!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Forex Trading Sessions Tanzania.

Trading Sessions In Tanzania.

 • London/European Session: 9:00 Am – 7:00 Pm
 • New York Session: 3:00 Pm – 12:00 Midnight
 • Tokyo/Asian Session: 1:00 Am – 8:00 Am

Bila shaka utakuwa unahangaika kufahamu nini maana ya trading session. Trading session ni nyakati tofauti tofauti ambapo masoko ya kifedha duniani yanakuwa yamechangamka, yani shughuli za uuzaji na ununuzi wa fedha zinafanyika kwa wingi. Kama tunavyo fahamu soko la forex huwa wazi masaa 24 kwa siku 5 za wiki duniani kote lakini kila nchi hutofautiana muda na hapo ndipo tunapopata hizi session.

Kwa nini London, Newyork na Tokyo?

Majina haya yametokana kwa sababu sehemu hizi tatu ndizo zinazo ongoza kwa volume. London session ndiyo inayoongoza kwa volume duniani hivyo hufanya session hii kuwa na liquidity kubwa ikufuatiwa na Newyork na mwisho kabisa Tokyo session. Kwenye haya maeneo matatu kuna traders wengi sana wanatrade pamoja na shughuli nyingi sana za ubadilishwaji wa fedha na takwimu za uchumi na siasa huripotiwa kila siku.

Session ipi ni bora?

London session ndiyo session bora zaidi kutrade kwa sababu nilizo sema hapo juu.

 1. Asilimia kubwa ya forex volume inachangiwa na London session (30%).
 2. Pair nyingi kubwa zinahusisha pair za ulaya kwa mfano GBP/USD, EUR/USD, EUR/CHF, GBP/CHF na nyingine nyingi.
 3. Kuna liquidity kubwa sana kwenye London session.
 4. London ina financial institutions kubwa duniani hivyo kuifanya ipatiwe jina la the Forex Capital of the world.
 5. Kama unaishi Tanzania basi London session huangukia muda muafaka sana wa saa tatu asubuhi hadi saa moja jioni hivyo una siku nzima ya kufanya trading.

Hii ndiyo session bora zaidi kufanya shughuli za trading.

New York Session ndiyo inayofuata kwa ukubwa wa volume duniani, hii haina tofauti sana na london lakini volume na volatility hazilingani sana na London session. Changamoto ni muda tu kwa sababu ukiwa Tanzania New York session huanza saa tisa jioni hadi saa sita usiku na kwa watu wengi wanakuwa wamechoka na hawawezi kufocus. Lakini kwa trader mwenye nia ya kufanikiwa basi muda huu huwezi kuwa kikwazo sana.

Asian Session

Hii hutoweza kutrade ukiwa Tanzania labda kama ni mtu wa kukesha usiku au uamke usiku. Session hii huanza saa sita siku na kuisha saa mbili asubuhi mara nyingi huwa hakuna volume na pair ambazo hutembea sana kwenye hii session ni NZD/USD na AUD/USD. New Zealand na Australia zote hupata na movement sana kwenye asian session.

Session Overlap

Session overlap hutokea pale ambapo session mbili zipo wazi kwa wakati mmoja kwa mfano kuanzia saa tisa jioni New York inapofunguliwa hukutana na London session ambayo ilikuwepo wazi toka saa tatu asubuhi. Overlap hii hubakia kwa masaa kadhaa hadi saa moja usiku London inapofungwa na kuiacha New York peke yake hadi saa sita usiku.

Huu muda ni mzuri sana wa kufanya trading kwa sababu masoko mawili makubwa duniani yako wazi kwa wakati mmoja. Hii hufanya kuwe na volume kubwa sana sokoni na unaweza kushuhudia pair kama EURUSD ikitembea kwa kasi sana. Vile vile Economic data za marekani hutolewa kwenye mida hii kiasi cha kufanya soko liwe na volatility sana, binafsi napendela kutrade muda huu.

Daylight Savings (DST)

Huu ni utamaduni wa kusogeza saa mbele kipindi cha kiangazi (Summer) ili mchana uwe mrefu. Sehemu duniani ambazo zinafanya tamaduni hizi husogeza saa zao mbele kwa saa moja na baada ya msimu wa kiangazi kuisha wanarudisha saa zao nyuma kwa saa moja.

Utamaduni huu huathiri muda wa session za London, New York pamoja na Tokyo kusogea mbele kwa saa moja. Vile vile utaona kwenye MT4 yako kwamba candle za h4 huchelewa kufunga kwa saa moja mbele.

Session time during daylight saving

 • London/European Session: 10:00 Am – 8:00 Pm
 • New York Session: 4:00 Pm – 1:00 Midnight
 • Tokyo/Asian Session: 2:00 Am – 10:00 Am

Kama umeona hapo session time zote zimesogea mbele kwa saa moja ili kufanya utamaduni huu wa day light savings. Yote haya ni kwa sababu wakati wa kiangazi mchana huwa mrefu na usiku huwa mfupi.

Lini hutokea?

Hii hutokea kipindi cha kiangazi lakini kila broker huwa ana utaratibu wa kufahamisha wateja wake kwa mfumo wa email ikiwa na tarehe husika mabadiliko hayo yatatokea.

Hii email ilitumwa mwaka jana kwa clients wote hivyo hata mwaka huu lazima tutegemee kupata tena zikifika tarehe zifuatazo:-

 • London 27th October 2020
 • New York 3rd November 2020
 • Asia 5th April 2020

Natumaini utakuwa umejifunza jambo la msingi sana kwenye somo hili. Kama hujaelewa unaweza kuuliza kwenye comment hapo chini na tutakusaidia kujibu haraka iwezekanavyo.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Constantine kalangi
Constantine kalangi
8 months ago

Ni pair zipi ambazo kwa anaejifunza anaeza ku trade katika new York session ni pair zipi zinafaa, katika Tokyo session, na ktika London sessesion

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x