FOREX TRADING TANZANIA, YAFAHAMU HAYA KABLA YA KUJIINGIZA KWENYE HII BIASHARA.NEW 

4.5 4 votes
Article Rating

Habari,

Ndugu waTanzania Mimi nikiwa kama mdau na miongoni Mwa Wa Tanzania wachache Walio wahi kuanza na kuyaona Mafanikio ya hii sekta mpya hapa nchini ya Forex trading, leo hii nimeona kuna ulazima wa kuandika Makala hii kumsaidia Mtazania yoyote uko nje atakae au anaye tamani kujiingiza kwenye hii biashara. Waweza jiuliza kwa nini nachukua jukumu hili, mafanikio katika sekta hii sio rahisi kama inavyo onekana kwenye mitandao na vyombo vya habari. Safari yangu ya mafanikio haikua rahisi, ilikua ni safari ya milima na mabonde, yaliopelekea matizo chungu nzima ambayo haina maana ya kuyaweka hapa, zaidi ya ambacho nataka ukifahamu.

Hivyo basi nimeona nifanye hivi kama njia moja wapo yakurudisha au kutoa kwa jamii bure kabisa kumsaidia yule anaeanza au ambae yupo safarini kuelekea mafanikio kwenye hii biashara, ili kuepukana na matatizo makubwa niliyo yapitia na kumsaidia kuyaona mafanikio kwa urahisi Zaidi.

Kama ningekua na mashine ya kurudisha muda nyuma, niwe mimi yule mgeni wa forex trading miaka mitatu  iliyopita, ningefanya hivyo ili tuu niwe na haya ninayo yafahamu leo kwa hakika ingenirahisisha  nakuongeza spidi ya mafanikio yangu na ningeyapata kwa haraka Zaidi. Lakini kibaya ni kwamba hakuna mashine kama hiyo lakini kwa wewe unaenza sasa hii nikama lulu kwako hivyo basi hivi ndo vitu vitano ambavyo ningevijua mwanzoni naamini  kwa asilimia mia moja ningefanikiwa mapema Zaidi.

NIVYEMA KUZINGATIA USIMAMIZI MZURI WA MTAJI KULIKO JAMBO LOLOTE LINGINE.

Tunapoanza Biashara ya trading, tena haswa trading forex wengi huja na ndoto mbali mbali na taswira binafsi yakujitajirisha haraka. Lakini  uhalisia ni kwamba njia pekee yakujitajirisha ni kuwa makini na jinsi unavyo risk pesa zako sokoni kwenye kila trade unayochukua.. Mfano, unaanza na mtaji wa $1000 sitegemei kukuona unarisk kwenye trade yoyote zaidi ya 2% ya mtaji wako ambayo ni $20. Kwa ambao wataanza na mtaji chini ya $300 ningeshauri kufungua cent account ilikukuwezesha kufanya usimamizi wa mtaji wako vizuri. Ukizingatia upande wa hasara  basi upande wa faida kamwe hautokua na shida. kwenye kila trade unayochukua hakikisha unapata faida ya zaidi ya kile kiasi ambacho hua una risk kwa lugha ya kitaalam tunasema RISK TO REWARD. Maanake yake faida zako ziwe Mara mbili na zaidia ya kiasi chako cha risk. kujifunza namna ya kusimamia mtaji wako vizuri bonyeza hapa 

NIRAHISI KU OVERTRADE KULIKO UNAVYO FIKIRIA.

Kitu ambacho niligundua baada ya kuwa mzoefu kwenye biashara hii siku za mwanzoni nilikua na overtrade na hata siku gundua na fanya hilo.

Nirahisi kutafuta visingizio vya trades unazochukua kwa wingi (kwaku overtrade). Lakini jibu kamili nikwamba je ime timiza vigezo vyako vya kutrade yaani (strategy)

Overtading nikitendo cha kuchukua trade nje ya strategy yako na niamini mimi, sio jambo gumu sana kufanya kwenye hii biashara, haswa kwa Traders wageni na nijambo ambalo lina umiza sana na kurudisha nyuma hatua zako zakimafanikio. Kujifunza zaidi namna ya kuepukana na overtrading bonyeza hapa

MATUMIZI YA TIMEFRAME NDOGO NI HATARI

Ukiangalia kwa makini hizi points zote zinaingiliana kwa mfano overtrading inasababishwa nakuangalia timeframe ndogo kama zile chini ya ‘1HOUR’,  laiti kama ningerudi nyuma kipindi nikiwa mgeni na forex ningejieleza haswaa  umuhimu wa matumizi ya timeframe za juu. Matumizi ya timeframe za chini yatakupelekea kuovertrade kwa sababu utahisi unaona fursa nyingi sokoni wakati kiukweli izo ni kele tu za soko. Kirahisi ni kwamba fursa zinazo patika timeframe za juu zina Asimilia kubwaa Zaidi ya kukutengenezea faida kuliko zile zinazo patikana timeframe za chini.

