NAMNA YA KUFANIKIWA NA BIASHARA YA FOREX KWA WAAJIRIWA WASIO NA MUDA WA KUTRADE KUTWA NZIMA.

Wengi huamini kuwa kupata mafanikio katika Biashara ya Forex Trading, ni lazima uwe Trader wakutwa nzima asiye na shughuli nyingine yoyote. Hii sikweli kabisa, biashara ya forex trading ni kwa mtu yoyote mwenye kujituma na mwenye nia ya dhati ya kufanikiwa.
Siwezi kushangaa ninapo ona traders wengi wanaamini hivyo kwamba kufanikiwa na forex trading lazima uwe mtu usiye na shughuli yoyote nyingine, hii ni kwasababu ya mfumo uliokuja kwa uvumi mkubwa wakutrade mara nyingi sana,kutwa nzima yaani (scalping).
Habari nzuri kwako, Katika Uzoefu wangu wa Forex Trading watu wanaofanikiwa Kirahisi na biashara hii ni wale wenye shughuli zakuwatinga kutwa nzima kiasi kwamba wanashindwa kufuatili kila PIP/POINT inayosogea kwenye Bei, kitu ambacho ni kikwazo cha Traders wengi kufanikiwa.
Traders wengi wanao fanya (scalping) Kutrade mara nyingi kutwa nzima hupata shida kufanikiwa kwasababu ya jinsi soko la forex lilivyo volatile na huendeshwa na Emotions za hali ya juu. kitendo cha kushinda kutwa nzima mbele ya kompyuta hua ni ngumu Sana kwa Traders kua na nidhamu ya kuto kuovertrade na kufuata mpango/strategy yake yakutrade.

Sasa basi twende moja kwa moja kwenye namna za mtu mwenye shughuli nyingi au mwaajiliwa anaweza kutrade forex na kufanikiwa!!!!

UFANYAJI ANALYSIS NA KUTRADE NEWYORK CLOSE DAILY CANDLES
Ninaposema Newyork close naamanisha mwisho wa Session Ya Newyork yaani kwa masaa ya Afrika mashariki ni saa sita kamili usiku. Pale ambapo, new York session inafungwa ndio muda muwafaka ukiwa umeshatoka kwenye michakato yako yakikazi, kufanya analysis na Kuweka order zako. Yote hii hufanywa kwa kutumia High timeframe kama zile za daily,kwa kusoma candlestick move ya mwisho ya Daily Timeframe. kama trader Unaye trade kupitia new York close candle unatakiwa kujifunza namna ya kufanya analysis na Higher timeframes na kuweza kujua direction ya soko kwa siku itakayo fuata. Ili kukuwezesha kutengeneza faida kwa siku au week nzima inayofuata bila kuhitaji kuwepo mbele ya kompyuta yako kutwa nzima.

Tuangalie mfano hapa chini

Ntajitahidi kukuelewesha kwa basic ndogo kabisa za forex Kama inavyonekana picha hapo juu kitendo cha kuweza kutambua soko unalotrade likoje kwa muda huo.
Mfano wa DAILY CHART hii Soko hapo ju ni Soko linalo RANGE/CONSOLIDATE, na kwa uwepo kwa candlestick pattern nilizo zizungushia maduara hapo juu unaweza kujua movement ijayo ya price inaelekea wapi izo candlestick patterns ni candle za rejection zinazo ashiria kugeuka kwa soko na kwamba soko litaelekea kwenye either supply or demand level, kwaio trader haitaji kuwepo kutwa nzima kwenye screen bali tu mara moja kwa siku, saa sita usiku pale candle inapofungua ya NEWYORK CLOSE.

Niwazi kwakufanya hayo tu haitokuku akishii mafanikio yako sokoni lakini kwa urahisi wakukuelewesha unaweza ukawa mtu ulie ajiliwa au unashughuli nyingi na pia ukafanikiwa Zaidi hata ya wale ambao wapo mbele ya screen kutwa nzima maana Kwenye biashara ya forex hautengenezi pesa kwa kutrade mara nyingi Zaidi bali kwa kuweza kujua ni fursa zipi nzuri kuzichukua kwa uchache ili ufanikiwe nazo nakutengeneza faida Kwenye Programu yangu wa mentorship nawafundisha wanafunzi wangu mbinu mbali mbali zakungundua ni fursa gani ina uwezekano mkubwa Zaidi wakutengeneza nazo.

KUTRADE NA KUSAHAU
Kama nilivyo onesha hapo juu kwenye picha NEWYORK candle close hutokea kila baada ya masaa 24 hivyo basi ukitumia mbinu hiyo itakurahisishia kutrade nakusahau. Na njia yakufanikiwa sokoni ni kwa kutrade na kusahau. Hutoweza kutrade na kusahau kama unachokifanya ni kurisk pesa yote na kutrade bila mpango au strategy, maana utakua hujui unataka nini sokoni hivyo kila point/pip itakayo sogea kwako ita kua na uzito mkubwa mwishowe utajimaliza na kutrade na emotions za hali ya juu. Hivyo basi kupitia nakala hii nilitaka kukuelezea ni jinsi gani unaweza kutrade hili soko ukafanikiwa ingawa ya kua mtu ulie na ubize wa hali ya juu.
Jifunze njia yangu ninayoitumia kutrade kwa uchache na kwa mafanikio ya hali juu kwa Kuchuja Fursa zipi zenye uwezekano mkubwa wa faida kwa kubonyeza HAPA

NAKUTAKIA KILA LA KHERI, NA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA HII YA FOREX TRADING, KWAHERI TAFADHALI TOA MAONI YAKO HAPO CHINI NINGEPENDA KUSIKIA KUTOKA KWAKO

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Most Voted
Newest Oldest
Inline Feedbacks
View all comments
Mathew
Mathew
1 year ago

Asante Moki Jr….nakubaliana na wewe…swing trader wanahitaji kids mchache Wa kuwa sokoni na ana uwezo Wa kupata faida kubwa kama analysis yake itakuwa correct.

gilead
gilead
1 year ago

I have been browsіng on-line more than 3 hours lately, yet I never found any attention-ɡrabbing
article ⅼike yours. It’s pretty price enouցh for me.
In my oрinion, if all webѕite owners and bloɡgers made exceⅼlent content as you did,
the net mіght be a lot more helpful than ever before.

cat hat
cat hat
1 year ago

Fantastic site you have here but I was curious about if you knew of any user discussion forums that cover
the same topics discussed in this article?
I’d really like to be a part of community where I can get comments from
other experienced individuals that share the same interest.
If you have any recommendations, please let me know. Thanks a
lot!

cat hat
cat hat
1 year ago

I like the efforts you have put in this,
thank you for all the great content.

GIDEON CHAO
GIDEON CHAO
1 year ago

nice

Jane chonya
Jane chonya
1 year ago

Habari
Je unatoa mafunzo ya hii biashara
Utaratibu ukoje

7
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x