FOREX TRADING TANZANIA, YAFAHAMU HAYA KABLA YA KUJIINGIZA KWENYE HII BIASHARA.

Habari,

Ndugu waTanzania Mimi nikiwa kama mdau na miongoni Mwa Wa Tanzania wachache Walio wahi kuanza na kuyaona Mafanikio ya hii sekta mpya hapa nchini ya Forex trading, leo hii nimeona kuna ulazima wa kuandika Makala hii kumsaidia Mtazania yoyote uko nje atakae au anaye tamani kujiingiza kwenye hii biashara. Waweza jiuliza kwa nini nachukua jukumu hili, mafanikio katika sekta hii sio rahisi kama inavyo onekana kwenye mitandao yakijamii na haswa kwa jinsi Forex Trading Tanzania ilivyo letwa, safari yangu ya mafanikio haikua rahisi, ilikua ni safari ya maumuvi makali ya kupoteza pesa yalio nilipelekea matatizo chungu nzima ambayo haina maana ya kuyaweka hapa, zaidi ya ambacho nataka ukifahamu.

Hivyo basi nimeona nifanye hivi kama njia moja wapo yakurudisha au kutoa kwa jamii bure kabisa kumsaidia yule anayeanza au ambae yupo safarini kuelekea mafanikio kwenye hii sekta, ili kuepukana na matatizo makubwa niliyo yapitia na kumsaidia kuyaona mafanikio kwa urahisi Zaidi.

Kama ningekua na mashine ya kurudisha muda nyuma, niwe mimi yule mgeni wa forex trading miaka miwili  iliyopita, ningefanya hivyo ili tuu niwe na haya ninayo yafahamu leo kwa hakika ingenirahisisha  nakuongeza spidi ya mafanikio yangu na ningeyapata kwa haraka Zaidi. Lakini kibaya ni kwamba hakuna mashine kama hiyo lakini kwa wewe unaenza sasa hii nikama lulu kwako hivyo basi hivi ndo vitu vitano ambavyo ningevijua mwanzoni naamini  kwa asilimia mia moja ningefanikiwa mapema Zaidi.

MATUMIZI YA INDICATORS NI UPOTEVU WA MUDA.

Hiki ni kitu ambacho kingeniokoa na upotevu wa muda mrefu na kuumiza kichwa, kama ninge gundua kama indicators ni upotevu wa muda mkubwa na ingepunguza muda wa mahangaiko yakujifunza. Sasa hii ni fursa ya wewe kuepukana na hiki kitu, najua mwanzoni zinaweza zikaonekana kama ni ujanja pale ukionesha marafiki na jamaa platform yako imejaa mistari mingi ya indicators lakini nakuhakikishia ni sawa nakujichimbia kaburi hatua kwa hatua jinsi kila siku unavyoendelea kuzitumia.

Kama umengundua mpaka sasa indicators zimetokana na Mjumuiko wa vigezo vya PRICE ACTION  hivyo basi kwanini uzitumie wakati unaweza tumia price action moja wa kwa moja.. Mafaniko kwenye hii sekta yanatokana na kuweka mambo kiurahisi yaani kupunguza vigezo vingi vinavyofanya ufanye maamuzi ya kununua na kuuza na sio vinginevyo. Mafaniko yangu yalianza kuoneka pale nilipo anza kutumia PRICE ACTION.

Kweli kabisa ‘moving averages’ zinausaidizi haswa kwa wageni na hii biashara kungundua ‘Support na resistance levels’ na Trend, ukweli ni kwamba kutoa Moving averages sioni umuhimu wa kutumia indicators na ahata hizi Moving averages zisitumii kabisa skuizi ni natumia PURE PRICE ACTION maana nimeshajenga uzoefu wa hali ya juu.

Kama hutoweza kutumia pure price action basi sahau mafanikio ya forex, Utabaki kua kama wale wadau WA FOREX TRADING TANZANIA wanao poteza pesa zao kila kukicha Na hivyo ndivyo ninavyo wafundisha wanafunzi wangu darasani.

NIRAHISI KU OVERTRADE KULIKO UNAVYO FIKIRIA.

Kitu ambacho niligundua baada ya kuwa mzoefu kwenye biashara hii siku za mwanzoni nilikua na overtrade na hata siku gundua na fanya hilo.