HUWEZI KUZUIA HASARA KABISA.

Inafurahisha sana unakuta traders wengi wanahangaika kuzuia hasara wakati ni jambo ambalo haliwezekani kuzuia hasara kabisa bali unaweza tu kuzipunguza kwa kufuata “system” yako.

Kama unafanya mambo kama haya:  trading bila stoploss, kusogeza stoploss kwenda breakeven mapema sana, kuchukua faida ndogo ndogo kulinganisha na hasara zako yaani kwa kifupi ni unajaribu kuepusha hasara na hicho nikitu kibaya rafiki yangu.

ZINGATIA KWENYE KUJIFUNZA NASIO KUTENGENEZA FAIDA UNAPOANZA TRADING.

Najua wengi wanao ni follow kwenye mitandao yakijamii watachukizwa nahili jambo lakini ni ukweli mtupu. Huwezi kufanikiwa na trading kama unachokiwaza ni faida tu na ndoto zisizo madhubuti. Kuwa Trader mzuri ndo kitu kinachotengeneza pesa sokoni na sio vinginevyo, mafanikio katika trading yanatokana na kua mjuzi na  mzoefu  wa ‘system’ yako na pia kua mzoefu na tabia yako ilivyo pale unapofanya maamuzi sokoni. Hivyo basi utaweza kufanya haya kwa kuzingatia kujifunza nasio kutengeneza faida na pia kuipenda kazi yako kwa kufanya mazoezi kama ‘backtesting’ n.k.

Je ? unahitaji kujifunza namna yakuwa Trader Bora atakaeweza kuishi kwa kutegemea trading kama chanzo chake namba moja cha kujiingizia mapato. Basi kama ni wewe bonyeza hapa kupata mafunzo ya Awali, bure kabisa leo hii.

Haya ndo machache Ambayo mtu yoyote akiyazingatia uko nje atafanikiwa na Trading. Ningependa kumuamsha mtu yoyote atake jiingiza kwenye biashara hii kuichukulia kwa uzito na umakini  kama kazi nyingine yoyote nasio kama Kamari yakukutajirisha haraka sana bila jitahada zozote.

FOREX TRADING TANZANIA Inawezekana!!

Sharing Is Caring
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
Subscribe
Notify of
guest
35 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
ray_heriel
2 months ago

Jiunge na Social Media Platform Kwa ajili ya Forex Traders Piptwitz Jifunze mengi kwa wengi https://piptwitz.com

Last edited 1 month ago by Profxtigers
Jack Concoius
Jack Concoius
1 year ago

Kwa mtu anaenza ukimwambia hivyo vitu ataona kama utani ila baada ya kupoteza hela na ndipo anaamka na kujua unuhimu wa hivyo vitu. Ni vitu muhimu sana kuzingatia haswa.

Profxtigers
Reply to  Jack Concoius
1 year ago

kweli Kabisa @jackConcoius

Eugene Sanga
1 year ago

Huwezi kufanikiwa na trading kama unachokiwaza ni faida tu na ndoto zisizo madhubuti. hii point ni nzuri sana Talking point. lazima tujifunze kwanza

Profxtigers
Reply to  Eugene Sanga
1 year ago

Exactly Mr.Eugene Sanga

Emanuel
Reply to  Eugene Sanga
1 year ago

Needs to start trading dear

Bilionea Asigwa
Bilionea Asigwa
1 year ago

Mbarikiwe sana
Nimejifunza kitu hapa

Profxtigers
Reply to  Bilionea Asigwa
1 year ago

Appreciate and welcome

Junior Kiterebu
Junior Kiterebu
1 year ago

Nimejifunza kitu Bro.!!Ubarikiwe mnooooooo

Profxtigers
Reply to  Junior Kiterebu
1 year ago

You Too, Thanks For passing by @Junior Kiterebu

Jesse
Jesse
Reply to  Profxtigers
1 year ago

Bro ahsante sana kwa ushauri aisee…
Kwa tunaotaka kuanza, una recommend tuanzie wapi?

Profxtigers
Reply to  Jesse
1 year ago

Anza kwa kujisomea kwanza upate basic knowledge, then ndo ufikirie kupata darasa.

Edfonce Akida
Edfonce Akida
1 year ago

Nashukuru sana mwalimu umenipa mwanga nasubiri tu darasa la mwanza lazma niwepo japo siishi mwanza

Profxtigers
Reply to  Edfonce Akida
1 year ago

Karibu Sana

Emily phillemon
Emily phillemon
1 year ago

” sijajiunga na hii biashara ila Nina one week nikitafuta taarifa za kunifanya nielewe kiasi kabla sijaianza,nikirelate na informations nilizokwishazipata, awesome content bro, unaongea ukweli .

