!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JE FOREX NI UTAPELI?



Forex trader feki na waalimu wanaotolewa na Forex brokers wanaodai wametajirika haraka na Forex trading.

Forex traders feki! hawa ni wajanja sana hukodisha magari ya kifahari wakidai ni ya kwao na wamenunua cash na kuonesha maisha ya kifahari kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na facebook kisha huandaa semina na kudanganya wahudhuriaji kwamba wametajirika kirahisi ndani ya miezi kadhaa na forex trading na kushawishi wa hudhuriaji kulipia kiingilio au kufungua akaunti za forex trading kwa broker flani ambae kasajiliwa kwenye nchi zenye usimamizi (regulation) mbovu. Vile vile wanadai kwamba ukisha lipia kiingilio au kufungua akaunti utapewa mbinu itakayokutajirisha haraka kama walivyotajirika wao wanadai watakupa mbinu za kukupa pesa haraka kumbe ni mbinu za kipuuzi zitakazo hakikisha unapoteza pesa zako zote kwa haraka sana na baadae trader feki hugawana pesa na broker.

Pia kuna Semina zinazoandaliwa na Forex brokers ambazo mara nyingi ni upuuzi mtupu usio na msaada wowote zaidi ya kukufanya ufungue akauti kwa broker husika. Ni brokers wachache sana ambao pia ni traders wazuri wengi hutegemea commission kutoka kwetu sisi traders ili kuendesha biashara zao na maisha yao.

Cha kufanya, jifunze Forex trading vizuri usifuate maisha ya kifahari yanayo oneshwa na traders feki. Hizo hutumika kama chambo za kukudaka ujiunge. Tafuta trader mzoefu atakae kuonesha pande zote mbili za forex trading hasara na faida jiridhishe kama kweli trader anayekuongoza anatengeneza faida na forex trading na sio tu kwa kuuza kozi na semina, lazima awe mtendaji wa anacho kizungumza.

Broker sio mtu mzuri kukuongoza katika trading hata akikudanganya kwamba anafanya trading yeye mwenyewe hua ni njia tu za kukufanya ufungue akaunti kwake na uanze trading ili apate commission kila unapo trade. Mtumie broker kama taasisi itakayo unganisha trade zako na soko kuu lakini sio kama mwalimu au kiongozi wako wa trading.

Forex trading sio njia ya kujitajirisha haraka na sio njia rahisi lakini ukifanya vizuri na kufuata sheria zote za mafanikio ni biashara itakayo kupatia uhuru wa kifedha kwa kipindi kirefu. Siwezi kukuambia Forex itakutajirisha kwa sababu sifahamu unaanza na mtaji kiasi gani mimi nimekuwa trader kwa miaka takribani mitano sasa na nimeweza kukuza mtaji wangu kutoka $510 mpka $88,341 kwa miaka minne. Haikuwa safari nyepesi wala ya mstari ulio nyoka, ilikuwa safari ngumu ya mabonde na milima. Na ukweli ni kwamba hata hapa nilipo fika siwezi kusema nimetajirika kwani $88,341 sio pesa ya kuishi maisha ya kitajiri kama inavyo oneshwa na hawa traders feki, ni fedha inayonipa uhuru wa kifedha kwa namna moja au nyingine. Mwaka wa kwanza hapa sijaongelea kwa maana huo mwaka nilikuwa napoteza pesa tu mwaka wa pili nao chali hadi mwaka wa tano ndipo nilipoweza kukuza mtaji wangu.

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Chogo
Michael Chogo
4 months ago

Somo kubwa sana kaka, itoshe tu kusema ASANTE

Ismail
Ismail
4 months ago

Asante kaka Kwa kutufumbua macho, kiukweli ubarikiwe sana, Na sintochoka kujifunza kutoka kwako Moki..

Uromi
Uromi
4 months ago

Kimsingi, ningepata namna ya kuwasiliana na ww ingependeza. Kama hutojali_naomba unitafte kwa hii email (ambroseuromi@yahoo.com)
Hongera kwa somo zuri hili

Pages: 1 2 3 4 5 6

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x