumbua macho, kiukweli ubarikiwe sana, Na sintochoka kujifunza kutoka kwako Moki..

Uromi
Uromi
4 months ago

Kimsingi, ningepata namna ya kuwasiliana na ww ingependeza. Kama hutojali_naomba unitafte kwa hii email (ambroseuromi@yahoo.com)
Hongera kwa somo zuri hili

Pages: 1 2 3 4 5 6

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x