Profxtigers
Reply to  Emily phillemon
1 year ago

appreciate

makagiveneth
makagiveneth
1 year ago

kk umekuwa mkweli sana.asante

Profxtigers
Reply to  makagiveneth
1 year ago

Asante sana

Exaud
Exaud
1 year ago

Asante sana kaka, points taken.

twahili
twahili
1 year ago

Mm pia nataka kuisomea hii biashara kaka sijui hata nafikaje darasan kwenu ila namba yangu hii,,-0714 3534 57

Emanuel madei
Emanuel madei
1 year ago

kaka Mimi kwa majina ni Emanuel madei, ni muda mrefu tangu nimesikia kuhusu forex trade na ningependa kuifanya hii biashara lakini sijui lolote kuhusu hii Biashara jinsi inavyofanywa, na napenda kujifunza naomba msaada wako, namba yangu ya simu 0653234785 / 0758969103
naomba msaada wako

Manasse Chief
Manasse Chief
11 months ago

Beginners, zingatieni haya. Ni ukweli mtupu, huwezi kuanza leo, ukafanikiwa leo, it took me 3 years to know what exactly forex is. A period in which I lost more than 25 M Tshs. In fact there’s a lot to learn, before you open a live accont and start trading. Forex is such a hard thing but highly profittable… For any new trader to become successful, there are three things that you need 1. Time for it ( you need enough time to learn and practise), fx can never be your after sth so tiring, coz it is an active learning.… Read more »

Profxtigers
Reply to  Manasse Chief
11 months ago

Thank you for this. New Traders have a good lesson to learn here.

Grace
Reply to  Manasse Chief
9 months ago

Uncle habari, naomba unielekeze ni bank gani tanzania naweza tumia kudeposit kwenye account ya forex, na aina ipi ya account nifungue kweny hiyo bank.

Profxtigers
Reply to  Grace
9 months ago

Habari Grace. Ili usipate usumbufu tumia Barclays Bank. Account Type Savings Plus.
Ambayo ina monthly charges ya Tzs 3500/=
Asante. Kwa Maelekezo zaidi Tuma Email Kwa support kwa msaada zaidi.

Grace
Reply to  Profxtigers
9 months ago

Habari, samahani nilitaka ufafanuzi zaidi ulipenedekeza bank ya barclays kwenye kudeposit/kuwithdraw kwa broker lakini inamakato makubwa ukilinganisha na bank ingine kama Equity bank. Je unashauri nitumue equity au bado unapendekeza barclays?. Msaada tafadhali.
Ahsante.

Profxtigers
Reply to  Grace
9 months ago

Kwanza kabisa inategemea na broker unae mtumia. Sina ufahamu na Equity ila ingekuwa ni vyema ukawauliza kama wana 3d Secured VISA ambayo ipo barclays. Mabroker wengi wanataka deposit itumike kwa 3D cards. Vilevile hutatumia Card zaidi ya kile ulicho deposit. Maana yake ni kwamba Kama ulideposit $300 kwa broker inamaanisha kwamba kiasi kile kile ndo kitarudi kupitia ile card, Faida ya juu au ziada itarudi kupitia Bank/Wire Transfer. Hata hivo mabroker sasa hivi wana mpesa ambayo ni haraka zaidi na nafuu kuliko bank. Broker Wa mpesa mzuri ni Tickmill tunaemtumia Link hii hapa TICKMILL OPEN ACCOUNT Vile vile ana customer… Read more »

Grace
Reply to  Profxtigers
3 months ago

Habari, naomba kufahamu hii bank transfer or bank wire inafanyika vp, na pia inagharama kiasi gani.
Ahsante.

ray_heriel
Reply to  Grace
3 months ago

Wire transfer inafanyika kupitia bank moja ka moja. Utaingia tickmill client area then utachagua bank transfer halafu utaweka kiasi kisha utapewa details za bank yao. Baada ya hapo utaenda bank yako utarequest wire transfer ifanyike kwenye hizo details ulizopewa kwenye client area. Asante

ray_heriel
Reply to  Grace
3 months ago

Unaweza kutembelea website yetu mpya social.profxtigers.com kwa msaada wa haraka zaidi

Herbert Mafundo
Herbert Mafundo
11 months ago

Mimi bado sijaelewa hata kidogo
0620231022

Annaniás
Annaniás
10 months ago

Nahitaji kujifunza forex na kuanzia trading ofisi zenu zipo wap?? Namba yangu ni 0762009367

Profxtigers
Reply to  Annaniás
10 months ago

Please send your credentials via email admin@profxtigers.com

Profxtigers
Reply to  Annaniás
10 months ago

make a booking

35
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x