!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Fixed Risk Amount Vs Risk Percent. Moja Kati ya hivi itakumaliza sana.

Somo la leo moja kwa moja litajikita kwenye jinsi ya kupima trading profits zako. Nina amini wengi mmeshasikia moja kati ya haya maneno. Risk Amount na Risk Percent, kwa wale wadau wa risk management wataelewa fika ni nini ninazungumzia hapa lakini kwa wewe unaekutana na concept hii leo embu tuangalie maana zake kwanza.

Fixed Risk Amount

Hiki ni kiwango cha risk kwenye mfumo wa pesa halisi kila unapotrade mara nyingi huwa ni fixed amount. Kwa mfano mtu mwenye mtaji wa dola $100 na kila trade anaweka risk ya $5 maana yake ni kwamba anatumia risk amount ya $5 kama risk yake. Ikitokea kwamba amepoteza ile trade atapoteza dola $5. Sasa kwenye mtaji wa dola $100 ana fursa 20 tu hivyo akikosea mfululizo mara 20 tu basi account imeshapotea.

Risk Percent

Hiki ni kiwango cha risk kwenye mfumo wa asilimia. Kila muda trader anapohitaji kutrade basi hufanya exposure wa mtaji wake kwa kutumia asilimia anazotaka au kuwa comfortable nazo. Kwa mfano trader mwenye mtaji wa dola 100 anaweka 5 percent risk itamlazimu kurisk dola 5 kama 5% yake. Lakini trade inayofuata haitokuwa 5% ya dola 100 bali itakuwa 5% ya dola 95 hivyo kiwango cha kurisk kitashuka kadiri mtaji unavyoshuka.

Option Yangu ni Risk Percent (%)

Kama mnavyofahamu mimi ni swing trader kwa muda mrefu sana na katika mambo ya msingi swing trader anahitaji kuzingatia ni survival how long can you handle draw downs before getting a chance to make a profit?

Hapa ndio suala la risk amount na risk percent linaingia kati. Kwa upande wangu napendelea kutumia risk percent na ninakupa sababu. Risk amount itakumaliza sana wakati wa draw downs.

Mwaka huu kwa mfano, ni mwaka mbovu sana interms of trading kwa sababu ya covid-19 kwenye nchi kubwa ulaya. Hii imepelekea strategy nyingi sana kushindwa kuhandle drawdown na ukweli ni kwamba sio trading strategy bali ni risk management strategy za watu wengi zimeshindwa kuvumilia mtikisiko na kufanya watu wengi wapate draw-down au kuchoma kabisa account zao, Kutumia Risk Amount ikiwa ni moja wapo ya sababu.

Advantage Ya Risk Percent over Risk Amount

Inapunguza spidi ya kupata draw-down kubwa

Ukiwa unatumia risk percent, kiasi cha pesa unachorisk kinashuka kadiri mtaji wako unavyopungua hivyo inakupa nafasi nzuri sana ya kusalimika kipindi cha draw-down. Kwa mfano niliyotoa hapo juu wakati naanza kuandika uzi huu nilisema imagine mtu ana mtaji wa $100 na ana risk 5% kila trade, Trade ya kwanza ikapata mzinga maana yake atabaki na dola 95 kwa hiyo ikitokea fursa nyingine sokoni atapiga hesabu ya kurisk 5% ya 95% ambayo ni dola 4.7, so trade ikipata hasara atapoteza dola 4.7 na sio dola 5 kamili. Unaweza kuona ni difference ya kiwango kidogo lakini kadiri unavyoshuka basi kiwango cha kurisk kitashuka. 5 percent ya dola 100 ni tofauti na 5% ya dola 90,80 au hamsini.

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Goodnardo Elioth Jr
Goodnardo Elioth Jr
8 months ago

Got you Brother

Baraka
Baraka
8 months ago

Imekaa poa kaka nmekuelewa

Michael Chogo
Michael Chogo
8 months ago

Somo zuri kaka, asante

Pages: 1 2

5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x