!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

JE FOREX NI UTAPELI?Forex brokers wenye leseni za biashara kutoka kwenye nchi zenye mamlaka na usimamizi mbovu.

Kwa kuwa hakuna forex broker mwenye leseni kutoka mamlaka yeyote ya usimamizi nchini, Forex traders hutafuta brokers nje ya nchi ili kuweza kutrade Forex. Hapa ndipo kuna changamoto za kufahamu utumie broker gani ambako pesa zako zitakuwa na usalama. Soma uzi huu: JINSI YA KUMKAGUA ONLINE FOREX BROKER utakupa maelezo ya kina jinsi ya kumkagua broker vizuri. Nchi kama marekani na uingereza mamlaka za usimamizi wa Forex brokers zina umakini na nguvu kubwa ya kusimamia taasisi za Forex trading.

Matapeli wengi wa Forex hupenda kufungua taasisi zao kwenye nchi kama Saint Vincent and the Grenadines, Belize na Cyprus nchi ambazo mamlaka zao ni legevu kwenye ufuatiliaji.

Nchini Kenya kuna Capital Markets Authority of Kenya (CMA). South Africa kuna the Financial Sector Conduct Authority (FSCA)  ambazo zina usimamzi kwa kiasi chake vile vile zipo karibu na nchini kwetu.

Kitu cha kwanza kabisa unapo tafuta Forex broker angalia yuko regulated nchi gani? Mimi nikiwa natafuta Forex broker huwa siulizi mara mbili ni aidha marekani chini ya Commodities Futures Trade Commission (CFTC) au National Futures Association (NFA) na uingereza chini ya  Financial Conduct Authority (FCA) huku nina amani na usalama wa pesa zangu.

Usiwe na imani na broker alichokiandika kwenye tovuti yake au atakacho sema endapo atakupigia simu. Fanya ukaguzi kwenye tovuti ya mamlaka anayodai inamsamimia ili kuhakikisha kama kweli yupo regulated.

Waogope kama ukoma Forex brokers ambao wamesajiliwa kwenye regulation mbovu kama nilizo ainisha hapo juu, Mara zote brokers hawa huwa ni market makers hasara zako ni faida yao ipo michezo mingi sana inayofanywa kwa traders ili wapoteze pesa zao.

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Chogo
Michael Chogo
4 months ago

Somo kubwa sana kaka, itoshe tu kusema ASANTE

Ismail
Ismail
4 months ago

Asante kaka Kwa kutufumbua macho, kiukweli ubarikiwe sana, Na sintochoka kujifunza kutoka kwako Moki..

Uromi
Uromi
4 months ago

Kimsingi, ningepata namna ya kuwasiliana na ww ingependeza. Kama hutojali_naomba unitafte kwa hii email (ambroseuromi@yahoo.com)
Hongera kwa somo zuri hili

Pages: 1 2 3 4 5 6

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x