!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Dalili 4 Zinazoashiria Kufeli Forex.

Sponsored Content

3. Kamari (Gambling)

Wakati naanza trading kuna trader mmoja aliwahi kunitamkia haya maneno “Ngoja nicheze forex leo nipate hela ya Msosi”. Ukitafakari kwa kina haya maneno trading imeonekana kama sehemu ya kuingia na kutoka chap chap ndio maana watu wengi wanashindwa kupata mafanikio wanayoyataka. Forex ukichukulia kama kamari nayo itabehave kama kamari, kibaya zaidi forex haina deposit limit yaani unaweza kujikuta unadeposit na kupoteza miaka nenda rudi kwa sababu umeichukulia kama kamari. Brokers wanatoa kitu kinaitwa leverage, hii leverage itakumaliza haraka sana usipokuwa kuwa makini kwa sababu it’s addictive.

Unachotakiwa ni kuifanya biashara hii kama a REAL BUSINESS yani faida na hasara, entries na exits, capital management vyote vinatakuwa kuwa handled professionally. Ukiweza kufanya hivi na ukaacha tabia hii mapema basi unaweza kuepukana kufeli. Kwenye hili sina maneno mengi sana kwani nimeshaandika sana kwenye site hii.

4. Kutokuwa na records na Ufuatiliaji.

Tokea siku ya kwanza wakati unaanza kujifunza Forex trading basi ni lazima uwe na tabia ya kuweka records ya kila unachokifanya na kufanya ufuatiliaji. Ni rahisi kuweka records lakini changamoto inakuja pale ambapo utahitaji kufanya ufuatiliaji na kufanya urekebishaji wa makosa ambayo yanajitokeza. Ukipuuzia kufanya hivi mwanzoni basi inakuwa tabia sugu ambayo huwa ni ngumu sana kuja kuibadilisha. Trader unatakiwa kuwa na personal trading journal au diary ambayo utakuwa unaijaza kila siku ukiandika mambo ya msingi.

Journal hii au diary itakusaidia sana kuweka mambo yako sawa. Kwa mfano hii hapo chini ni digital journal ambayo nimedevelop personally kwa ajili ya kurecord trade zangu au chochote kile kinachohusiana na trading, Ina msaada sana kwangu kwa sababu record hazifutiki na siwezi kupoteza data yeyote. Wote tunafahamu ni jinsi gani notebook zinavyojaa au kupotea mara kwa mara. Hivyo nakushauri uanze mapema tabia hii ya kuweka record za trade zako.

Personal Journal

Summary

Sio kila trader atafanikiwa lakini idadi kubwa ya traders wanafeli kwa kujitakia wenyewe yaani wanafahamu kabisa nini cha kufanya lakini kwa sababu ya kupuuza basi huwa ndio mwisho wao. Hizi dalili nilizozitaja hapa juu ni wazi kwamba karibu kila trader amewahi kuziona lakini kwa sababu ambazo nyingi ni uzembe basi wameshindwa kufanyia kazi na kupelekea kufeli katika biashara hii. Trader unayesoma uzi huu jaribu kubadilika mapema kabla mvua haijanyesha epuka stress kwa kuweka jitihada binafsi kwenye trading development. Tukutane Ijuma ijayo kwa somo pevu lengine.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
13 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Anesius
Anesius
9 days ago

Yes

Max
Max
18 days ago

Bro signal tamu sana sema daah ni kweli najikuta nakua kilaza kadiri siku zinavyoenda.

Shaaban
Shaaban
18 days ago

Kweli kabisa

Don
Don
18 days ago

ray sorry iv ulisoma ifm ?

Maselekk
Maselekk
14 days ago

Ujumbe makini Sana huu

Mr.tarq
Mr.tarq
10 days ago

Jaman mm jisaidien ndio kwanza nimpya sielew jinsi ya kufanya hii biashara tafadhalini

Pages: 1 2

13
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x