!BREAKING: Profxtigers Launches Piptwitz™ - A Professional Forex Community Built For Traders.

Dalili 4 Zinazoashiria Kufeli Forex.

Kupuuzia dalili mara nyingi imekuwa chanzo cha kupatikana kwa matatizo makubwa zaidi katika siku za usoni. Kwa mfano, mtu anapopuuzia uvimbe katika sehemu fulani ya mwili wake kwa muda mrefu bila kwenda hospitali. Mtu huyu anaweza kuwa na cancer na muda wote ambao amekuwa akipuuzia uvimbe kumbe ndio ulikuwa wakati wake wa kuokoa maisha yake, mpaka anafika hatua ya kukubali kwenda hospitali basi ugonjwa unakuwa umekithiri sana kiasi cha kushindwa kupona kabisa.

Huu ni mfano hai kabisa hata kwenye biashara ya Forex, Traders wengi wamekuwa wakipuuzia dalili ambazo zinaashiria kufeli katika siku za mbeleni. Kuna traders wameshindwa kabisa kufanikisha ndoto zao kwa sababu ya kupuuzia dalili hizi. Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na uzi huu wa leo tunakwenda kuangazia mawingu ambayo yana uwezo mkubwa sana wa kukufelisha kwenye hii biashara ya Forex.

Ninasema yana uwezo mkubwa sana ya kukufelisha kwa sababu bila kuweka nguvu na jitihada binafsi kufanyia kazi mawingu haya basi kuna uwezekano wa kufeli kwa asilimia 100%. Sio kwamba haiwezekani kufanikiwa lakini unahitaji nguvu kubwa ya kujituma na sio tu mara moja bali ni kila siku unapoketi kwenye chati zako na kutrade.

1. Unategemea Signals Kutengeneza Pesa.

Wauza signal watanicrush sana lakini ndio ukweli, Unapomuuzia trader mgeni signal humuandai kuwa independent trader, unazidi kumfanya adumae kiakili na uwezo wake wa kufikiri hasa pale kwenye kuchambua chart unashuka sana. Ukiwa new trader nafahamu unakuwa kwenye ile hali ya kutaka kupiga pesa fasta lakini kumbuka haraka haraka haina baraka. Ukishasubscribe kwenye signal za provider yeyote ile basi huo ndio mwanzo wa kutafuta nani ndiye best provider ambaye signal zake hazikosei. Focus yote inahama kutoka kwenye kujifunza na kuzama kwenye rally ya kutafuta holy grail signal kitu ambacho hutokipata maisha yako yote. Vilevile umeshawahi kujiuliza huyu provider akiacha kutoa signals hali itakuaje? Je hii ina maana kwamba na wewe utaacha kutengeneza pesa? Ukweli ni kwamba new traders hawafahamu hili ndio maana failure rate ni kubwa sana. Kama umesubscribe kwenye signal provision yeyote ni wakati wako wa kupunguza kuzitegemea kwa sababu mbele ya safari hazina faida yeyote labda kama huna mpango wa kujifunza kitu ambacho sio kweli. Kila trader ana ndoto za kuwa the best ila ni uvivu wa kusoma na tamaa all at once ndizo humfanya trader anatafuta easy solution kama signals.

2. Kudeposit Mtaji Ambao Ni Mkopo (Loan).

Mtaji wa kutrade Forex umekuwa ni changamoto sana kwa traders wengi hivyo inapelekea kukopa pesa ili kufanya trading ili warudishe pesa hizo baada ya kupata faida. Kwanza kabisa kwa trader mgeni this is a failed mission kwa sababu rule number one ya trading ni “Deposit Funds That You Are Ready To Lose” Unapokopa pesa kwa ajili ya trading automatically unakuwa chini ya pressure nzito na akili yako haiwezi kufunction vizuri especially kwenye bad trading conditions. Mpaka hapo umevunja rule ya kwanza, hauko tayari kupoteza hiyo pesa. Wote tunafahamu nini kinatokea endapo unatrade na pressure na pesa ya mtu. Outcome yake ni kufanya makosa ya kijinga, kuwa na hasira ya kurevenge hasara pamoja na ku-overrisk. Ewe new trader unayesoma huu uzi epuka kukopa pesa kwa ajili ya trading, anza na mtaji wako mdogo kwa sababu through the learning process utapata uzoefu wa hali ya juu na kukuongezea odds zako za mafanikio. Nimeona watu wengi na marafiki wakifeli kabisa kwa sababu ya kukopa pesa kwa ajili ya trading. Ukiona una dalili ya kuomba mkopo acha kabisa, futa akilini deposit pesa yako binafsi. Epuka madeni. Madeni yanarudisha nyuma jitihada zako.

Sponsored Learn More

Subscribe
Notify of
guest
13 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Anesius
Anesius
6 months ago

Yes

Max
Max
7 months ago

Bro signal tamu sana sema daah ni kweli najikuta nakua kilaza kadiri siku zinavyoenda.

Shaaban
Shaaban
7 months ago

Kweli kabisa

Don
Don
7 months ago

ray sorry iv ulisoma ifm ?

Maselekk
Maselekk
7 months ago

Ujumbe makini Sana huu

Mr.tarq
Mr.tarq
7 months ago

Jaman mm jisaidien ndio kwanza nimpya sielew jinsi ya kufanya hii biashara tafadhalini

Pages: 1 2

13
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x