Nirahisi kutafuta visingizio vya trades unazochukua kwa wingi (kwaku overtrade). Lakini jibu kamili nikwamba je ime timiza vigezo vyako vya kutrade yaani (strategy)

Overtading nikitendo cha kuchukua trade nje ya strategy yako na niamini mimi, sio jambo gumu sana kufanya kwenye hii biashara, haswa kwa Traders wageni na nijambo ambalo lina umiza sana na kurudisha nyuma hatua zako zakimafanikio.

MATUMIZI YA TIMEFRAME NDOGO NI HATARI

Ukiangalia kwa makini hizi points zote zinaingiliana kwa mfano overtrading inasababishwa nakuangalia timeframe ndogo kama zile chini ya ‘1HOUR’,  laiti kama ningerudi nyuma kipindi nikiwa mgeni na forex ningejieleza haswaa  umuhimu wa matumizi ya timeframe za juu. Matumizi ya timeframe za chini yatakupelekea kuovertrade kwa sababu utahisi unaona fursa nyingi sokoni wakati kiukweli izo ni kele tu za soko. Kirahisi ni kwamba fursa zinazo patika timeframe za juu zina Asimilia kubwaa Zaidi ya kukutengenezea faida kuliko zile zinazo patikana timeframe za chini.

HUWEZI KUZUIA HASARA KABISA.

Inafurahisha sana unakuta traders wengi wanahangaika kuzuia hasara wakati ni jambo ambalo haliwezekani kuzuia hasara kabisa bali unaweza tu kuzipunguza kwa kufuata “system” yako.

Kama unafanya mambo kama haya:  trading bila stoploss, kusogeza stoploss kwenda breakeven mapema sana, kuchukua faida ndogo ndogo kulinganisha na hasara zako yaani kwa kifupi ni unajaribu kuepusha hasara na hicho nikitu kibaya rafiki yangu.

ZINGATIA KWENYE KUJIFUNZA NASIO KUTENGENEZA FAIDA UNAPOANZA TRADING.

Najua wengi wanao ni follow kwenye mitandao yakijamii watachukizwa nahili jambo lakini ni ukweli mtupu. Huwezi kufanikiwa na trading kama unachokiwaza ni faida tu na ndoto zisizo madhubuti. Kuwa Trader mzuri ndo kitu kinachotengeneza pesa sokoni na sio vinginevyo, mafanikio katika trading yanatokana na kua mjuzi na  mzoefu  wa ‘system’ yako na pia kua mzoefu na tabia yako ilivyo pale unapofanya maamuzi sokoni. Hivyo basi utaweza kufanya haya kwa kuzingatia kujifunza nasio kutengeneza faida na pia kuipenda kazi yako kwa kufanya mazoezi kama ‘backtesting’ n.k

Haya ndo machache Ambayo mtu yoyote akiyazingatia uko nje atafanikiwa na Trading. Ningependa kumuamsha mtu yoyote atake jiingiza kwenye biashara hii kuichukulia kwa uzito na umakini  kama kazi nyingine yoyote nasio kama Kamari yakukutajirisha haraka sana bila jitahada zozote.

FOREX TANZANIA Inawezekana!!

Sharing Is Caring
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
avatar
13 Comment threads
18 Thread replies
3 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
18 Comment authors
ray_ herielGraceGraceAnnaniásHerbert Mafundo Recent comment authors
  Subscribe  
newest oldest most voted
Notify of
Jack Concoius
Guest
Jack Concoius

Kwa mtu anaenza ukimwambia hivyo vitu ataona kama utani ila baada ya kupoteza hela na ndipo anaamka na kujua unuhimu wa hivyo vitu. Ni vitu muhimu sana kuzingatia haswa.

Tudor

kweli Kabisa @jackConcoius

Eugene Sanga
Member
Eugene Sanga

Huwezi kufanikiwa na trading kama unachokiwaza ni faida tu na ndoto zisizo madhubuti. hii point ni nzuri sana Talking point. lazima tujifunze kwanza

Tudor

Exactly Mr.Eugene Sanga

Emanuel
Guest

Needs to start trading dear

Bilionea Asigwa
Guest
Bilionea Asigwa

Mbarikiwe sana
Nimejifunza kitu hapa

Tudor

Appreciate and welcome

Junior Kiterebu
Guest
Junior Kiterebu

Nimejifunza kitu Bro.!!Ubarikiwe mnooooooo

Tudor

You Too, Thanks For passing by @Junior Kiterebu

Jesse
Guest
Jesse

Bro ahsante sana kwa ushauri aisee…
Kwa tunaotaka kuanza, una recommend tuanzie wapi?

