!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Hizi Ni Sababu Zinazokufanya Usifikie Malengo yako Kwenye Trading.

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo.

Kila mwaka mpya unapoanza watu wengi sana huandika malengo yao ya kutimiza mwaka huo mpya wazungu wanaita New Year Resolutions Nikuambie tu kwamba katika plan zinazoongoza kuvunjwa ni hizi za mwaka mpya yaani new year resolution. Kundi kubwa la vijana huweka plan zao lakini wiki moja baadae wameshindwa kuyafanyia kazi malengo hayo, kwa sababu Talk is Cheap yaani kuongea ni rahisi sana kuliko kufanya action.

Wakati naanza trading kitambo kidogo nyuma kuna mwaka niliweka plans zangu lakini nikajikuta wiki mbili baadae nimerudia ujinga wangu wa mwaka uliopita. Hii inatokana na mazoea mabaya na hakuna kitu kitamu kama bad habits, kwanza ukianza kuzitoa ili uweze kuweka good habits mwili wenyewe pamoja na akili unakataa ndio maana ni ngumu mno. Sasa kama huna discpline na patience huwezi ukafanikiwa katika jambo lolote.

Hii iko vile vile kwenye Forex Trading, What you do in real life will reflect kwenye trading yako. Kama umeshindwa kufikia malengo yako kwenye maisha ya kawaida usitegemee maajabu kwenye trading. Unaweza ukabaki hapo hapo maisha yako yote na ukakosa wa kumlaumu. Leo nitakupa sababu chache sana amabazo zinakufanya usifikie malengo yako kwenye trading na vile vile unaweza kutumia sababu hizo hizo kwenye maisha ya kawaida.

Huna hata hiyo plan yenyewe.

Plan ni muhimu sana kwani ndipo unapoanzia. Kama huna hata hiyo plan my friend bado uko gizani sana, hauna tofauti na treni iliyokosa kichwa au ndege isiyo na engine. Hivyo basi weka plan kwenye trading yako, kama huna strategy tafuta, wekeza nguvu kuijua plan hiyo usiku na mchana, usiwe yule trader ambaye akiamka leo anatumia trendline, kesho anatumia support na resistance kesho kutwa yupo na Elliott wave au wyckoff strategy. Tafuta moja kati ya hizo ambayo utaiamini na kufanyia kazi ndipo usogee mbele. Vile vile ni vyema ukaweka malengo ya kifedha yenye uhalisia, huwa nasikitika sana kuona trader anaanza na dola 100 halafu anataka awe na 6 figure ndani ya miezi mitatu, lazima utafeli hii plan kwani haina uhalisia wowote.

Ifikirie plan yako muda wote, tafuta njia ya jinsi utaifanya iwe better kila siku.

Usiwe ile type ya watu ambao plan zao huzitupia kabatini au kwenye diary. La hasha ili kitu kiwe bora lazima kiwe na innovation, ukiwa unafikiria jambo kila muda lazima upate njia ya kuliboresha. Hivyo ukianza kusoma strategy kwa mtu flani usibaki nalo tu hivyo ifikirie kila muda tafuta njia ya kuiongezea mambo yako mwenyewe ili iendane na wewe. Jambo la muhimu ni kwamba usimodify mpaka ukatoka nje ya basics. Hii itakupa motivation ya kuendelea kutimiza malengo yako na kufanya uipende process nzima.

Haufanyi Ufuatiliaji.

Follow up ni jambo la msingi kwani hutegeneza sense of responsibility yaani uwajibikaji. Mtu anayefanya mazoezi ya kupunguza uzito lazima awe anapima kilo kila baada ya wiki ili kuona progress na kama akiona kilo hazishuki basi anajua kuna kitu hakiko sawa na kurekebisha. Hivyo hivyo hata trader akiwa hafanyi follow up ya trade zake na system yake hakuna namna anaweza kujua kama amepiga hatua mbele au nyuma. Hata malengo yako uliyoweka kwenye jambo lolote hayawezi kutimia bila kuwa una ufuatiliaji wa karibu.

Chochote kizuri maishani, ukiona trader anapiga faida, au ameenda vacation ni matunda ya kuweka malengo na kuwa discpline kuyafanyia kazi ikiwemo na ufuatiliaji. Hivyo basi hata wewe unaweza ukafanikiwa sana kama ukiweza kuwa na nidhamu na kuwajibika.

You can be a successful trader too. Trading is a marathon and not a sprint, lazima uwekeze muda na pesa kuyapata hayo mafanikio unayotaka.

Nitaendela kukupa madini kila wiki na nia yangu nikisaidie ukae kwenye mstari ulionyooka.

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
setisfx
setisfx
9 months ago

Thanks alot brother

Joshua
Joshua
9 months ago

Ahsante Chief

Josh Julius
Josh Julius
8 months ago

Thanks for the article brother

5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x