!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Forex Trading: Mtego Ulionasa asimilia 90 ya Traders.

Ni miezi minne sasa imepita toka nimeandika uzi wangu wa mwisho. Kama hukusoma unaweza kufuatilia hapa kwani niliandika mambo ya msingi ambayo nisingependa yakupite UNAHITAJI MUDA KIASI GANI KUWA PROFITABLE?

Sasa, uzi wa leo unaweza ukaibua hisia tofauti lakini imenibidi niandikie ili nikutoe kwenye gray area na kukuweka sawa katika safari yako ya trading.

Sababu kubwa kwa nini zaidi ya asilimia tisini ya traders wanachoma pesa zao ni kudakwa na mtego huu wa fikra ambao ndio kihunzi kigumu kuliko chote kwenye biashara hii?

Ngoja nikuambie kitu kimoja, Lengo lako la kwanza unalotakiwa kuweka unapoanza trading ni

Kuwa na uwezo wa kumanage risk kwenye trading plan Madhubuti.

Ukiweza kufanya hivyo basi haitakuwia vigumu kutengeneza pesa. Statement rahisi sana, sio? Lakini hapo ndipo panapoumana na traders wengi. Ukimkuta trader yeyote ana trade forex jaribu kumuuliza what is your risk plan? Au strategy yako ni ipi? Kwa asilimia kubwa hawana majibu na hata akijitahidi vipi basi atakuwa na kimoja tu. Hawezi kuwa na vyote kwa Pamoja.

Trader wa namna hii anakuwa na frequency patterns kama ifuatavyo.

  1. Mtaji mdogo sana na anataka kufanikiwa na mtaji huo huo mdogo, option aliyonayo ni kucheza kamari kwa sababu hawezi kufanya risk management.
  2. Telegram channel yake imejaa magroup mengi ya signal, moyoni akiwa na Imani kwamba kuna signal moja itatolewa na itamfanya atimize ndoto zake.
  3. Hajawahi kutulia na plan moja hata kwa wiki moja.
  4. Ameshasoma course za mentors wote ila bado Forex imekataa.

Trader kama huyu haitaji tena elimu ya technical trading, huyu anahitaji mental guidance kwa sababu trading is a mental game. Ukiendelea kuhangaika kutafuta technical solutions utaishia kuwa failure miaka yako yote.

Technical solutions kwa mfano trading strategies etc, zote zinachangia asilimia 30 tu ya mafanikio yako ya trading, kibaya zaidi naona traders wanapoteza muda wao miaka nenda rudi wakihangaika na technical solutions wakati ni asimilia 30 tu. Stop Wasting time on non-productive agendas.

Kipengele muhimu zaidi cha safari yako ya trading ni kile kinachokusaidia kuelewa juu yako mwenyewe.

Usipojitambua, hauna nafasi ya kufanikiwa na trading, Iko hivi ngoja nikupe tip. Kwenye trading psychology kila binadamu ana triggure zake. Kila mtu anafahamu wapi yuko weak kwenye trading na wapi yuko strong. Ila cha ajabu unakuta trader ana miaka hadi mitatu haelewi pressure point zake, yuko triggured na kila kitu anachoona mbele yake hata kama outcome yake ni mbovu kiasi gani.

Binafsi nilikuwa sipendi kupata hasara na ikitokea nimeweka trade imegonga stoploss basi automatically ubongo wangu unaingia kwenye revenge mode, guess what? Scenario inakuwa kama unapigana na bondia mwenye nguvu zaidi yako. Unampiga ngumi yenye kilo tano yeye anarudisha yenye kilo kumi tano. Ukirudia mara tatu au nne basi unakuwa umeshapigwa KO.

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Big Lot Fx
Big Lot Fx
2 months ago

Kaka hizi nondo ni balaa sana nakushkuru na ubarikiwe

Innocent Meriolika
Innocent Meriolika
2 months ago

Fuck, I was wasting my time all these years. This is revolutionary

Joshua
Joshua
2 months ago

itoshe kusema kwamba umetuokoa sana na hii thread.Mungu akubariki sana my brother.

ScareFx_dealers
ScareFx_dealers
2 months ago

Duuuuu asee Asante Sana Kaka,huu Uzi umejaa ukweli na uwazii ubarikiwe mnoo

Last edited 2 months ago by ScareFx_dealers

Pages: 1 2 3 4

8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x