Tudor

Anza kwa kujisomea kwanza upate basic knowledge, then ndo ufikirie kupata darasa.

Edfonce Akida
Guest
Edfonce Akida

Nashukuru sana mwalimu umenipa mwanga nasubiri tu darasa la mwanza lazma niwepo japo siishi mwanza

Tudor

Karibu Sana

Emily phillemon
Guest
Emily phillemon

” sijajiunga na hii biashara ila Nina one week nikitafuta taarifa za kunifanya nielewe kiasi kabla sijaianza,nikirelate na informations nilizokwishazipata, awesome content bro, unaongea ukweli .

Tudor

appreciate

makagiveneth
Guest
makagiveneth

kk umekuwa mkweli sana.asante

Tudor

Asante sana

Exaud
Guest
Exaud

Asante sana kaka, points taken.

twahili
Guest
twahili

Mm pia nataka kuisomea hii biashara kaka sijui hata nafikaje darasan kwenu ila namba yangu hii,,-0714 3534 57

Emanuel madei
Guest
Emanuel madei

kaka Mimi kwa majina ni Emanuel madei, ni muda mrefu tangu nimesikia kuhusu forex trade na ningependa kuifanya hii biashara lakini sijui lolote kuhusu hii Biashara jinsi inavyofanywa, na napenda kujifunza naomba msaada wako, namba yangu ya simu 0653234785 / 0758969103
naomba msaada wako

Manasse Chief
Guest
Manasse Chief

Beginners, zingatieni haya. Ni ukweli mtupu, huwezi kuanza leo, ukafanikiwa leo, it took me 3 years to know what exactly forex is. A period in which I lost more than 25 M Tshs. In fact there’s a lot to learn, before you open a live accont and start trading. Forex is such a hard thing but highly profittable… For any new trader to become successful, there are three things that you need 1. Time for it ( you need enough time to learn and practise), fx can never be your after sth so tiring, coz it is an active learning.… Read more »

Tudor

Thank you for this. New Traders have a good lesson to learn here.

Grace
Member
Grace

Uncle habari, naomba unielekeze ni bank gani tanzania naweza tumia kudeposit kwenye account ya forex, na aina ipi ya account nifungue kweny hiyo bank.

Tudor

Habari Grace. Ili usipate usumbufu tumia Barclays Bank. Account Type Savings Plus.
Ambayo ina monthly charges ya Tzs 3500/=
Asante. Kwa Maelekezo zaidi Tuma Email Kwa support kwa msaada zaidi.

Grace
Member
Grace

Habari, samahani nilitaka ufafanuzi zaidi ulipenedekeza bank ya barclays kwenye kudeposit/kuwithdraw kwa broker lakini inamakato makubwa ukilinganisha na bank ingine kama Equity bank. Je unashauri nitumue equity au bado unapendekeza barclays?. Msaada tafadhali.
Ahsante.

Tudor

Kwanza kabisa inategemea na broker unae mtumia. Sina ufahamu na Equity ila ingekuwa ni vyema ukawauliza kama wana 3d Secured VISA ambayo ipo barclays. Mabroker wengi wanataka deposit itumike kwa 3D cards. Vilevile hutatumia Card zaidi ya kile ulicho deposit. Maana yake ni kwamba Kama ulideposit $300 kwa broker inamaanisha kwamba kiasi kile kile ndo kitarudi kupitia ile card, Faida ya juu au ziada itarudi kupitia Bank/Wire Transfer. Hata hivo mabroker sasa hivi wana mpesa ambayo ni haraka zaidi na nafuu kuliko bank. Broker Wa mpesa mzuri ni Tickmill tunaemtumia Link hii hapa TICKMILL OPEN ACCOUNT Vile vile ana customer… Read more »

Herbert Mafundo
Guest
Herbert Mafundo

Mimi bado sijaelewa hata kidogo
0620231022

Annaniás
Guest
Annaniás

Nahitaji kujifunza forex na kuanzia trading ofisi zenu zipo wap?? Namba yangu ni 0762009367

Tudor

Please send your credentials via email admin@profxtigers.com

Tudor

make a booking