!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Fahamu Muundo Mzima Wa Soko La Forex.

Kanusho: Hali ya kiuchumi/kifedha ya msomaji haijazingatiwa, kilichoandikwa kwenye nakala hii kamwe isichukuliwe kama ushauri wa uwekezaji au fursa ya uwekezaji bali itumike kama elimu tu na matokeo yaliopita hayakuhakikishii matokeo yajayo

Nina imani utakuwa umesoma uzi wangu wa mara mwisho wa FOREX TRADING NI NINI na umejifunza mengi sana. Leo nitakuletea muendelezo wake na kukuelezea kwa undani zaidi muundo mzima wa soko hili. Dhumuni langu ni uwe na uelewa mpana kabla hujafanya maamuzi ya kutrade forex. Soko la forex ni soko kubwa sana duniani, Kuna mzunguko wa kiasi cha dola trillioni 6 kwa siku na huu ni mujumuiko wa shughuli zote za kiuchumi kuanzia wasafiri, makampuni mbali mbali na transaction za kibenki. Karibu kila kitu kinachohusisha ubadilishaji wa fedha basi huchangia kwa kiasi chake.

Lakini cha kushangaza sisi retail traders tunachangia kiasi kidogo sana kwenye mzunguko huu kwa sababu mbali mbali ikiwemo mitaji midogo. Institutional traders kwenye taasisi mbali mbali kama hedge funds, Investment banks ndio wenye ushawishi mkubwa sana kiasi cha kuwa na uwezo wa kushawishi price movements. Unaweza pia kusoma uzi wangu wa HOW TO TRADE LIKE BANKS. THEY CONTROL 92% OF THE VOLUME na kuona ni jinsi gani taasisi hizi zina ushawishi mkubwa sana juu ya retail trader.

Wahusika wakuu (Forex Market Participants).

Kabla ya kuanza trading inabidi ufahamu unakwenda kuwekeza muda na pesa zako kwenye kitu gani na unakwenda kupambana na nani? Soko la forex ni la ushindani na kuna makundi yafuatayo:-

1. Liquidity Providers (LP)

Hili ndilo kundi la kwanza la wahusika, hujumuisha mabenki makubwa, makampuni na serekali kubwa mbali mbali hapa duniani. Ninaweza kusema kwamba ukiwaondoa hawa kwenye hii chain basi biashara ya forex itaathirika sana kwani hawa wana control volume kwa kiasi kikubwa zaidi ya asilimia 90%. Interbank liquidity hufanya soko kuwa na movement kwani ni kiasi kikubwa sana cha mabilioni ya pesa kinahitajika kutembeza pip au point chache tu. Sasa kwa akili ya kawaida unadhani retail traders wana uwezo huo?

Retail traders tunawahitaji sana liquidity providers kwa sababu tunaweza kutengeneza faida pale tu soko linapotembea either kwenda juu au chini na hawa jamaa wanachangia movement ya soko kwa kiasi kikubwa sana.

2. Forex Brokers (Madalali)

Dalali ni mtu wa kati na utaniuliza je huyu ana faida gani? Huwezi kudeal na interbank kama huna mtaji mkubwa hivyo hawa madalali wana mitaji mikubwa sana na wanadeal na hizi taasisi na wanaunganisha order zetu baada ya kutupatia price or data feed kutoka kwa LP. Dalali anachofanya ni kuongeza markup spreads kwenye kila order kama faida yake. Ukiweka order ya Buy au Sell broker hakupi bei halisi ya soko ila anachofanya anaongeza spread pale. Spread ni tofauti kati ya buying au selling price. Kwa mfano Bei ya EURUSD ni 1.5 ili dalali aweza kupata faida dalali anaongeza pip moja au mbili so utanunua EURUSD kwa 1.7 faida yake hapo ni 0.2.

Unaweza kuona ni kiasi kidogo lakini madalali wana order nyingi sana kiasi cha kuwafanya kuwa wakubwa wengine kufikia hatua ya kuwa market makers yani wana uwezo wa kutengeneza soko internally bila ku route order kwa LP.

Broker anachofanya ni kukusaidia wewe kuwa na access ya soko, vile vile anakupa leverage kama una mtaji mdogo. Vilevile dalali hutoa platform ambazo retail traders wanatumia kufanya trading activites bure bila malipo platform hii ambayo hupatikana kwa mfumo wa software huitwa (metatrader 4). Madalali wako wengi sana na siyo wote ni waaminifu hivyo kuwa makini unapochagua dalali wa kufanya nae kazi, Soma uzi huu muhimu sana: JINSI YA KUMKAGUA ONLINE FOREX BROKER.

3. Retail Traders

Hili ni kundi la mwisho. Retail trader ni yule anayenunua na kuuza kwa rejareja. Yani mimi na wewe au mtu yeyote anayetrade binafsi. Ukiwa kwenye hili kundi inakubidi uwe na weledi na hekima ya hali ya juu unapofanya maamuzi yako kwenye trading. Kundi hili hupata taarifa (economic news) wa mwisho na ni ngumu kutengeneza pesa kama huna edge.

Ukiwa retail trader unahitaji skill kutengeneza pesa. Skill of trading hujengwa kwa muda mrefu na huitaji watu wavumilivu, usidhani unaweza kuwa a pro trader ndani ya muda mfupi wa kuanza trading kwani unahitaji kuwekeza muda wako na pesa kwenye kujifunza ndipo utaweza kufanikiwa.

Nakumubuka wakati naanza kutrade forex miaka ya nyuma nilingia kwenye mkumbo huo wa kutrade forex bila kujua kwa undani hii ni biashara gani na ilipelekea kupata hasara sana hivyo unaweza kusave pesa zako kama utafuata ushauri huu. Unaweza kusoma nyuzi huzi kupata uelewa mpana zaidi.

FOREX TRADING TANZANIA, YAFAHAMU HAYA KABLA YA KUJIINGIZA KWENYE HII BIASHARA.

FOREX TRADING NI NINI?

Kujifunza zaidi skill ya trading unaweza kujiunga na elite community yetu na kupata nafasi ya kusoma kwa udani zaidi biashara hii ya Online Forex Trading.

Endelea kusoma kwenye tovuti yetu kuna masomo mengi sana ambayo yatakusaidia wakati huu unapoanza trading kama career yako. Kama una maswali weka comment yako chini.

Sponsored Learn More

Ni follow kwenye Mtandao wa Piptwitz.com Kama @ray_heriel, Huwa na share tips mbali mbali kuhusu trading kila siku.

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Saidy amani
Saidy amani
9 months ago

naomba kufahamu mnapatikana wapi na unajiunga vipi?

2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x